Tuna Tatizo na Mfumo, Muundo na Utendaji wa Polisi; Hatuna Tatizo na Kila Polisi Tanzania!

Back rush uliyoipata kuwatetea mashujaa naona imemfanya Mwanakijiji afungue uzi huu kusawazisha mambo.

Hiyo reaction waliyoionyesha ni ujumbe tosha kwa Waziri wa Mambo ya ndani, Police na Mkuu wa Nchi jinsi Jeshi let us la police lilivyo na mtizamo hasi kwa Raia wake.
Ni watu wa visasi sana. Hawajui bado wanawatia raia hasira. Kama hao waliowadhania ni majambazi wakawaua, itakuwaje kama hawakuwa majambazi? Hawaoni uhasama utazidi kuongezeka?
 
Hata kama wanakosea lakin haiwezi kuwa ndo sawa wao kuuawa,anyway pole nyingi kwa familia zilizopatwa na msiba huu,, lakin
Ninachokiona sasa hivi ni watuKuuawa ovyoovyo,
Kama mkuu anasema sasa mtaliona jeshi la polisi katika sura yake halisi ana maana gani?
Anataks kutuaminisha kuwa hawakuwa wakifanya kazi yao? Na je kutokana na hilo haoni kuwa hafai kuwa katika nafasi hiyo?
 
Tatzo ni uelewa.. Watu wengi sio waelewana ni vibendera bila kuelewa..
Kuielewesha jamii isiyo na uelewa ni vigumu sana..

Watu wengne wanatukana na kukejeli wakat ukiwauliza hao unaowatukana walikufanyia nn? Atakujibu kwasababu ametekwa Roma mkatoliki..

Kwahyo watu kama hao ni kuwaacha wakejeli ,watukane, washangilie mpaka nafsi zao ziwe na furaha. Lakn kwakuwa mwalimu yupo ambaye ni wakat atakuja kutufunza..

Wao wanafikiri zile siraha zinaenda kuchezewa bongo movie

Unafki Wa watanzania! Hawa hawa wanaotukana wakiibiwa au wakitapeliwa, wakipata matatzo yoyote utawakuta wamejazana vituo vya polisi..
64de564e6a336bad489de7d0a91b030b.jpg
wawe walinzi wa wote kwanza siyo Kwa ajili yenu tu na mali zenu za wizi. Nyinyi Ndio mnafanya tuwachukie. Huko mkuranga ukisikia wananchi walivyokuwa wananyanyaswa na kutolewa lugha za maudhi Ndio maana nao wanapotezea.

R.I.P polisi
 
Tafakari: Kuna watu kwa bahati mbaya sana wanachanganya matatizo yetu tuliyonayo na mfumo wetu wa jeshi la polisi na hata uongozi na utendaji kazi wake na matatizo na kila Mtanzania ambaye ni polisi. Kwamba, kwa vile tuna matatizo tunayoyalalamikia mara nyingi basi tuna matatizo na polisi wote Tanzania.

Fikra za namna hii ni fikra ambazo hazijafikiriwa vizuri. Tuna matatizo katika elimu na tuna matatizo na mfumo katika elimu kwani matokeo yake tunayaona, na tunalalamika kila kukicha na kutoa mawazo ili kuuboresha. Haina maana tuna matatizo na walimu wote Tanzania. Kwa vile mwalimu wa shule fulani kamcharaza mtoto hadi akazimia haina maana basi walimu wote wakipatwa na ajali tushangilie!

Tuna matatizo katika sekta ya afya na sehemu nyingine hadi watu wamepoteza vifo kwenye hospitali na kliniki zetu wakati mwingine sababu ya uzembe, ukosefu wa weledi na hata wakati mwingine ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya ufisadi. Watu wanalalamikia wauguzi na hata madaktari. Haina maana kesho akitokea mwehu mmoja akaanza kuua manesi Muhimbili au madaktari pale Bugando watu ambao wamewahi kupoteza au kupata huduma mbaya hospitali waanze kufurahia ati kwa sababu "kwani na sisi sio binadamu mbona manesi wanatutendea vibaya sana".

Naweza na kutoa mifano mingine mingi. Kufurahia au kushangilia au hata kuona ati polisi yamewakuta yanayopaswa kuwakuta ati kwa sababu polisi wanatutendea vibaya (baadhi yao) na kuwa tumepata huduma fulani mbaya ni kukosa ukomavu wa kihisia na kifikra.

