Tuna Tatizo na Mfumo, Muundo na Utendaji wa Polisi; Hatuna Tatizo na Kila Polisi Tanzania!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,848
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,848 2,000
Tafakari: Kuna watu kwa bahati mbaya sana wanachanganya matatizo yetu tuliyonayo na mfumo wetu wa jeshi la polisi na hata uongozi na utendaji kazi wake na matatizo na kila Mtanzania ambaye ni polisi. Kwamba, kwa vile tuna matatizo tunayoyalalamikia mara nyingi basi tuna matatizo na polisi wote Tanzania.

Fikra za namna hii ni fikra ambazo hazijafikiriwa vizuri. Tuna matatizo katika elimu na tuna matatizo na mfumo katika elimu kwani matokeo yake tunayaona, na tunalalamika kila kukicha na kutoa mawazo ili kuuboresha. Haina maana tuna matatizo na walimu wote Tanzania. Kwa vile mwalimu wa shule fulani kamcharaza mtoto hadi akazimia haina maana basi walimu wote wakipatwa na ajali tushangilie!

Tuna matatizo katika sekta ya afya na sehemu nyingine hadi watu wamepoteza vifo kwenye hospitali na kliniki zetu wakati mwingine sababu ya uzembe, ukosefu wa weledi na hata wakati mwingine ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya ufisadi. Watu wanalalamikia wauguzi na hata madaktari. Haina maana kesho akitokea mwehu mmoja akaanza kuua manesi Muhimbili au madaktari pale Bugando watu ambao wamewahi kupoteza au kupata huduma mbaya hospitali waanze kufurahia ati kwa sababu "kwani na sisi sio binadamu mbona manesi wanatutendea vibaya sana".

Naweza na kutoa mifano mingine mingi. Kufurahia au kushangilia au hata kuona ati polisi yamewakuta yanayopaswa kuwakuta ati kwa sababu polisi wanatutendea vibaya (baadhi yao) na kuwa tumepata huduma fulani mbaya ni kukosa ukomavu wa kihisia na kifikra.

Mimi nimeandika sana juu ya matatizo ya polisi na wakati mwingine kwa ukali sana. Nimeandika nilipoona wanaingiza siasa sana, hawatendei haki watu, au wanaminya demokrasia bila sababu ya msingi. Nimeandika kutetea vyama vya upinzani dhidi ya polisi na wakati mwingine hata kutoa maoni ya kuliboresha jeshi hilo. Kwa wasiojua wazo la kuanzishwa Kanda za Polisi (japo halijakamilishwa lote) tulianza nalo kwenye mtandao huu wakati wa bcstimes.

Ninaandika haya yote kama nilivyodokeza kwenye mada ile nyingine nikiwa ni zao la polisi Watanzania na nikiwa na familia iliyojaa polisi pande zote mbili. Ninapokosoa au kulalamika juu ya tukio au matukio fulani haina maana polisi akiuawa basi nifurahie au nichekelee au hata nione kuwa inawapasa. Nitakuwa nimekosa hekima, ukomavu na hata weledi wa kuwa mtu mwenye kufikiri vizuri.Ninapokosoa jeshi la polisi na kulalamikia ni kwa sababu najua ni kwa namna gani linapaswa kuwa bora zaidi kwa ajili yake yenyewe, kwa ajili ya taifa na kwa ajili ya kila mtu. Lakini pia ni kwa sababu polisi kama vyombo vingine vya dola lina jaribu kubwa sana la kutokujali.

Nimejifunza sana hapa US ambako nimeona jinsi jamii ya weusi ilivyo na matatizo ya kudumu na vikosi mbalimbali vya polisi na haipiti mwezi au hata wiki kabla hujasikia mahali fulani polisi wamemtendea kitu kibaya mtu mweusi asiye na hatia. Hata hivyo, pamoja na matatizo na hata malalamiko hutaona wala hutashuhudia weusi hawa wakishangilia polisi wakiuawa! Hawashangilii kwa sababu wanajua kuwa matatizo ya polisi yanapaswa kulalamikiwa na kushughulikiwa lakini wakati huo huo kuhakikisha kuwa polisi wao wanakuwa salama kwani usalama wa polisi ni usalama wa raia.

