Tunadanganyana sana juu ya mambo haya (TUBADILIKE)

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
1.Ningeweza kufanya kama Ningekuwa na pesa
Japokuwa asilimia kubwa ya sentensi nyingi zinazoanzia na hilo neno hapo juu huwa kweli,
(mfano: ningekuwa na fedha ningenunua kisiwa nikae huko na familia yangu) lakini Muda mwingi watu wengi tumekuwa tunasingizia kukosa fedha hata kama hatukutimiza wajibu wetu!
Wengi huamini fedha ndio kila kitu katika maisha yao. Hata kama wangekuwa na uwezo wa kufanya suala Fulani bila ya fedha, huliacha bila hata ya kujaribu na kuona haliwezekani bila ya fedha!
“Money without brains is always dangerous”

2.Siwezi Kuishi Bila Yeye
Inaweza kuonekana ni ngumu lakini kila binadamu ameumbwa akiwa na utashi wake, na ukamilifu wa kuweza kuyaendesha maisha yake. Kinacholeta tofauti hapo ni namna gani umeuzoeza mwili/ mawazo yako kumtegemea mtu Fulani.Japokuwa siku zote tunaogopa kumkosa mtu huyo, cha ajabu ni kwamba, tunapomkosa tunakaa muda flani tu na kusahau yote licha ya kuvunjika moyo hapo kabla, na kuhisi moyo wako umenyofolewa kitu ambacho hakitarudi tena.

3. Nimeshazeeka Siwezi kufanya hili/ Umri wangu Bado!
Kwa utafiti mdogo, Nimegundua kuwa waafrika wengi husubiri wafike miaka 30 ndipo waanze kuvaa majukumu mengi (mfano Kuwa na familia, kujenga, kununua ardhi, usafiri nk) Na je umegundua kwamba wakifika umri wa miaka 40 hujiona wazee na kukata tama na kutojihusisha na kujifunza vitu vipya? “mambo ya vijana hayo”Na watu wengi wenye miaka zaidi ya 50 hujiona wamechelewa na teknolojia imeshawapita, kumbe maisha yamerahisishwa! Kama uliweza kujifunza mambo mengi magumu ambayo mpaka unajisifu kwamba vijana wengi wa sasahivi hawayawezi, kwa nini uogope kujifunza kutumia kompyuta, mitandao au simu za kisasa? Hujachelewa anza sasa!
4. Ntajaribu/Ntaonja Kidogo Tuuu!
Shauri yako!

5.Laiti ningekuwa na muda ninge…
Pengine unayawaza haya huku umekaa sebuleni, ni asubuhi na bado unanguo za kulalia, unaangalia darini ukiwaza ungekuwa na muda ungefanya moja, mbili, tatu! Mara Nyingi Tumekuwa Tukipoteza Muda wetu mwingi Tukiandaa orodha ya mambo ambayo Tungeyafanya kama tungekuwa na Muda!
6.Mimi naliweza hili sio lile (am good at this, not that!)
Pengine Kwa kuogopa Kudhubutu Wengi wetu Huamini kwamba uwezo wetu ni katika mambo kadhaa tu, na aina Fulani ya majukumu ni kwa ajili ya watu Fulani. Na mimi naweza kitu Fulani mpaka awepo mtu Fulani!
7. Kesho
Hakuna neno la uongo kama neno “kesho” wengi wetu huwa wavivu na kujipa moyo kwa kuwa tu kuna kesho! Tutaacha viporo vya kazi, masomo n kusahau kwamba kesho bora ni ile itakayozalisha kitu chake na si itakayofanya mambo ya leo!

8. Kuhisi Mapungufu yetu tunayajua wenyewe!
Wajua mtu wako wa karibu sana anayajua mapungufu yako pengine kuliko wewe? Wengi wetu huwa tunajiona tuko sawa upande Fulani na kuhisi mapungufu yetu tunayajua wenyewe! Hii husababisha kutokukubali kama tumekosea na kwamba tunamapungufu katika hilo!.Ukweli ni kwamba, ukiona mtu zaidi ya mmoja anakueleza juu ya tatizo lako Fulani, hata kama unajihisi huna tatizo upande huo, jaribu kubadilika!

9. NAJUA NINACHOKIFANYA!!
Haya bwana!… Ndio unajua, niseme nini tena!
10. Sio Hadhi yangu!
Pengine kwa kuhisi unamapungufu Fulani basi huwezi hata kujaribu kufanya jambo Fulani au una uwezo Fulani basi kwa hili sio hadhi yangu, wanastahili hadhi ya chini sio mimi.!
SI KWELI. BADILIKA.
 
Well said.
Umesahau neno "NINGEJUA" hili pia linakuja sana baada ya mtu kukosea badala ya kusema "SASA NAFANYA HIVI" (Baada ya kutambua kosa) anabaki kujutia tu.
 
Well said.
Umesahau neno "NINGEJUA" hili pia linakuja sana baada ya mtu kukosea badala ya kusema "SASA NAFANYA HIVI" (Baada ya kutambua kosa) anabaki kujutia tu.
Kabisa mkuu umenena vyema sana,
 
Hio namba 3 ipo sana Mkoa wa lindi. Yaan uvivu wa kazi na kufikiri, mtu akifika miaka 25 ana mtt ana miaka kumi au kumi na moja basi utamkuta hajielewiii eti anajiona mzee anasubir kuwa bibi. Lol
 
Back
Top Bottom