Tuna shamba eka 1,000 morogoro tunataka ushirikiano wa kulilima

Bin Faza

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
502
191
Waungwana,

Ninapenda kutangaza ya kwamba, tunayo ardhi ya shamba yenye ukubwa wa eka 1,000 na tunatafua wafadhili wa kuanzisha kilimo. Eneo halijawahi kulimwa na wataamu wanasema eneo hilo linaweza kulimwa bila ya mbolea kwa miaka mitano. Eneo lipepitiwa na mto kwahivo ni urahisi kupata maji ya irrigation

kilimo kinachoweza kupendekezwa ni pamona na aloe vera, sun flower na cash crops kwa pamoja.

Mtu yeyote anaweza kuivest au uanyejuwa wapi tunaweza kupata investment tuko tayari kushirikiana nae, na kutakuwa na maandishi ya kusheria baina yetu.

Kwa maelezo zaidi niandikie

ahsante
 
Waungwana,

Ninapenda kutangaza ya kwamba, tunayo ardhi ya shamba yenye ukubwa wa eka 1,000 na tunatafua wafadhili wa kuanzisha kilimo. Eneo halijawahi kulimwa na wataamu wanasema eneo hilo linaweza kulimwa bila ya mbolea kwa miaka mitano. Eneo lipepitiwa na mto kwahivo ni urahisi kupata maji ya irrigation

kilimo kinachoweza kupendekezwa ni pamona na aloe vera, sun flower na cash crops kwa pamoja.

Mtu yeyote anaweza kuivest au uanyejuwa wapi tunaweza kupata investment tuko tayari kushirikiana nae, na kutakuwa na maandishi ya kusheria baina yetu.

Kwa maelezo zaidi niandikie

ahsante

Wako wengi sana wa aina yako, waligrab land..... now awanahaha kutafuta wabia kazi kweli kweli
 
Du nkiona habari kama hizi nasikitika sana.

Mkuu sio lazima uwe na mamilioni ndio uanze kilimo (large scale) cha kufanya

  1. Nunua ngombe iether wa kienyeji ma wa kisasa wasiopungua kumi na tano wafuge kwenye hilo eneo.
  2. Tenga eneoa la kilimo cha mazao kama mpunga, mahindi, mbaazi, pamoja na matunda kama embe, papai, nk. eneo la kilimo anza hata na ekari kumi tu nakuhakikishia miaka 3 ijayo eneo litakua halikutoshi.

Kuingia ubia ndugu yangu kuna shida nyingi sana na kuna migogoro isiyoisha mfano mzuri angalia kiwanda cha UNNAT kilivyoingia kwenye mgogoro na kupelekea kufungwa kwa kiwanda na sasa kiwanda na eneo loe linauzwa.

CHELEWA UFIKE,
 
Hilo eneo liko wapi Msamvu, Kihonda, Boma Road au Kingorwila??

Wadau lazima tujue sehem halisi shamba lilipo ili tufikie uamuzi wa kuja au kutokuja. Na pia mmepataje shamba kubwa namna hiyo bila kujua matumizi yake??

Pia inaonekana mko wengi, je mko wangapi??
 
Utayaweza masharti ya investors weee, start small, upo Karibu na mto irrigate eka kumi mahindi, seci tym haitakuwa kumi utakuwa na uwezo WA ishirini
 
Kichakuro,

Nakushukuru sana kwa nasaha na mashauri yako, hiyo rai yako inaonekana inaweza kufika maendeleo kwa njia ya utaratibu na uhakika zaidi

ahsante sana
 
Sisi tupo wawili kila mmoja na eka 500 lakini waraka wa umilikaji ni mmoja tu (sisi ni ndugu) na tunalilipia kodi serekalini kila mwaka kwahivo ni ardhi halali kabisa na mtaji wa kuanzia kazi hapo inategema ni kilimo cha aina gani kitafanyika
 
ngoshas,

nakushukuru sana, kusema ukweli sijui masharti ya wawekezaji lakini ndio nimo katika kujaribu, lakini wazo la kuanza kazi ya kilimo kwa eka 10 kumi ni wazo pia zuri sana
 
The Planner,
Jirani yetu analima sun flower na anafanikiwa vyema sana, si kwamba shamba zima limezungukwa na maji, only 4,5 Km za upana wa shamba ndio zimepakana na mto kwa urefu kuko kukavu tu
 
Morogolo kubwa ndugu mkata,chanzuru,dumila,msalabani,mkono wa mara,msimba au moro ya wapi?
 
Ulukolokwitanga

Shamba tumelipata serekalini na tunalilipia kodi kil amwaka, kwahivo ni sehemu halali inayotamgulikana katik arejista za serikali.

Tupo wawili na nitakujibu hasa lipo mitaa ipi kwani bro wangu ndie aloshughulikia kulipata shamba,
 
Ulukolokwitanga

Shamba tumelipata serekalini na tunalilipia kodi kil amwaka, kwahivo ni sehemu halali inayotamgulikana katik arejista za serikali.

