Tuna Serikali Ya Aina gani? Viongozi Wetu wanafikiria nini?

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Rais wetu hana uchungu na nchi wala hela zetu za kodi. Kila siku ni safari za nje ambao zimefika pabaya, anadhihakiw, anatukanwa na kudhalilishwa hadi na raia wa nchi anazopenda kwenda kuomba misaada. Kitu ambacho kinatutia aibu watanzania kwani rais wetu anapoitwa " RETARD" ina maana sisi pia ni retard kwani tumemchagua sisi. Gazeti la the Guardian ikiripoti kutoka DAVOS, ilibeba maneno mazito tena machungu. Kwani rais alichokifanya na hotuba yake ni aibu. Alishindwa kuelezea mambo yote aliyoombwa kuzungumzia.

Makamu wa rais anaonekana hana kazi ya maana kwa maana yeye muda wote ana mikasi ya kukatia utepe. Yaani kila siku kwenye luninga yeye na mkasi mkononi wakati angekuwa angalau anatumia mida hiyo kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu.

Waziri Mkuu ni kama mtoto wa miaka minne, akitishwa kitu analilia lia. Hana msimamo kama kiongozi, hana maamuzi ya uongozi. Pinda anaonekana kama mtoto wa kambo, yaani yeye anaendeshwa kama mkokoteni

Spika wa Bunge. Sitaki kutumia neno baya kwa maana ni mwanamke mwenzangu tena mamangu, lakini kwa bahati mbaya ameliharibu chama tawala ndani ya bunge. Anaonyesha ubaguzi wa wazi dhidi ya wapinzania, hana msimamo na haonekani kuwa na upeo wa kufikiri au kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa. Jamani hawa viongozi wanatupeleka wapi
 
Inauma lakini kama umeligunduwa hilo anza kulifanyia kazi. Kinyume na hapo bora uhame nchi ili usipate kuaibika zaidi.
 
Back
Top Bottom