Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kama wapo viongozi wanaonunua viongozi wengine hilo ni tatizo kubwa kweli kweli, lakini cha kujiuliza wanafanya hivyo ili iweje katika hatua ya juu kabisa? na katika mazingira kama hayo , expectation yao ni ili mwisho iwe nini?
Haya, Hao wanaohongwa ni wapinzani (ndio mbadala). Wanahongwa milioni mbili wanaachana na uongozi. Mara wanatamani kuhongwa ajira za ualimu (sifa wanazo za kuwa waalimu by competence lakini wanafikiri wanatakiwa wapate by favoritism). Mbona viongozi hawa wanakuwa na "Low expectation" kiasi hiki jamani?
Haya ukirudi kwa upande mwingine; sisi sote tumeweka matumaini yetu yote kwa makundi tajwa hapo juu. Sasa fikiria ni nini hatma yetu?
Wakuu; Tatizo letu watanzania ni kufikiri. Tuna tatizo kubwa sana kwenye namna tunavyofikiri na nilazima tulielewe hili na kulikubali kwanza. Tuna "Very low expectation & vision". Wanaokuwa viongozi kwenye vyama na mwishowe kwenye nchi wanatokana na sisi, kwa hiyo vile walivyo, ni reflection ya tulivyo.
Enyi watu mnaoamini mna uelewa mzuri, mna dhamira njema, ni waadilifu, mna maono mapana, wazalendo na mmejaa utu ndani yenu; Acheni kukaa kimya bila kusema wala kufanya chochote na kuacha mambo yawe yatakavyokuwa kama vile hamuhusiki wala hamuwajibiki kwa vyovyote vile. Tutaelekea shimoni kweli nawaambieni. Tushirikianeni kwanza kuboresha namna tunavyofikiri na kuwasaidia wengine kufanya hivyo hivyo ili kutoka miongoni mwetu, tuweze kuwa na viongozi wenye vision pana ambao watakuwa ni msaada zaidi kwetu na kwa nchi yetu baadae.
Suala la chama gani kinashinda uchaguzi halina maana ikiwa watu ni wale wale na wote wana matatizo yale yale na mawazo na expectations za namna ile ile.
Naombeni mnielewe tafadhali!