Tuna la kujifunza zaidi kwa Laizer wa Tanzanite

waneemayote

Member
Oct 20, 2019
54
150
Baada ya Laizer kupiga hela ya TANZANITE mengi yamezungumzwa, Mimi nimelitazama Jambo hili katika Kona nyingine. Nimeaangalia matajiri wetu wakubwa Tanzania kuanzia wa kwanza Hadi wa 12 list yao Ni Kama ifuatavyo:-

1.Mohammed Dewji.
2.Rostam Azizi.
3.Said Salim Bakhresa.
4.Reginald Mengi.
5.Ally Awadh.
6.Shekhar Kanabar.
7.Shubash Patel.
8.Fida Hussein Rashid.
9.Yusuph Manji
10.Salim Turkey
11. Ghalib said Mohamed
12.Yogesh Manek

Kuna Mambo ya kujifunza hapa.

✓ Tuwekeze zaidi kwenye Elimu ya ujasiriamali kwani kwenye list ya watu Hawa 12 wote ni wafanyabiashara. Kwa Sasa Tanzania vijana kwa wazee wanawekeza Sana kwenye Siasa kitu ambacho kinaleta reflection ya kizazi Cha baadaye kukosa matajiri kwani kila mtu anafikiria Siasa. Rwanda wao SoMo la ujasiriamali lipo kwenye mtaala Kama SoMo la lazima kwa wanafunzi wote wa advance. Yaani ni sawa na hapa kwetu SoMo la GS.

✓ Katika list hiyo amejitokeza Mengi tu Kama mtu mwenye Asili ya kibantu na Mswahili mwenzetu. Hapa hata watoto wanaokuwa wanajengeka mentality kuwa ili uwe tajiri kazima uwe na Asili Fulani. Katika hili wanakosa Mambo makubwa mawili Moja motivation kuwa watafanikiwa wakiwekeza, lakini la Pili role Model wa kumfuata. Kwa bahati mbaya mzee wetu Mengi ameshatangulia mbele ya haki hivyo tumebakia patupu kwa Sasa. Kuna watu wanaweza kudhani Ni ubaguzi Ila Kuna Jambo la muhimu Sana hapa hasa la kutengeneza matajiri wenye vinasaba na sisi.

✓ Matajiri wengi ni wale wale, yaani hakuna matajiri wapya wanaoibuka na kuleta ushindani. Hii inatokana na watu kutokuzifahamu fursa au fursa zinapojitokeza wale wale wenye mitaji wanazichukua. Serikali Ina wajibu mkubwa Sana wa kukuza, kutoa Elimu, na kusaidiwa kitaalamu kwa wanaotaka kujaribu Jambo fulan.

✓ Matajiri wanalisaidia Taifa katika Mambo makuu mawili, moja husaidia kutoa ajira kwa raia wake. Hivyo kila tunapopata Tajiri mpya Kama Laizer tumefungua ajira mpya mahali lakini la Pili wana kazi ya kulisiaidia Taifa pale linapokumbwa na majanga kwa kuchangia. Hili la Pili ni la kizalendo zaidi, mzee wetu Mengi alifanya na ziada kwa kuwatafuta Walemavu na kukaa nao meza Moja.

✓ Maeneo mawili ambayo kwa Sasa ukiwekeza unatajirika ni kwenye ujasiriamali na kwenye uvumbuzi (hasa Technology). Matajiri wengi wanatokea kwenye Sector hizi mbili. TUWEKEZE zaidi kwenye maeneo haya. Tuwekeze zaidi kwa vijana wetu wa veta na wabunifu wetu.

✓Katika Maelezo yake Laizer anataka kujenga shule na kufungua Mall kuna maswali mawili matatu najiuliza hiyo shule anajenga maeneo gani yasiokuwa na shule? (Do we have demand of schools in Arusha?) kwa kanda ya Kaskazini hatuna tatizo la majengo ya shule, ila tuna tatizo la walimu bora na mitaala mizuri.

Ukanda wa Kaskazini una shule lukuki zenye majina makubwa mno na ufaulu Bora kabisa. Hata shule za Serikali ukanda huu zinafanya vizuri Sana na wazazi wameshaelewa wengi hawapeleki private wanakimbizia shule za kawaida hili sio eneo sahihi la kupeleka mtaji kwa Sasa.

Kuhusu mall watanzania hatuna utamaduni wa kununua vitu malls, walikuja uchumi super markets kutoka kenya walifunga walikuja shoprites walifunga NAKUMAT walifunga, Moshi kulikuwa na mr. Price alifunga. Tanzania Tuna utamaduni wa kununua magengeni na kuamini malls ni za matajiri na ni expensive.

✓Laizer ajifunze kwa jamaa aliyeitwa Askofu yupo wapi kwa Sasa huyu jamaa alipataga pesa akazimwaga tokea Gorofani watu wakapigania chini ya Gorofa, kabla ya kutumia hizo fedha atulie Kama Mwezi mmoja au hata miwili then atafute washauri wa kibiashara wamshauri. Mtaji kwa Sasa anao lakini anahitaji mshauri Bora, Kuna kitu anapaswa kukifanya na kingemlipa haswa asiende haraka atulie na atafute washauri Bora.... Wala hana haja ya kuiga biashara za watu wengine. Narudia Kuna Jambo ambalo anapaswa kulifanya lingemlipa vibaya sana.....