Mimi nimeandika sana juu ya matatizo ya polisi na wakati mwingine kwa ukali sana. Nimeandika nilipoona wanaingiza siasa sana, hawatendei haki watu, au wanaminya demokrasia bila sababu ya msingi. Nimeandika kutetea vyama vya upinzani dhidi ya polisi na wakati mwingine hata kutoa maoni ya kuliboresha jeshi hilo. Kwa wasiojua wazo la kuanzishwa Kanda za Polisi (japo halijakamilishwa lote) tulianza nalo kwenye mtandao huu wakati wa bcstimes.

Ninaandika haya yote kama nilivyodokeza kwenye mada ile nyingine nikiwa ni zao la polisi Watanzania na nikiwa na familia iliyojaa polisi pande zote mbili. Ninapokosoa au kulalamika juu ya tukio au matukio fulani haina maana polisi akiuawa basi nifurahie au nichekelee au hata nione kuwa inawapasa. Nitakuwa nimekosa hekima, ukomavu na hata weledi wa kuwa mtu mwenye kufikiri vizuri.Ninapokosoa jeshi la polisi na kulalamikia ni kwa sababu najua ni kwa namna gani linapaswa kuwa bora zaidi kwa ajili yake yenyewe, kwa ajili ya taifa na kwa ajili ya kila mtu. Lakini pia ni kwa sababu polisi kama vyombo vingine vya dola lina jaribu kubwa sana la kutokujali.

Nimejifunza sana hapa US ambako nimeona jinsi jamii ya weusi ilivyo na matatizo ya kudumu na vikosi mbalimbali vya polisi na haipiti mwezi au hata wiki kabla hujasikia mahali fulani polisi wamemtendea kitu kibaya mtu mweusi asiye na hatia. Hata hivyo, pamoja na matatizo na hata malalamiko hutaona wala hutashuhudia weusi hawa wakishangilia polisi wakiuawa! Hawashangilii kwa sababu wanajua kuwa matatizo ya polisi yanapaswa kulalamikiwa na kushughulikiwa lakini wakati huo huo kuhakikisha kuwa polisi wao wanakuwa salama kwani usalama wa polisi ni usalama wa raia.

Kama polisi watatembea na kuhofia kuwa kila raia anayekuja mbele yao ana lengo baya nao, au kila anayewasimamisha anaweza kuwa na bunduki basi tunaweza kuwa na polisi ambao watakuwa wamejaa hofu sana na itakuwa ni hatari kwa raia hasa. Hili ni mojawapo ya mambo ambayo yanatokea Marekani sana ambapo Polisi wanakuwa katika hali ya shuku sana hasa kwa vile nchi hii raia wanaruhusa kubwa sana ya kuwa na silaha za moto na baadhi yao hawajachelewa kuzitumia dhidi ya raia kama tulivyoshuhudia mwaka jana ambapo polisi watano waliuawa kule Jiji la Dallas tena wakilinda maandamano ya watu waliokuwa wanalalamikia jeshi la polisi!

Tuna matatizo na jeshi la polisi, tuna mambo hatuyapendi na kuna mambo ambayo tungependa yawe yameshughulikiwa miaka ishirini iliyopita. Lakini hili halina maana kuwa tunataka polisi wetu wauawe kwa kisingizio chochote kile na kamwe hatuna furaha katika mauaji yao.

Hekima na ukomavu katika maisha unatukataza kuwa hivyo. [HASHTAG]#FarewellHeroes[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KwaheriMashujaa[/HASHTAG]
Katiba mpya ndiyo muarobaini japo watawala hawataki 'There taking advantage of our poorness'
 
Asante Mzee Mwanakijiji, tuna matatizo na jeshi la polisi, tuna mambo hatuyapendi na kuna mambo ambayo tungependa yawe yameshughulikiwa miaka ishirini iliyopita kama uliyvosema. Binafsi nafikiri muda wa mafunzo ya awali ya kipolisi ni mdogo mno kumwezesha mhitimu kuwa na weledi kitaaluma na kisakolojia. Anakuwa hajaziweka vizuri sheria kichwani na kuondoa dhana ya kwamba upolisi ni kuogofya raia. Polisi wengi wakiwa na bunduki wanajiona kuwa wao ni zaidi ya raia wa kawaida. Kuelewa dhana hii labda uwe umeisha kamatwa na polisi wa kawaida au hata wale usalama barabarani.

Angalia jinsi walivyokwenda kupambana na majambazi yaliyoua wenzao nane. Inasemekana polisi waliwachukua 'watuhumiwa' wa ujambazi ili wapelekwe maeneo wajifichao wenzao, matokeo yake ni kwamba hao waongozaji ('watuhumiwa' wa ujambazi) waliuawa sambamba na majambazi wanne na polisi mmoja akajeruhiwa mkono! Hii haijakaa sawa kitaalamu au kisheria.

