Tunaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania au wa Tanganyika?

dega

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
3,138
3,042
Mbona mnatuchanyanya hivi mkisema Miaka 60 ya UHURU wa TANZANIA mnakusudia hii Tanzania iliyozaliwa 64 au kuna nyengine?

Hivi waandishi wa habari na wanasiasa mnaosema UHURU WA TANZANIA hivi kweli hamjui historia yenu? Kwanini munainyanyapaa TANGANYIKA kiasi hiki?

Historia itabakia ni historia tuu hata mkitumia nguvu kiasi gani kuipotosha

Au Mimi ndio sifahamu haya mambo? Kama NI hivyo nielewesheni ni Tanzania gani iliyopata UHURU 1961?

Ni haya tu
 
Tanganyika Nyerere aliiflashi chooni mwaka 1964. Haipo tena. Angalia kwenye Atlas leo, Tanganyika haipo tena, angalia Google maps huoni Tanganyika.
 
Miaka 60 ya uhuru wa SISIYEMU madarakani wenye kuleta mateso na umasikini kwa watanzania. Huku ukijinufaisha wao na wachache kati yao katika kuhakikisha wanaendelea kusalia madarakani kufurahia mema ya nchi.
 
Ni Uhuru wa Tanzania bara

Jina lilibadlishwa kisheria kuwa Tanzania Kama wewe unavyoweza badili jina tukasema Leo birthday ya Juma jina lako jipya baada ya kuslimu ukubwani na kubadili jina la asili la Chapombe na kuitwa Juma badala ya kuendelea nalo jina la Chapombe msikitini

Ni Uhuru wa Tanzania bara

Ila Zanzibar huwa hawataki Hilo wao huadhimisha uhuru.wa Zanzibar sio wa Tanzania visiwani!

Linatakiwa kuongeza neno bara nyuma kuwa ni uhuru wa Tanzania bara
 
Ni Uhuru wa Tanzania bara

Jina lilibadlishwa kisheria kuwa Tanzania Kama wewe unavyoweza badili jina tukasema Leo birthday ya Juma jina lako jipya baada ya kuslimu ukubwani na kubadili jina la asili la Chapombe na kuitwa Juma badala ya kuendelea nalo jina la Chapombe msikitini

Ni Uhuru wa Tanzania bara

Ila Zanzibar huwa hawataki Hilo wao huadhimisha uhuru.wa Zanzibar sio wa Tanzania visiwani !!!

Linatakiwa kuongeza neno bara nyuma kuwa Ni uhuru wa Tanzania bara
HAKUNA jina liliobadilishwa.

Hiyo Tz ni jina la muungano wa nchi 2
 
Kama ni Tanzania sherehe ziwe pande zote mbili,kwa tafsiri ya Tanzania
Tanzania bara mgeni Rasmi anatakiwa kuwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa Kama ambavyo Zanzibar kusherehekea Uhuru wao mgeni Rasmi huwa Raisi wa Zanzibar sio wa muungano
 
Ni Uhuru wa Tanzania bara

Jina lilibadlishwa kisheria kuwa Tanzania Kama wewe unavyoweza badili jina tukasema Leo birthday ya Juma jina lako jipya baada ya kuslimu ukubwani na kubadili jina la asili la Chapombe na kuitwa Juma badala ya kuendelea nalo jina la Chapombe msikitini

Ni Uhuru wa Tanzania bara

Ila Zanzibar huwa hawataki Hilo wao huadhimisha uhuru.wa Zanzibar sio wa Tanzania visiwani !!!

Linatakiwa kuongeza neno bara nyuma kuwa Ni uhuru wa Tanzania bara
Hatukuwahi kuwa na Tanzania bara miaka 60 iliyopita hivyo tunachoadhimisha ni Uhuru wa Tanganyika.

Msijaribu kubadilisha historia kwa manufaa yenu binafsi.
 
Hatukuwahi kuwa na Tanzania bara miaka 60 iliyopita hivyo tunachoadhimisha ni Uhuru wa Tanganyika.

Msijaribu kubadili have historia kwa manufaa yenu binafsi.
Sawa Ni Uhuru wa Tanganyika mgeni rasmi anatakiwa kuwa waziri mkuu Kassim Majaliwa sababu Uhuru wa nchi hizi mbili sio Jambo la muungano .Raisi wa muungano hayamhusu .Yeye anatakiwa kuwa mgeni rasmi sherehe ya muungano tu na sio sherehe ya Uhuru wa Tanganyika au Zanzibar

Una hoja
 
Ni Uhuru wa Tanzania bara

Jina lilibadlishwa kisheria kuwa Tanzania Kama wewe unavyoweza badili jina tukasema Leo birthday ya Juma jina lako jipya baada ya kuslimu ukubwani na kubadili jina la asili la Chapombe na kuitwa Juma badala ya kuendelea nalo jina la Chapombe msikitini

Ni Uhuru wa Tanzania bara

Ila Zanzibar huwa hawataki Hilo wao huadhimisha uhuru.wa Zanzibar sio wa Tanzania visiwani !!!

Linatakiwa kuongeza neno bara nyuma kuwa Ni uhuru wa Tanzania bara
Tanzania Bara ya chato labda, acheni upotoshaji
 
Kuna siku wajukuu zetu watahoji ipo wapi Tanganyika yao sijui tutawajibuje wakati huo tutakuwa hatuna meno mdomoni.
 
Mbona mnatuchanyanya hivi mkisema Miaka 60 ya UHURU wa TANZANIA mnakusudia hii Tanzania iliyozaliwa 64 au kuna nyengine?

Hivi waandishi wa habari na wanasiasa mnaosema UHURU WA TANZANIA hivi kweli hamjui historia yenu? Kwanini munainyanyapaa TANGANYIKA kiasi hiki?

Historia itabakia ni historia tuu hata mkitumia nguvu kiasi gani kuipotosha

Au Mimi ndio sifahamu haya mambo? Kama NI hivyo nielewesheni ni Tanzania gani iliyopata UHURU 1961?

Ni haya tu
Tunaadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania, japo iliyopata uhuru ni Tanganyika. Kwa vile Tanganyika doesn't exist anymore, kilichopo ni Tanzania.
P
 
Back
Top Bottom