Kama polisi watatembea na kuhofia kuwa kila raia anayekuja mbele yao ana lengo baya nao, au kila anayewasimamisha anaweza kuwa na bunduki basi tunaweza kuwa na polisi ambao watakuwa wamejaa hofu sana na itakuwa ni hatari kwa raia hasa. Hili ni mojawapo ya mambo ambayo yanatokea Marekani sana ambapo Polisi wanakuwa katika hali ya shuku sana hasa kwa vile nchi hii raia wanaruhusa kubwa sana ya kuwa na silaha za moto na baadhi yao hawajachelewa kuzitumia dhidi ya raia kama tulivyoshuhudia mwaka jana ambapo polisi watano waliuawa kule Jiji la Dallas tena wakilinda maandamano ya watu waliokuwa wanalalamikia jeshi la polisi!

Tuna matatizo na jeshi la polisi, tuna mambo hatuyapendi na kuna mambo ambayo tungependa yawe yameshughulikiwa miaka ishirini iliyopita. Lakini hili halina maana kuwa tunataka polisi wetu wauawe kwa kisingizio chochote kile na kamwe hatuna furaha katika mauaji yao.

Hekima na ukomavu katika maisha unatukataza kuwa hivyo. [HASHTAG]#FarewellHeroes[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KwaheriMashujaa[/HASHTAG]
 
Ndera

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Messages
657
Points
1,000

Ndera

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2013
657 1,000
Kero nyingi sana tunazipata toka kwa hao polisi, hawana utu,wanatumia nguvu pasipo hitaji nguvu, haki hakuna, wananchi tumepoteza ukaribu na hao polisi kutokana na mfumo wao kandamizi!!
 
Mgirik

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Messages
12,241
Points
2,000

Mgirik

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2013
12,241 2,000
Tatzo ni uelewa.. Watu wengi sio waelewana ni vibendera bila kuelewa..
Kuielewesha jamii isiyo na uelewa ni vigumu sana..

Watu wengne wanatukana na kukejeli wakat ukiwauliza hao unaowatukana walikufanyia nn? Atakujibu kwasababu ametekwa Roma mkatoliki..

Kwahyo watu kama hao ni kuwaacha wakejeli ,watukane, washangilie mpaka nafsi zao ziwe na furaha. Lakn kwakuwa mwalimu yupo ambaye ni wakat atakuja kutufunza..

Wao wanafikiri zile siraha zinaenda kuchezewa bongo movie

Unafki Wa watanzania! Hawa hawa wanaotukana wakiibiwa au wakitapeliwa, wakipata matatzo yoyote utawakuta wamejazana vituo vya polisi..
 
Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
26,390
Points
2,000

Tetty

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
26,390 2,000

Unachosema ni ukweli kabisa,je Polisi wenyewe hasa wadogo wameshajua wafanyacho ni kosa??

Je,pale Polisi wa Cheo cha juu kabisa anapokubali kutumia na wanasiasa kwa sababu ya vyeo vyao inawapa picha gani Polisi wa ngazi ya chini na RAIA??

Unadhani Polisi wa ngazi za juu walifanya kazi zao Kwa weledi Polisi wa chini watafanyaje??

Issue si System, issue hapa ni wakubwa wa polisi kuamua kwa dhati kutotumika vibaya na Watawala sababu ya nafasi zao.

Wakikubali hata kufukuzwa kazi kutetea haki za RAIA na taaluma yao hawa ndiyo wakuwapigia makofi kwa maana hakika wanatekeleza majukumu yao ya kulinda RAIA na Mali zao.

Waache kubagua RAIA Watanzania kwa itikadi au ukabila.Ni muda muafaka wa kujitambua wao sasa.

Inawezekana kabisa jirani walikuwa wanajua lakini tumeshahimizwa RAIA tuwaogope polisi utaenda kuwaambia kuna msala mahali wajiangalie??Kwa jinsi polisi walivyo,wanaweza kumfuata mtuhumiwa wakakutaja halafu inakuwaje??

Wajifunze kutokana na makosa.Tunachukia tabia na hulka zao na si u binadamu wao.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,613
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,613 2,000
Tafakari: Kuna watu kwa bahati mbaya sana wanachanganya matatizo yetu tuliyonayo na mfumo wetu wa jeshi la polisi na hata uongozi na utendaji kazi wake na matatizo na kila Mtanzania ambaye ni polisi. Kwamba, kwa vile tuna matatizo tunayoyalalamikia mara nyingi basi tuna matatizo na polisi wote Tanzania.