Ilizidi kunishangaza baada ya msemaji wa kikosi cha polisi kutoa taarifa ya 'majigambo' kwamba jeshi lake limeisha ua majambazi wanne na bado namba itazidi kuongezeka hadi izidi ile ya polisi waliouawa. Kwani kuna vita inapigannwa?

Kwa nini mkoa wa Pwani unakuwa na matukio mengi ya Polisi kuuawa? Ni kwa nini mto Ruvu unakuwa ndio utumiwao kuzamisha watu waliouawa?

Tuwe wakweli wa nafsi zetu, msingi imara wa amani uliowekwa na waasisi wa taifa hili umepata ufa mkubwa, let us go back to the drawing board to redesign our peace foundation.

Tatzo ni uelewa.. Watu wengi sio waelewana ni vibendera bila kuelewa..
Kuielewesha jamii isiyo na uelewa ni vigumu sana..

Watu wengne wanatukana na kukejeli wakat ukiwauliza hao unaowatukana walikufanyia nn? Atakujibu kwasababu ametekwa Roma mkatoliki..

Kwahyo watu kama hao ni kuwaacha wakejeli ,watukane, washangilie mpaka nafsi zao ziwe na furaha. Lakn kwakuwa mwalimu yupo ambaye ni wakat atakuja kutufunza..

Wao wanafikiri zile siraha zinaenda kuchezewa bongo movie

Unafki Wa watanzania! Hawa hawa wanaotukana wakiibiwa au wakitapeliwa, wakipata matatzo yoyote utawakuta wamejazana vituo vya polisi..
64de564e6a336bad489de7d0a91b030b.jpg
Kulinda watu na mali zao ni jukumu na wajibu wa polisi na sio fever, hii ndio kazi yao na ndio walioichagua watake wasitake.
 
Na hapo ndipo low intelligence yenu ilipo, unasema Upolisi ni kama udaktari? Unajua mafunzo ya Askari wewe? Askari hatakiwi kuhoji Amri ktk kwa mkubwa wake bali ni kutekeleza tu, kama una tatizo na Askari wetu elekezea kwa watoa Amri na siyo mtii Amri, na ndiyo maana hata kwenye Mahakama za Kimataifa za kihalifu hakuna Askari anayeshitakiwa bali mtoa Amri ndiyo hushitakiwa na siyo Askari, kwani yeye hutii Amri tu na siyo vinginevyo!
Aisee, umeandika kwa hasira,
 
Nadhani tuna tatizo kubwa sana linalohitaji suluhisho la haraka . Soma tu comments za watu utajionea mwenyewe.
 
Unachosema ni ukweli kabisa,je Polisi wenyewe hasa wadogo wameshajua wafanyacho ni kosa??

Je,pale Polisi wa Cheo cha juu kabisa anapokubali kutumia na wanasiasa kwa sababu ya vyeo vyao inawapa picha gani Polisi wa ngazi ya chini na RAIA??

Unadhani Polisi wa ngazi za juu walifanya kazi zao Kwa weledi Polisi wa chini watafanyaje??

Issue si System, issue hapa ni wakubwa wa polisi kuamua kwa dhati kutotumika vibaya na Watawala sababu ya nafasi zao.

Wakikubali hata kufukuzwa kazi kutetea haki za RAIA na taaluma yao hawa ndiyo wakuwapigia makofi kwa maana hakika wanatekeleza majukumu yao ya kulinda RAIA na Mali zao.

Waache kubagua RAIA Watanzania kwa itikadi au ukabila.Ni muda muafaka wa kujitambua wao sasa.

Inawezekana kabisa jirani walikuwa wanajua lakini tumeshahimizwa RAIA tuwaogope polisi utaenda kuwaambia kuna msala mahali wajiangalie??Kwa jinsi polisi walivyo,wanaweza kumfuata mtuhumiwa wakakutaja halafu inakuwaje??

Wajifunze kutokana na makosa.Tunachukia tabia na hulka zao na si u binadamu wao.
Je ni polisi gani atakaye wakemea wanasiasa wanaolitumia jeshi la polisi kwa maslahi yao binafsi?

Watanzania wengi wa leo wamekuwa wabinafsi.
 
Hapa mzee mzima uko out of touch. Wananchi walio wengi wanaoishi hapa Tanzania hawawezi kuwa na mtizamo kama wako wala kuukubali. Kiukweli na kiuhalisia, ni vigumu kuishi nchini na kuwa na mapenzi ya dhati kwa vyombo vya usalama.
 
Unachosema ni ukweli kabisa,je Polisi wenyewe hasa wadogo wameshajua wafanyacho ni kosa??

