Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Tunachofikiri ndio tunachozalisha. Sisi ni zao la akili na mawazo yetu wenyewe. Aina ya taifa letu ni zao la mawazo yetu wenyewe liwe zuri au baya. Taifa hili tutalijenga kwa akili zetu wenyewe. Inategemea tuna busara na hekima kiasi gani. Tutalijenga taifa hili kulingana na akili zetu na tutalibomoa hivyo hivyo kulingana na akili zetu ni za kipuuzi kwa kiwango gani. Hakuna kinachokuja kwa bahati mbaya. Majaliwa ya binadamu yanatokana na matendo yake mwenyewe.
Umaskini wetu kama taifa hakuna mtu wa kumlaumu. Uwezo wa kuondoa umaskini huu uko chini ya nguvu zetu.
Kama tu wadhaifu sana kuuondoa au tumekosa maarifa ya kufanya hivyo au utashi wa kuuondoa hilo ni juu yetu pia.
Lakini nguvu ya kuuondoa tunayo lakini imelala au inatumika katika mambo yasiyo na manufaa.
Au pengine sababu ya migawanyiko yetu. Au kwa kutenda au kutokutenda kwetu na kwa tabia na aina ya fikra tulizonazo. Na pengine kukosa nidhamu na dira ya pamoja na muelekeo ili tupeleke nguvu zetu huko.
Sent using Jamii Forums mobile app