Fikra za namna hii ni fikra ambazo hazijafikiriwa vizuri. Tuna matatizo katika elimu na tuna matatizo na mfumo katika elimu kwani matokeo yake tunayaona, na tunalalamika kila kukicha na kutoa mawazo ili kuuboresha. Haina maana tuna matatizo na walimu wote Tanzania. Kwa vile mwalimu wa shule fulani kamcharaza mtoto hadi akazimia haina maana basi walimu wote wakipatwa na ajali tushangilie!

Tuna matatizo katika sekta ya afya na sehemu nyingine hadi watu wamepoteza vifo kwenye hospitali na kliniki zetu wakati mwingine sababu ya uzembe, ukosefu wa weledi na hata wakati mwingine ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya ufisadi. Watu wanalalamikia wauguzi na hata madaktari. Haina maana kesho akitokea mwehu mmoja akaanza kuua manesi Muhimbili au madaktari pale Bugando watu ambao wamewahi kupoteza au kupata huduma mbaya hospitali waanze kufurahia ati kwa sababu "kwani na sisi sio binadamu mbona manesi wanatutendea vibaya sana".

Naweza na kutoa mifano mingine mingi. Kufurahia au kushangilia au hata kuona ati polisi yamewakuta yanayopaswa kuwakuta ati kwa sababu polisi wanatutendea vibaya (baadhi yao) na kuwa tumepata huduma fulani mbaya ni kukosa ukomavu wa kihisia na kifikra.

Mimi nimeandika sana juu ya matatizo ya polisi na wakati mwingine kwa ukali sana. Nimeandika nilipoona wanaingiza siasa sana, hawatendei haki watu, au wanaminya demokrasia bila sababu ya msingi. Nimeandika kutetea vyama vya upinzani dhidi ya polisi na wakati mwingine hata kutoa maoni ya kuliboresha jeshi hilo. Kwa wasiojua wazo la kuanzishwa Kanda za Polisi (japo halijakamilishwa lote) tulianza nalo kwenye mtandao huu wakati wa bcstimes.

Ninaandika haya yote kama nilivyodokeza kwenye mada ile nyingine nikiwa ni zao la polisi Watanzania na nikiwa na familia iliyojaa polisi pande zote mbili. Ninapokosoa au kulalamika juu ya tukio au matukio fulani haina maana polisi akiuawa basi nifurahie au nichekelee au hata nione kuwa inawapasa. Nitakuwa nimekosa hekima, ukomavu na hata weledi wa kuwa mtu mwenye kufikiri vizuri.Ninapokosoa jeshi la polisi na kulalamikia ni kwa sababu najua ni kwa namna gani linapaswa kuwa bora zaidi kwa ajili yake yenyewe, kwa ajili ya taifa na kwa ajili ya kila mtu. Lakini pia ni kwa sababu polisi kama vyombo vingine vya dola lina jaribu kubwa sana la kutokujali.

Nimejifunza sana hapa US ambako nimeona jinsi jamii ya weusi ilivyo na matatizo ya kudumu na vikosi mbalimbali vya polisi na haipiti mwezi au hata wiki kabla hujasikia mahali fulani polisi wamemtendea kitu kibaya mtu mweusi asiye na hatia. Hata hivyo, pamoja na matatizo na hata malalamiko hutaona wala hutashuhudia weusi hawa wakishangilia polisi wakiuawa! Hawashangilii kwa sababu wanajua kuwa matatizo ya polisi yanapaswa kulalamikiwa na kushughulikiwa lakini wakati huo huo kuhakikisha kuwa polisi wao wanakuwa salama kwani usalama wa polisi ni usalama wa raia.

Kama polisi watatembea na kuhofia kuwa kila raia anayekuja mbele yao ana lengo baya nao, au kila anayewasimamisha anaweza kuwa na bunduki basi tunaweza kuwa na polisi ambao watakuwa wamejaa hofu sana na itakuwa ni hatari kwa raia hasa. Hili ni mojawapo ya mambo ambayo yanatokea Marekani sana ambapo Polisi wanakuwa katika hali ya shuku sana hasa kwa vile nchi hii raia wanaruhusa kubwa sana ya kuwa na silaha za moto na baadhi yao hawajachelewa kuzitumia dhidi ya raia kama tulivyoshuhudia mwaka jana ambapo polisi watano waliuawa kule Jiji la Dallas tena wakilinda maandamano ya watu waliokuwa wanalalamikia jeshi la polisi!

