CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,357
- 6,422
Nimefuatilia maoni ya wadau humu JF kuhusu ufisadi, the bottomline ni kuwa wachangiaji wengi wana maoni ya wivu wa kimaskini na siyo uzalendo kutoka rohoni. Mtu anasema afadhali akanyee ndoo, inakusaidia nini katika shida zako Kitilya akinyea ndoo. Mara nyingi masikini kama sisi tunafurahia mwenye nacho akikosa na siyo nifanye kazi niwe kama yeye au kumzidi. NAJIULIZA: Sisi masikini tukipata nafasi nyeti zenye fedha kama za TRA, Bandarini, and the like na hatukuwekewa udhibiti kama ilivyokuwa utawala wa JK, tutakuwa waaminifu?