Tuna mikwara sana Watu wa Dar es Salaam, kila Mtu mtemi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,822
DOWN TOWN KITAMBO

Kuna Mshkaji wangu mmoja, kipindi hicho naishi Segerea.. Siku moja, ilikuwa Jumamosi, akanipitia home, akaniambia twende Mikocheni saloon.

Kweli pamoja na kuishi Segerea, bado misele yangu mingi ilikuwa around Mikocheni na viunga vyake. Sasa nikamuuliza what's so special about hiyo saloon?! , akanijibu "Jamaa wananyoa Vizuri sana".. In comparison to where? Nikamuuliza.. Haikuwa ina make sense.

Mwisho akaamua kuwa straight, akaniambia pale wananyoa Washua, Mawaziri wengi wananyoa pale. Akanitajia kwa haraka Mawaziri hao, mmojawapo Dr Hussein Mwinyi.

Still haikuwa ina make sense kwangu, driving all the way, just kwenda kunyoa, kisa hiyo saloon na Dr Mwinyi ananyoa.
Ikanikumbusha purukushani ya viti wakati niko UDSM.

Siku moja tukiwa Cafteria ya Manzese, na wenzangu ambao walikuwa serious sana na shule, tukahangaika kupata viti.

Nikaona viti viwili vya bati, havijakaliwa. Nikavichukua, nikavitoa kwa nje, mahali ambalo tunataka kujisomea.

Ile tunaanza kukaa tu, akaja Mzee mmoja, ana upara hivi. Sura si ngeni, ni Muuza Matunda pale Cafteria.

Bila kusalimia Mzee kwa sauti ya juu akatutaka turudishe viti vyake.

Mimi nilimtilia shaka kama vile viti vyake.

Nikamuuliza "Babu hivi tutajuaje kama hivi viti ni vyako?"

Babu akakomaa, akasema ni vyake. Nikawaambia "Babu hivi viti haiwezi kuwa vyako kwa kuwa tu wewe umesema ni vyako, ukiondoa Mali chache za Wana Jumuiya ya Chuo, Fenicha nyingi ni Mali ya chuo, nadhani na hivi viti ni Mali ya Chuo".

Babu akawa mkali, akahamisha hoja, akasema mimi najifanya najua. Nikajua fika Babu kashazidiwa hoja huyu, nikaamua kumkera, nikamwambia "Babu, tunahama kwenye hoja, si unithibitishie tu kwamba hivi viti ni vyako? Taja hata alama tu! Afu kuhusu kujifanya kujua, umekosea Babu, mi sijifanyi najua, najua kweli"

Daaaah, Babu alikasirika sana.. Akaniambia wewe mtoto mdogo sana kwangu, mimi nimeanza shughuli zangu chuoni miaka ya 70 huko, wewe utakuwa hujazaliwa!

Nikamwambia Babu ni kweli, ukija kwenye umri, uko sahihi, umenizidi sana. Turudi kwenye viti, hivi viti nitajuaje kama ni vyako?

Basi Bwana likazuka varangati, Babu hazungumzii tena viti. Anasema mimi nina dharau, si chochote si lolote.

Babu akaenda mbali, akasema yeye ameanza kuuza Matunda kitambo sana, mimi sijazaliwa. Na ameona watu wengi wamepita pale.

Kwa sauti ya mamlaka akaniambia "Mimi nipo hapa nafanya shughuli zangu miaka mingi sana, kina Yoweri Museveni wa naanza chuo mpaka wanamaliza ni nawaona!"
Nikamuuliza Babu, "Unamaanisha Yoweri Museveni Rais wa Uganda?"
Babu akanijibu "Ndio, huyo huyo unayemjua wewe, mimi numemuona wakati anasoma"
Nikamuuliza tena "Wakati Museveni anaanza mwaka wa kwanza we ulikuwepo hapa?" Babu akaniitikia kwa kutikisa kichwa kama dalili ya dharau, ndiooo!
Nikamuuliza tena "Ulikuwa Unauza Matunda?"
Akaitikia tena ndiooo.
Nikameza mate kidogo, nikamwambia Babu usiongee tena hivyo kwa ufahari, sio jambo la kujisifia. How comes Museveni amekuja hapa, amesoma, akarudi kwao, akahustle then akawa Rais, tena kwa muda mrefu, halafu wewe bado Unauza Matunda, na unaongea kwa kujisifia. Ina maana hakuna progress yoyote umefanya kwa miaka yote hiyo hapa chuoni zaidi ya kuuza Matunda.

Babu akakaa kimya, akajiondokea akaenda kunyanyua viti eneo jingine.

Dr Hussein Mwinyi Sasa ni Rais wa Zanzibar, yule Jamaa yangu ambae alikuwa wananyolewa saloon moja Mikocheni, bado anahangaika na Business Plans zake kwenye Flash.

Tuna mikwara sana watu wa Daslaam.

IMG_20201123_124923_3.jpg
 
View attachment 1636091
Bila mkwara Dar es salaam huli!
 
Jamaa yangu kafungua biashara mpya, anapiga hela kichizi, kafungua duka la kuuza funguo za magari na key holder zake.
Unanunua unaingung'iniza kwenye suruari kisha unaenda kutegua Pisi kali
Ha ha ha !
Dar hapa mambo ni uchizi mtupu, utapeli kwa kwenda mbele na kama ukikaa kihasara hasara imekula kwako.
Mabinti pisi kali zinaingizwa mjini kila uchao na mabraza meni wa mishen town.
 
Back
Top Bottom