Tuna matatizo na jeshi la polisi, tuna mambo hatuyapendi na kuna mambo ambayo tungependa yawe yameshughulikiwa miaka ishirini iliyopita. Lakini hili halina maana kuwa tunataka polisi wetu wauawe kwa kisingizio chochote kile na kamwe hatuna furaha katika mauaji yao.

Hekima na ukomavu katika maisha unatukataza kuwa hivyo. [HASHTAG]#FarewellHeroes[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KwaheriMashujaa[/HASHTAG]

Tatizo unatumia muda na nguvu nyingi kujaribu kuwaelezea watu ambao wana low intelligence, unapoteza muda hawa watu ni stupid, mtu ambaye anamchukia Askari ambaye kazi yake ni kutii tu Amri na siyo kuhoji, mtu huyu ni mjinga hivyo utakesha hapa lkn chadema hautaelewana nao kwa maana wanashindwa kutofautisha kati ya hayo mawili na sababu ni kwamba wana low intelligence na hamna kitu utafanya!
 
Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2007
Messages
11,467
Points
2,000

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2007
11,467 2,000
Back rush uliyoipata kuwatetea mashujaa naona imemfanya Mwanakijiji afungue uzi huu kusawazisha mambo.

Hiyo reaction waliyoionyesha ni ujumbe tosha kwa Waziri wa Mambo ya ndani, Police na Mkuu wa Nchi jinsi Jeshi let us la police lilivyo na mtizamo hasi kwa Raia wake.
 
Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
26,390
Points
2,000

Tetty

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
26,390 2,000
Tatzo ni uelewa.. Watu wengi sio waelewana ni vibendera bila kuelewa..
Kuielewesha jamii isiyo na uelewa ni vigumu sana..

Watu wengne wanatukana na kukejeli wakat ukiwauliza hao unaowatukana walikufanyia nn? Atakujibu kwasababu ametekwa Roma mkatoliki..

Kwahyo watu kama hao ni kuwaacha wakejeli ,watukane, washangilie mpaka nafsi zao ziwe na furaha. Lakn kwakuwa mwalimu yupo ambaye ni wakat atakuja kutufunza..

Wao wanafikiri zile siraha zinaenda kuchezewa bongo movie

Unafki Wa watanzania! Hawa hawa wanaotukana wakiibiwa au wakitapeliwa, wakipata matatzo yoyote utawakuta wamejazana vituo vya polisi..
Ni kweli kabisa huwezi kuelewa jambo mpaka limekupata,hakika umenena.

Hebu fikiria RAIA wangapi wamepoteza maisha baada ya kutoa information kwa Polisi kuhusu uhalifu??

Ni nani ndani ya Jeshi hilo wako busy kutoa taarifa za watoa taarifa??Ni kweli hawajulikani??

Basi ukijua Watanzania wangapi wamepoteza maisha au viungo vyao baada ya kutoa taarifa Polisi kuhusu majaribio ya uhalifu ndipo utaelewa kwa nini RAIA wanahasira na Polisi.

Ni wakati wa Polisi kujisahihisha kuanzia juu kabisa level ya IGP hadi level ya mfagia ofisi.In short wasiwe wabaguzi,waache siasa na waache kutoa siri za watoa siri za majaribio ya uhalifu na mwisho wakome kubambikizia RAIA kesi
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
8,632
Points
2,000

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
8,632 2,000
Mkuu Mzee Mwanakijiji

Usimlazimishe kila mtu aa feel unavyo feel wewe kutokana na hili tukio lililowapata Polisi juzi.

Kila mtu anapata hisia ya jambo kutokana na fikra zake kutokana na namna jambo husika lilivyomgusa.

Mfano mdogo tu, je unaweza kuishangaa familia ya Marehemu Daudi Mwangosi wakiwa hawana feeling kabisa na hili tukio au tukio lolote baya linalowakumba polisi hapa Nchini?? Je familia za wale wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge waliouwawa na kina Zombe wasipokuwa na feeling yoyote na tukio kama hili utawalaumu??

Vipi kwa watu wanaofanyiwa mambo mabaya na polisi, kusumbuliwa rushwa, kubambikiwa kesi, kunyanyaswa kwa namna mbalimbali, kutekwa, kuteswa nk nk unategemea watakuwa na same deep feelings/sympathy kama ulizonazo wewe..??