Je,pale Polisi wa Cheo cha juu kabisa anapokubali kutumia na wanasiasa kwa sababu ya vyeo vyao inawapa picha gani Polisi wa ngazi ya chini na RAIA??

Unadhani Polisi wa ngazi za juu walifanya kazi zao Kwa weledi Polisi wa chini watafanyaje??

Issue si System, issue hapa ni wakubwa wa polisi kuamua kwa dhati kutotumika vibaya na Watawala sababu ya nafasi zao.

Wakikubali hata kufukuzwa kazi kutetea haki za RAIA na taaluma yao hawa ndiyo wakuwapigia makofi kwa maana hakika wanatekeleza majukumu yao ya kulinda RAIA na Mali zao.

Waache kubagua RAIA Watanzania kwa itikadi au ukabila.Ni muda muafaka wa kujitambua wao sasa.

Inawezekana kabisa jirani walikuwa wanajua lakini tumeshahimizwa RAIA tuwaogope polisi utaenda kuwaambia kuna msala mahali wajiangalie??Kwa jinsi polisi walivyo,wanaweza kumfuata mtuhumiwa wakakutaja halafu inakuwaje??

Wajifunze kutokana na makosa.Tunachukia tabia na hulka zao na si u binadamu wao.
Polisi wasiongozwe na wanasiasa Kamanda wa Polisi ndio awe Chairman wa kamati ya usalama ya mkoa, wanasiasa wawaache polisi wafanye kazi zao kama walivyosomea. Tukiwa na jeshi la Polisi ambalo linatii amri zao wenyewe tutakua salama na kelele za wanasiasa. Tuwaheshimu polisi wafanye kazi zao kwa weledi kwani na wao wanakereka wakiingiliwa na wanasiasa ambao hupita lakini wao wanabakia polisi maana ni kazi yao
 
Tatizo unatumia muda na nguvu nyingi kujaribu kuwaelezea watu ambao wana low intelligence, unapoteza muda hawa watu ni stupid, mtu ambaye anamchukia Askari ambaye kazi yake ni kutii tu Amri na siyo kuhoji, mtu huyu ni mjinga hivyo utakesha hapa lkn chadema hautaelewana nao kwa maana wanashindwa kutofautisha kati ya hayo mawili na sababu ni kwamba wana low intelligence na hamna kitu utafanya!
Hopeless kabisa wewee..
Yani wewee utatii tu kila jambo uliloamriwa kufanya na mkubwa wako hata kama ni la hatari kwa maisha yako wewe Polisi au la unaemfanyia??
Aisee kwenye kifuko cha kukaa ubongo naona cha kwako kumejaa makamasi...
Jinga.
 
Hakuna kazi ya kutii bila kufuata Sheria na Katiba za nchi.

Hakuna mahali panaposema ukiambiwa na Mkuu wa mkoa au wilaya kamteke na kumyesa Barbarosa basi unaenda kufanya tu kwa sababu umepewa amri na mkuu.

Ndiyo upumbavu na upuuzi tunaousema.Wafuate sheria na taaluma zao.Waache kuwa tawi la Chama Cha Mauaji.

Hili ni moja la kosa kubwa sana ndugu zetu polisi wanalifanya kila siku, wao wanaona wapo juu ya sheria na utetezi wao ni sisi tunatumwa na wakubwa. Inabidi polisi wafuate sheria na taratibu za kikatiba zilizowekwa. Katiba hakuna kitu kama hiko cha "NIMETUMWA NA WAKUBWA", ndiyo maana watu wengi leo wanalalamika kwa nini polisi Form Four failure ndiyo wanakuwa wananafasi ya kuwa mapolisi kuliko hata wasomi. Hizi failure zao wanazowapa nafasi ndiyo mwisho wanashindwa hata kuReason wanapopewa maagizo ambayo hayapo sawa.

Upumbavu wanoufanya kwa jamii wasifikire jamii hii haiumii,wote ni binadamu hakuna nguruwe.Tunaona mnavyokuja juu kama moto wa kifuu,hatulaani kufa au kuuawa kwa polisi tunalaani kuuawa kwa Binadamu,maana u binadamu wake ndiyo uliomfanya awe Polisi.

Leo kila mtu anaona jinsi polisi wanavyokatamiza haki za watu na kuua watu hovyo hovyo lakini bado unataka watu wawe na feelings za kuwasifu bila kujali madhara wanayopata kutoka na vitendo vyao viovu.

Upolisi ni taaluma kama taaluma nyingine ni kama Udaktari na uanasheria.Taaluma hizi tatu zinawafunga kwenye eneo moja kutetea na kulinda uhai wa binadamu bila kujali Itikadi au Ukanda wao Bali utu wao.

Tusipumbazwe na upuuzi wa wachache kufanya maovu,ni wakati wa polisi kujitafakari kama kweli wanahitaji ka kuogopewa au kuwa rafiki wa RAIA??

Enzi za JKN polisi alikuwa Rafiki na Leo.polisi ni nani??Kama Rais anawaamvia Polisi anataka RAIA iawaogope polisi,tujiulize wanapata wapi information za wahalifu??

Polisi wameamua kuweka margin kati ya raia na wao, na hata viongozi wakuu hawafanyi njia zozote zile kuondoa huu mstari mwekunde waliouweka, ndiyo kwanza wanasema "I WISH I COULD BE IGP", ushirikiano wa polisi na wananchi ni kitu cha lazima na cha msingi, kama leo polisi na raia hawapendani, sifikir kama kazi ya polisi itafanyika kiusalama na kiuhakika, kwasababu wahalifu wote tunaishi nao mitaani lakini siku za nyuma isharipotiwa watu wanatoa taarifa polisi lakini mwisho polisi wanawachoma raia kwa wahalifu na mwisho raia mwema wanapata matatizo.

Simchukii polisi maana ni binadamu anastahili kuishi na chukia hulka na matendo ya polisi ifike mahali wajirekebishe.

Polisi ni binadamu wanastahili kuishi na kuheshimika.Waanze kuona RAIA ni binadamu w anastahili kuishi na kuheshimika.Na bila RAIA polisi hawezi kufanya kazi yake kwa wepesi.

Mwisho toa pole kwa familia kwa jeshi la polisi na familia zao kwa matatizo waliyopata, lakini polisi lazima ifanye reform ya nguvu sana ya kiutendaji na bila kusahau kufuata sheria na taratibu na kujitoa kuwa sehemu ya chama tawala.

Asante
 
Hili ni moja la kosa kubwa sana ndugu zetu polisi wanalifanya kila siku, wao wanaona wapo juu ya sheria na utetezi wao ni sisi tunatumwa na wakubwa. Inabidi polisi wafuate sheria na taratibu za kikatiba zilizowekwa. Katiba hakuna kitu kama hiko cha "NIMETUMWA NA WAKUBWA", ndiyo maana watu wengi leo wanalalamika kwa nini polisi Form Four failure ndiyo wanakuwa wananafasi ya kuwa mapolisi kuliko hata wasomi. Hizi failure zao wanazowapa nafasi ndiyo mwisho wanashindwa hata kuReason wanapopewa maagizo ambayo hayapo sawa.

Leo kila mtu anaona jinsi polisi wanavyokatamiza haki za watu na kuua watu hovyo hovyo lakini bado unataka watu wawe na feelings za kuwasifu bila kujali madhara wanayopata kutoka na vitendo vyao viovu.

Polisi wameamua kuweka margin kati ya raia na wao, na hata viongozi wakuu hawafanyi njia zozote zile kuondoa huu mstari mwekunde waliouweka, ndiyo kwanza wanasema "I WISH I COULD BE IGP", ushirikiano wa polisi na wananchi ni kitu cha lazima na cha msingi, kama leo polisi na raia hawapendani, sifikir kama kazi ya polisi itafanyika kiusalama na kiuhakika, kwasababu wahalifu wote tunaishi nao mitaani lakini siku za nyuma isharipotiwa watu wanatoa taarifa polisi lakini mwisho polisi wanawachoma raia kwa wahalifu na mwisho raia mwema wanapata matatizo.
Mwisho toa pole kwa familia kwa jeshi la polisi na familia zao kwa matatizo waliyopata, lakini polisi lazima ifanye reform ya nguvu sana ya kiutendaji na bila kusahau kufuata sheria na taratibu na kujitoa kuwa sehemu ya chama tawala.
 
Ni watu wa visasi sana. Hawajui bado wanawatia raia hasira. Kama hao waliowadhania ni majambazi wakawaua, itakuwaje kama hawakuwa majambazi? Hawaoni uhasama utazidi kuongezeka?
Jeshi letu la police linafanya kazi kisiasa. Siyo rahisi likapendwa na raia. Mwanakijiji analijua hilo ndiyo maana analeta propaganda kulitetea. As individuals tutajua kuwa ni watu wazuri na wana ndugu, jamaa na marafiki wengi tu ambao watawalilia. But as a nation kwa style yao lazima watu watagawanyika.

Kama police wetu wanataka wapendwe kama hao Mwanakijiji anaowatolea mfano basi waanze pia kumfanya kazi kama hao.
 
Back
Top Bottom