Tupo wawili na nitakujibu hasa lipo mitaa ipi kwani bro wangu ndie aloshughulikia kulipata shamba,

Morogoro karibu kila zao linakubali, ukitaja eneo lazima uta_attract interest za watu kibao. Kama ni jirani na mto Wami kitunguu kinakubali sana. Kama ni eneo la Mhonda kule ndio balaa kuanzia embe, nazi, machungwa, ndizi hadi Cocoa zinakubali. Kama umepima UKIMWI ukajiona uko vizuri panda MITIKI hapo baada ya miaka 12 we ni tajiri wa kutupwa, huitaji kununua miche unatengeneza nursery yako mwenyewe hapo hapo shambani, then baada ya miaka mitatu unachukua long term loan unakuwa unakula na kunywa bia taratibu huku unasubiri miti ikomae

Kama mko vizuri upstairs na mna hati ya hilo shamba hamna haja ya kutafuta wadau humu JF, fungueni kampuni, nendeni TIB mkachukue zile hela za pale Agriculture Window then pigeni kazi. Wanazila tu mafisadi akina Simon Group huku wakuwa wanalima rami wakati vijana kibao wanashindwa kuingia kwenye kilimo chenye tija kwa kukosa mitaji.
 
Ulukolokwitanga

Umeniweka kwenye wazo zuri sana, nyaraka zipo na hazina dowa na nitashughulika na hapo TIB, wao wanatowa pesa kwa mantarafu ipi, mikopo au misaada au uwekezaji?
 
Mi ngoja nijipange nitakuja kuwekeza kwenye kufuga nguruwe nikianza na nguruwe 50 sio mbaya, kisha nikafuga Moro pazuri sana kwa kuwekeza.
 
Ulukolokwitanga

Umeniweka kwenye wazo zuri sana, nyaraka zipo na hazina dowa na nitashughulika na hapo TIB, wao wanatowa pesa kwa mantarafu ipi, mikopo au misaada au uwekezaji?

Hawa jamaa wanatoa mikopo kwa ajili ya kilimo, lakini hawatoi kwa individuals, wanatoka kwa makampuni na dhamani inakuwa ni hilo shamba kama lina hati. Mikopo yao inaanzia shilingi milioni 100 na kuendelea na inawza kuwa long term loan kutegemeana na aina ya shuguli unataka kufanya. Tena kwa kilimo cha mazao kama miti unaweza kunegotiate ile miaka ambayo mitiki haizalishi uwe una_service loan kwanza hadi utakapoingia wakati wa uzalishaji ndio uanze kulipia.

Fursa zipo nyingi kama una hati na kufungua kampuni ni rahisi sana. Unajua zamani wakati wa ujamaa na kujitegemea tuliaminishwa kuwa kukopa ni bad practice, ndio maana wabongo wengi akisikia habari za kukopa anawaza kuuziwa nyumba yake au dhamana yake badala ya kuwaza kuugeuza huo mkopo kuwa profit making venture. Kazi kwako kijana, the higher the risk, the higher the return. Kama maelezo yako ni sahihi unahitaji kuwa na milioni moja tu ya kwako kujiweka katika mazingira ya kukopesheka na unaweza kujikuta una bilioni moja ya kufanyia kazi msimu wa kilimo utakapoanza mwezi wa 9
 
Kama uko serious sio lazima sana ulitumie shamba lote kwa mara moja. Tenga ten acres halafu fanya yafuatayo

1) . Nunua Ng'ombe Jike kama Kumi mpaka Ishirini
- Mitamba kams 10. Walozaa Kama 5 na Ndama 5
- Chagua Fresians, Asians na Mpwapwa (Hawa wanahimili Joto)

2) . Wazalishe kwa artifiacial Insermination (Uzalishaji wa chupa) faida yake ni kuwa unaweza chagua mbegu ya ndama uitakayo


3). Tenga tena Ekari tano lima mazao haya yafuatayo
A. Green Beans, zinauza sana, na majani yake utalishia ngo'ombe zako
B. Baby Corn (Mahindi Machanga) yanauza sana, na majani yake yana maziwa kwa ng'ombe
C. Alizeti utapata mashudu
D. Desimodiamu(kiingeereza ila sikumbuki spelling) ni majani yenye maziwa sana.


Kwa kufanya hivyo ng'ombe mmoja ataweza kukupa lita za maziwa 20 mpaka 40 kwa mkamuo mmoja. Jumla lita 40 mpaka 80 kwa siku kwa ng'ombe mmoja.


Kwa ushauri zaidi na jinsi pia ya kuwapata nitakupa mawasiliano, na ukitaka hao ng'ombe ntakuuzia na ushauri wa kitaalamu ntakupa. Pia mifano hai nitakuonesha na ntakupeleka kwa mashamba mengi.

Baada ya muda hizo ekari ulizotenga zitakuwezesha kuendesha shamba lote in five years to come.
 
Back
Top Bottom