Hii ni kwasababu moja kubwa.

Polisi wetu wamekuwa wakitumiwa na wakikubali kutumika vibaya kwenye mission mbaya mbali mbali zinazofanywa na serikali dhidi ya raia wake na hasa wafuasi wa vyama vya upinzani na matokeo yake kuacha makovu hasi makubwa kwa wananchi wake.

Wala usifananishe Polisi na matukio kama ya Mwalimu kumchapa mwanafunzi/mtoto na kumjeruhi au wauguzi wa afya kuwanyanyasa wagonjwa.
Haya matukio ya hizi kada nyingine huwa matukio yake ni machache sana na hata matukio yoyote ya uvunjaji wa taratibu zao za kazi yakitokea huwa tunaona hatua huwa zinachukuliwa.

Tumeona mara kadhaa manesi wazembe au walimu wazembe wakiadhibiwa lakini sio polisi.

Polisi wanafanya makosa, watu wanalalamika lakini hatua hazichukliwi muda mwingine aliyefanya kosa anapandishwa cheo..refer Kamanda Kamuhanda alivyoshiriki kwenye mauaji ya Mwangosi na akapanda cheo.

Please waache watu wawe na uhuru wao wa kufeel haya matukio yanapotokea. Usilazimishe deep feelings zako ziwe za wote.
 
mburasi

Member
Joined
Dec 19, 2016
Messages
33
Points
125

mburasi

Member
Joined Dec 19, 2016
33 125
Mimi nadhani sio kwamba wanashangilia polisi kuuwawa kwa mfano maeneo hayohayo viongozi waserikali za vijiji wamekuwa wakiuwawa baada ya kupewa vitisho na wengine wamehama vijiji lkn serikali haikujali lkn lilivyotokea hili mpaka Raisi kaongea kwa hyo inanaokana raia sio kitu
 
Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
26,390
Points
2,000

Tetty

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
26,390 2,000
Tatizo unatumia muda na nguvu nyingi kujaribu kuwaelezea watu ambao wana low intelligence, unapoteza muda hawa watu ni stupid, mtu ambaye anamchukia Askari ambaye kazi yake ni kutii tu Amri na siyo kuhoji, mtu huyu ni mjinga hivyo utakesha hapa lkn chadema hautaelewana nao kwa maana wanashindwa kutofautisha kati ya hayo mawili na sababu ni kwamba wana low intelligence na hamna kitu utafanya!
Hakuna kazi ya kutii bila kufuata Sheria na Katiba za nchi.

Hakuna mahali panaposema ukiambiwa na Mkuu wa mkoa au wilaya kamteke na kumyesa Barbarosa basi unaenda kufanya tu kwa sababu umepewa amri na mkuu.

Ndiyo upumbavu na upuuzi tunaousema.Wafuate sheria na taaluma zao.Waache kuwa tawi la Chama Cha Mauaji.

Upumbavu wanoufanya kwa jamii wasifikire jamii hii haiumii,wote ni binadamu hakuna nguruwe.Tunaona mnavyokuja juu kama moto wa kifuu,hatulaani kufa au kuuawa kwa polisi tunalaani kuuawa kwa Binadamu,maana u binadamu wake ndiyo uliomfanya awe Polisi.

Upolisi ni taaluma kama taaluma nyingine ni kama Udaktari na uanasheria.Taaluma hizi tatu zinawafunga kwenye eneo moja kutetea na kulinda uhai wa binadamu bila kujali Itikadi au Ukanda wao Bali utu wao.

Tusipumbazwe na upuuzi wa wachache kufanya maovu,ni wakati wa polisi kujitafakari kama kweli wanahitaji ka kuogopewa au kuwa rafiki wa RAIA??

Enzi za JKN polisi alikuwa Rafiki na Leo.polisi ni nani??Kama Rais anawaamvia Polisi anataka RAIA iawaogope polisi,tujiulize wanapata wapi information za wahalifu??

Simchukii polisi maana ni binadamu anastahili kuishi na chukia hulka na matendo ya polisi ifike mahali wajirekebishe.

Polisi ni binadamu wanastahili kuishi na kuheshimika.Waanze kuona RAIA ni binadamu w anastahili kuishi na kuheshimika.Na bila RAIA polisi hawezi kufanya kazi yake kwa wepesi.
 
SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,748
Points
2,000

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,748 2,000
Pengine marekani sio mfano mzuri sana. Marekani imeshuhudia mauaji kadhaa ya polisi wake kama ulipizaji kisasi.

Wangalikuwa na usathimilivu kiasi hicho kusingekuwa na ulipizaji kisasi kutoka kwa raia wake. Hapa Tanzania, angalau watu wana retaliate miyoni tu kama tunavyoona katika hili la hawa polisi nane.

Kwa hivyo mtazamo wangu ni kuwa Tanzania tumestaarabika zaidi kuliko marekani katika kuheshimu polisi.
 
Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
26,390
Points
2,000

Tetty

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
26,390 2,000
Mkuu Mzee Mwanakijiji

Usimlazimishe kila mtu aa feel unavyo feel wewe kutokana na hili tukio lililowapata Polisi juzi.

Kila mtu anapata hisia ya jambo kutokana na fikra zake kutokana na namna jambo husika lilivyomgusa.

Mfano mdogo tu, je unaweza kuishangaa familia ya Marehemu Daudi Mwangosi wakiwa hawana feeling kabisa na hili tukio au tukio lolote baya linalowakumba polisi hapa Nchini?? Je familia za wale wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge waliouwawa na kina Zombe wasipokuwa na feeling yoyote na tukio kama hili utawalaumu??

Vipi kwa watu wanaofanyiwa mambo mabaya na polisi, kusumbuliwa rushwa, kubambikiwa kesi, kunyanyaswa kwa namna mbalimbali, kutekwa, kuteswa nk nk unategemea watakuwa na same deep feelings/sympathy kama ulizonazo wewe..??

Hii ni kwasababu moja kubwa.

Polisi wetu wamekuwa wakitumiwa na wakikubali kutumika vibaya kwenye mission mbaya mbali mbali zinazofanywa na serikali dhidi ya raia wake na matokeo yake kuacha makovu makubwa kwa wananchi wake.

Wala usifananishe Polisi na matukio kama ya Mwalimu kumchapa mwanafunzi/mtoto na kumjeruhi au wauguzi wa afya kuwanyanyasa wagonjwa.
Haya matukio ya hizi kada nyingine huwa matukio yake ni machache sana na hata matukio yoyote ya uvunjaji wa taratibu zao za kazi yakitokea huwa tunaona hatua huwa zinachukuliwa.

Tumeona mara kadhaa manesi wazembe au walimu wazembe wakiadhibiwa lakini sio polisi.

Wanafanya makosa, watu wanalalamika lakini hatua hazichukliwi muda mwingine aliyefanya kosa anapandishwa cheo..refer Kamanda Kamuhanda alivyoshiriki kwenye mauaji ya Mwangosi na akapanda cheo.

Please waache watu wawe na uhuru wao wa kufeel haya matukio yanapotokea. Usilazimishe deep feelings zako ziwe za wote.
Nimekupenda bure.Ndiyo sababu nasema.Polisi ni Binadamu tunatumia wa sababu tumepoteza binadamu mwenzetu,lakini ni wakati muafaka wajisahihishe.

Tuanze na Waziri wa Mambo ya ndani na IGP wetu wajisahihishe.

Huku uraiani sisi siyo nguruwe ni binadamu kama wao.

Jatuhitaji kuwa na blue and red blood wote tunared blood,blue blood tumwachie Malkia wa uingereza.

IGP aone umuhimu wa taasisi hiyo kuacha kuwa tawi la CCM.

IGP a one umuhimu wa kuona wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kutumia nafasi zao kuumiza RAIA kwa kisingizio ya uenyekiti wa Kamati ya usalama!.

Leo mwenyekiti wa Usalama wa mkoa yuko wapi??Au mwenyekiti wa Usalama wa wilaya yuko wapi??

Tuache kufanya siasa pori hazitusaidii kama Taifa.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
8,632
Points
2,000

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
8,632 2,000
Nimekupenda bure.Ndiyo sababu nasema.Polisi ni Binadamu tunatumia wa sababu tumepoteza binadamu mwenzetu,lakini ni wakati muafaka wajisahihishe.

Tuanze na Waziri wa Mambo ya ndani na IGP wetu wajisahihishe.

Huku uraiani sisi siyo nguruwe ni binadamu kama wao.

Jatuhitaji kuwa na blue and red blood wote tunared blood,blue blood tumwachie Malkia wa uingereza.

IGP aone umuhimu wa taasisi hiyo kuacha kuwa tawi la CCM.

IGP a one umuhimu wa kuona wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kutumia nafasi zao kuumiza RAIA kwa kisingizio ya uenyekiti wa Kamati ya usalama!.

Leo mwenyekiti wa Usalama wa mkoa yuko wapi??Au mwenyekiti wa Usalama wa wilaya yuko wapi??

Tuache kufanya siasa pori hazitusaidii kama Taifa.
Salute Mkuu Tetty..
Umesema kweli tupu.
 
Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Messages
6,063
Points
2,000

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2014
6,063 2,000
polisi wakiacha tu kuwa walinzi wa viongozi wa juu wa CMM na mali zao za wizi tutawapenda nakuwapa ushirikiano. Watanzania tunajilinda wenyewe hatutegemei kabisa polisi. Ndio maana milango yetu na madirisha ni ya chuma. Tunamthamini mbwa kama mlinzi muaminifu mzuri na mtiifu kuliko polisi.

Sisi kwenda kukimbilia kushtaki polisi ni formality tu. Msaada wao mkubwa unakuja pale una hela halafu unataka kulipiza kisasi au kumkomoa mtu aliyekufanyia mabaya.

watanzania wanaweza kuishi bila hofu na amani Kwa kujilindA wenyewe bila jeshi la polisi. KWASABABU JESHI LA POLISI NI WALINZI TU WA MASLAHI YA WATAWALA WAONEVU WA CCM NA MALI ZAO ZA WIZO. ukibisha nilichoandika utakuwa mtu wa ajabu sana.

Licha ya yote hayo ikifika kwenye ishu ya msiba wote tunashirikiana. R.I.P wafanya biashara wa madini, Mwangosi na Polisi
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
8,632
Points
2,000

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
8,632 2,000
Hakuna kazi ya kutii bila kufuata Sheria na Katiba za nchi.

Hakuna mahali panaposema ukiambiwa na Mkuu wa mkoa au wilaya kamteke na kumyesa Barbarosa basi unaenda kufanya tu kwa sababu umepewa amri na mkuu.

Ndiyo upumbavu na upuuzi tunaousema.Wafuate sheria na taaluma zao.Waache kuwa tawi la Chama Cha Mauaji.

Upumbavu wanoufanya kwa jamii wasifikire jamii hii haiumii,wote ni binadamu hakuna nguruwe.Tunaona mnavyokuja juu kama moto wa kifuu,hatulaani kufa au kuuawa kwa polisi tunalaani kuuawa kwa Binadamu,maana u binadamu wake ndiyo uliomfanya awe Polisi.

Upolisi ni taaluma kama taaluma nyingine ni kama Udaktari na uanasheria.Taaluma hizi tatu zinawafunga kwenye eneo moja kutetea na kulinda uhai wa binadamu bila kujali Itikadi au Ukanda wao Bali utu wao.

Tusipumbazwe na upuuzi wa wachache kufanya maovu,ni wakati wa polisi kujitafakari kama kweli wanahitaji ka kuogopewa au kuwa rafiki wa RAIA??

Enzi za JKN polisi alikuwa Rafiki na Leo.polisi ni nani??Kama Rais anawaamvia Polisi anataka RAIA iawaogope polisi,tujiulize wanapata wapi information za wahalifu??

Simchukii polisi maana ni binadamu anastahili kuishi na chukia hulka na matendo ya polisi ifike mahali wajirekebishe.

Polisi ni binadamu wanastahili kuishi na kuheshimika.Waanze kuona RAIA ni binadamu w anastahili kuishi na kuheshimika.Na bila RAIA polisi hawezi kufanya kazi yake kwa wepesi.
Asante kwa kumpa fact.
 
Na hapo ndipo low intelligence yenu ilipo, unasema Upolisi ni kama udaktari? Unajua mafunzo ya Askari wewe? Askari hatakiwi kuhoji Amri ktk kwa mkubwa wake bali ni kutekeleza tu, kama una tatizo na Askari wetu elekezea kwa watoa Amri na siyo mtii Amri, na ndiyo maana hata kwenye Mahakama za Kimataifa za kihalifu hakuna Askari anayeshitakiwa bali mtoa Amri ndiyo hushitakiwa na siyo Askari, kwani yeye hutii Amri tu na siyo vinginevyo!
 
Forum statistics

Threads 1,381,193
Members 525,998
Posts 33,791,877
Top