Tuna vitabu vya hotuba tele za Rais Julius Nyerere. Je, hotuba za maraisi waliomrithi zina tatizo?

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
500
Hotuba za Rais Julius Nyerere zimekusanywa kwenye vitabu kadhaa. Ni nyingi yaani hata kusoma headlines tu inachosha. Hotuba zake zingine zinaruswa kwenye kipindi cha Usia wa Baba.

Binafsi nikisikia hta htouba moja huwa ninasimama hata kama ni kile kipande cha kutoa vichekesho.

Wako wanaopata PhD. kwa kuchambua hotuba za Julius Nyerere, tena wakati mwingine nasikia akina Shivji wametafuta hata maandishi yake binafsi na kuyachambua, tena akiwa bado mwanafunzi.

Je, hotuba za hawa marais wengine, mbona hakuna makusanyo hata kidogo. Kuna tatizo gani kwenye hotuba zao? Je, hazikuwa na faida pamoja na wote kukaa miaka kumi ikulu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom