Tunaanza kuipima nguvu ya Freeman Mbowe (Chadema) kupitia Kamati teule ya Jaji Mutungi. Ni Katiba mpya vs Tume Huru!

Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya Panya kwa Mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.
Cha kushangaza Zitto naye ameingia kwenye kundi la wajinga.

Yule Jecha aliyempora ushindi Maalim Seif na kufuta uchaguzi alikuwa akiongoza tume huru ya Zec.
 
Wanasiasa zungukeni wee lakini mwisho wa siku katiba mpya tutaandika sisi wananchi wanyonge tena kwa wino wa damu.
Haki siku zote haiombwi inapiganiwa
Sio lazima katiba mpya ndo tulete mageuzi. Misingi ya kweli ya kizalendo ya akina kinjekitile ngwale tutaifuata. Hayo mengine ni uzushi tuu na viini macho
 
U
Tume huru itashinda, katiba mpya kabla ya 2025 ni ndoto ya mchana. Tumewashauri saaaaana CDM kwenye hili, lakini sikio la kufa halisikii dawa
Umoja wakitaifa utazidi kuteteleka zaidi na zaidi.
Engine ya gari kwanza ndipo ujenge bodi ya gari
Sasa bodi ya gari halafu injini,utapachikaje? Zitaanza welding nyingi.
KATIBA MPYA =TUME HURU YA UCHAGUZI.
Huwezi ijadili tume huru ya uchaguzi huku Luna sheria zinazompa mamlaka mkuu wa Nchi kuteua maafisa wa Tume.
 
Nimeipitia orodha ya wajumbe 23 wa kamati iliyoundwa na msajili wa vyama vya siasa kupitia mapendekezo ya kikao cha wadau wa vyama vya siasa ambayo kimsingi yalijikita uundwaji Tume Huru ya Uchaguzi.

Nimezisikia pia salamu za mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe aliyeko mahabusu ambazo kimsingi zimejikita kwenye mapambano ya kudai Katiba Mpya.

Tulipofika ni patamu.

Ukitaka Katiba Mpya unakwenda na Mwamba.

Ukitaka Tume Huru ya Uchaguzi unakwenda na Mutungi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana.
Mtungi ni kibaraka wa CCM hakuna tume huru itakayoundwa na wanaccm na vibaraka wao
 
Nimeipitia orodha ya wajumbe 23 wa kamati iliyoundwa na msajili wa vyama vya siasa kupitia mapendekezo ya kikao cha wadau wa vyama vya siasa ambayo kimsingi yalijikita uundwaji Tume Huru ya Uchaguzi.

Nimezisikia pia salamu za mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe aliyeko mahabusu ambazo kimsingi zimejikita kwenye mapambano ya kudai Katiba Mpya.

Tulipofika ni patamu.

Ukitaka Katiba Mpya unakwenda na Mwamba.

Ukitaka Tume Huru ya Uchaguzi unakwenda na Mutungi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana.
Huwezi ukatenganisha katiba mpya na tme huru ya uchaguzi. Tume huru ni moja ya mada za katiba mpya. Lengo la Mtungi ni kuchelewesha mchakato wa katiba mpya kwa kupotosha.
 
Tume huru itashinda, katiba mpya kabla ya 2025 ni ndoto ya mchana. Tumewashauri saaaaana Chadema kwenye hili, lakini sikio la kufa halisikii dawa

Lakini bila katiba mpya huwezi kuwa na tume huru labda kama hujuwi kwamba tume itatokana na hiyo katiba inayomfanya Rais kuwa dikteta. Kama kuna Rais ambaye katiba imemfanya dikteta atashindwaje kuivuruga hiyo tume hata ikiundwaje.
 
Nimeipitia orodha ya wajumbe 23 wa kamati iliyoundwa na msajili wa vyama vya siasa kupitia mapendekezo ya kikao cha wadau wa vyama vya siasa ambayo kimsingi yalijikita uundwaji Tume Huru ya Uchaguzi.

Nimezisikia pia salamu za mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe aliyeko mahabusu ambazo kimsingi zimejikita kwenye mapambano ya kudai Katiba Mpya.

Tulipofika ni patamu.

Ukitaka Katiba Mpya unakwenda na Mwamba.

Ukitaka Tume Huru ya Uchaguzi unakwenda na Mutungi.

Mungu wa mbinguni awabariki sana.
Tunataka katiba mpya yenye tume huru
Ccm laghai inaona afadhali ya tume huru kuliko katiba mypya, watabana wataachia tu
 
Back
Top Bottom