Tuna Rais mjenzi. Je, Watanzania hawawezi kujenga maghorofa, barabara na madaraja?

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,944
2,030
Wakuu, Rais Magufuli amekaa sana huko Wizara ya Ujenzi anajua kila kitu huwezi kumdanganya. Kinachoniuma Jana nilikuwa pale Philips kuna kakaravati kanajengwa kapitishe maji chini ya barabara, nilipopita Mara ya kwanza niliwakuta wabongo,niliporudi mara ya pili nkamkuta mchina amekuja kukagua. Nikajiuliza maswali; mheshimiwa dokta John Joseph Pombe Magufuli anafikiriaje haya mambo ya kuleta hawa raia wa nje kuja kufanya hizi project?

Kuna mafundi ujenzi wanamaliza pale Veta na Mlimani wanafundishwa nini huko chuoni mpaka kila project kubwa wanapewa raia wa nje?

Hili in JIPU tunalopaswa kulitumbua kubana MATUMIZI KWA KUTOLIPA KWA DOLA TUKAWALIPA WATZ WENZETU KWA SHILINGI KAMA WANAZO SIFA ZA KUJENGA MADARAJA,BARABARA NA MOGHOROFA.

Tusahauni habari za majengo kudondoka,maghorofa kuanguka,madaraja kukatika,awamu hii ya Magufuli, sehemu ya mifuko miwili huwezi changanya nusu mfuko, hili ndilo lilowapotezea wakandarasi wetu sifa awamu zilizopita.

Watanzania hatuwezi kutengeneza magari, siamini kama ujenzi unatushinda.
 
Mara nyingi kazi za aina hiyo tenda utangazwa, na tenda inaweza kuwa International tender au National Competitive Tender kulingana na nature, capital, technical nk inayotakiwa kufanya kazi hiyo. Kama ni tenda ya kimataifa kinachoangaliwa ni uwezo wa kampuni husika kufanya kazi hiyo kwa kuangalia vigezo vilivyoanishwa bila kujalisha kampuni hiyo ni ya hapa nchini au laa, japokuwa kwa tender za ndani (National) utakiwa kampuni iwe ya ndani ya nchi kufanya kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom