Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Tafakari: Kuna watu kwa bahati mbaya sana wanachanganya matatizo yetu tuliyonayo na mfumo wetu wa jeshi la polisi na hata uongozi na utendaji kazi wake na matatizo na kila Mtanzania ambaye ni polisi. Kwamba, kwa vile tuna matatizo tunayoyalalamikia mara nyingi basi tuna matatizo na polisi wote Tanzania.
Fikra za namna hii ni fikra ambazo hazijafikiriwa vizuri. Tuna matatizo katika elimu na tuna matatizo na mfumo katika elimu kwani matokeo yake tunayaona, na tunalalamika kila kukicha na kutoa mawazo ili kuuboresha. Haina maana tuna matatizo na walimu wote Tanzania. Kwa vile mwalimu wa shule fulani kamcharaza mtoto hadi akazimia haina maana basi walimu wote wakipatwa na ajali tushangilie!
Tuna matatizo katika sekta ya afya na sehemu nyingine hadi watu wamepoteza vifo kwenye hospitali na kliniki zetu wakati mwingine sababu ya uzembe, ukosefu wa weledi na hata wakati mwingine ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya ufisadi. Watu wanalalamikia wauguzi na hata madaktari. Haina maana kesho akitokea mwehu mmoja akaanza kuua manesi Muhimbili au madaktari pale Bugando watu ambao wamewahi kupoteza au kupata huduma mbaya hospitali waanze kufurahia ati kwa sababu "kwani na sisi sio binadamu mbona manesi wanatutendea vibaya sana".
Naweza na kutoa mifano mingine mingi. Kufurahia au kushangilia au hata kuona ati polisi yamewakuta yanayopaswa kuwakuta ati kwa sababu polisi wanatutendea vibaya (baadhi yao) na kuwa tumepata huduma fulani mbaya ni kukosa ukomavu wa kihisia na kifikra.
Mimi nimeandika sana juu ya matatizo ya polisi na wakati mwingine kwa ukali sana. Nimeandika nilipoona wanaingiza siasa sana, hawatendei haki watu, au wanaminya demokrasia bila sababu ya msingi. Nimeandika kutetea vyama vya upinzani dhidi ya polisi na wakati mwingine hata kutoa maoni ya kuliboresha jeshi hilo. Kwa wasiojua wazo la kuanzishwa Kanda za Polisi (japo halijakamilishwa lote) tulianza nalo kwenye mtandao huu wakati wa bcstimes.
Ninaandika haya yote kama nilivyodokeza kwenye mada ile nyingine nikiwa ni zao la polisi Watanzania na nikiwa na familia iliyojaa polisi pande zote mbili. Ninapokosoa au kulalamika juu ya tukio au matukio fulani haina maana polisi akiuawa basi nifurahie au nichekelee au hata nione kuwa inawapasa. Nitakuwa nimekosa hekima, ukomavu na hata weledi wa kuwa mtu mwenye kufikiri vizuri.Ninapokosoa jeshi la polisi na kulalamikia ni kwa sababu najua ni kwa namna gani linapaswa kuwa bora zaidi kwa ajili yake yenyewe, kwa ajili ya taifa na kwa ajili ya kila mtu. Lakini pia ni kwa sababu polisi kama vyombo vingine vya dola lina jaribu kubwa sana la kutokujali.
Nimejifunza sana hapa US ambako nimeona jinsi jamii ya weusi ilivyo na matatizo ya kudumu na vikosi mbalimbali vya polisi na haipiti mwezi au hata wiki kabla hujasikia mahali fulani polisi wamemtendea kitu kibaya mtu mweusi asiye na hatia. Hata hivyo, pamoja na matatizo na hata malalamiko hutaona wala hutashuhudia weusi hawa wakishangilia polisi wakiuawa! Hawashangilii kwa sababu wanajua kuwa matatizo ya polisi yanapaswa kulalamikiwa na kushughulikiwa lakini wakati huo huo kuhakikisha kuwa polisi wao wanakuwa salama kwani usalama wa polisi ni usalama wa raia.
Kama polisi watatembea na kuhofia kuwa kila raia anayekuja mbele yao ana lengo baya nao, au kila anayewasimamisha anaweza kuwa na bunduki basi tunaweza kuwa na polisi ambao watakuwa wamejaa hofu sana na itakuwa ni hatari kwa raia hasa. Hili ni mojawapo ya mambo ambayo yanatokea Marekani sana ambapo Polisi wanakuwa katika hali ya shuku sana hasa kwa vile nchi hii raia wanaruhusa kubwa sana ya kuwa na silaha za moto na baadhi yao hawajachelewa kuzitumia dhidi ya raia kama tulivyoshuhudia mwaka jana ambapo polisi watano waliuawa kule Jiji la Dallas tena wakilinda maandamano ya watu waliokuwa wanalalamikia jeshi la polisi!
Tuna matatizo na jeshi la polisi, tuna mambo hatuyapendi na kuna mambo ambayo tungependa yawe yameshughulikiwa miaka ishirini iliyopita. Lakini hili halina maana kuwa tunataka polisi wetu wauawe kwa kisingizio chochote kile na kamwe hatuna furaha katika mauaji yao.
Hekima na ukomavu katika maisha unatukataza kuwa hivyo. [HASHTAG]#FarewellHeroes[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KwaheriMashujaa[/HASHTAG]