Kila la Kheri Laizer tunatarajia baada ya miaka 10 uingie kwenye top ten hapa.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,227
2,000
Adui wa muafrika ni muafrika mwenyewe.

Matajiri Tanzania ni wahindi na wachina wanakuja kwa kasi.

Hawapati vikwazo kwenye kuwekeza kama wabongo wanavyopata.

Ukitaka uwe tajiri bongo, hama nenda Ulaya au Marekani, utatoboa.

Muulize Mengi alichokipata alipotaka kuinunua New Afrika.
 
Pips Man

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,438
2,000
tatizo letu waswahili ndo hili ... huyo mr.laizer unaambiwa ameshashika pesa km hizo na anamall kubwa arusha na ni mdau wa elimu sana ameshajenga madarasa kadhaa kwenye shule za serikali km mchango wake hivyo anachokifanya na atachokifanya si mgeni nacho ni mzoefu na mfanya biashara mkubwa arusha...
 
troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
15,197
2,000
Mwezi uliopita kama sikosei nilikutana na taarifa mtandaoni ikisema
Kuna mzee huko mererani anaitwa Laizer miaka 17 amewekeza kwenye kutafuta tanzanite. Operation cost kwa siku ni karibu laki 6. Na hajawahi pata hata jiwe la laki 1.

Hii taarifa niliipataga Twitter na niliscreen shot na pia niliweka status.
Juzi nilipokuta hii taarifa na jina tena ni huyu mzee hakika nilijisemea imani yake imemponya.
 
blance86

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,506
2,000
Mnapocopy maandika ya watu wapeni heshima wenyewe jamani kwani unapungukiwa nn?
 
dudupori

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
1,661
2,000
Wasameheni hao mataga hawana wanachoelewa...
Duh naona watu laizer ndy wamemjua Sahv

Ova
Kwa taarifa yako Laizer ni tajiri bilionea mkubwa kabla hata ya haya mawe ya jana. Ameekeza sana mjini arusha.
Katika sekta hiyo ya madini pia ni mkomavu, kwa hiyo usifikiri kaanza jana.
Amesema atajenga kwa ajili ya jamii ya wamasai jambo ambalo ni jema pia. View attachment 1488523
Watu wengi hawamjui laizer kwakweli, huyu jamaa ndio mmiliki pia wa ile hoteli ya Manyara Inn iliyopo mirerani pale songa mbele, anamiliki mall Arusha na utajiri wake ni wakitambo tangu 2000 huko tunamsikia laiza, Anahudumia mgodi tangu mda sanaaa.... Kwa watu wa Arusha na mirerani hususan wanamjua vilivyo na kwenye sekta ya elimu amechangia sana tu...
 
Shaka Zulu Master

New Member
Apr 10, 2020
3
45
Baada ya Laizer kupiga hela ya TANZANITE mengi yamezungumzwa, Mimi nimelitazama Jambo hili katika Kona nyingine. Nimeaangalia matajiri wetu wakubwa Tanzania kuanzia wa kwanza Hadi wa 12 list yao Ni Kama ifuatavyo:-

1.Mohammed Dewji.
2.Rostam Azizi.
3.Said Salim Bakhresa.
4.Reginald Mengi.
5.Ally Awadh.
6.Shekhar Kanabar.
7.Shubash Patel.
8.Fida Hussein Rashid.
9.Yusuph Manji
10.Salim Turkey
11. Ghalib said Mohamed
12.Yogesh Manek

Kuna Mambo ya kujifunza hapa.

✓ Tuwekeze zaidi kwenye Elimu ya ujasiriamali kwani kwenye list ya watu Hawa 12 wote ni wafanyabiashara. Kwa Sasa Tanzania vijana kwa wazee wanawekeza Sana kwenye Siasa kitu ambacho kinaleta reflection ya kizazi Cha baadaye kukosa matajiri kwani kila mtu anafikiria Siasa. Rwanda wao SoMo la ujasiriamali lipo kwenye mtaala Kama SoMo la lazima kwa wanafunzi wote wa advance. Yaani ni sawa na hapa kwetu SoMo la GS.

✓ Katika list hiyo amejitokeza Mengi tu Kama mtu mwenye Asili ya kibantu na Mswahili mwenzetu. Hapa hata watoto wanaokuwa wanajengeka mentality kuwa ili uwe tajiri kazima uwe na Asili Fulani. Katika hili wanakosa Mambo makubwa mawili Moja motivation kuwa watafanikiwa wakiwekeza, lakini la Pili role Model wa kumfuata. Kwa bahati mbaya mzee wetu Mengi ameshatangulia mbele ya haki hivyo tumebakia patupu kwa Sasa. Kuna watu wanaweza kudhani Ni ubaguzi Ila Kuna Jambo la muhimu Sana hapa hasa la kutengeneza matajiri wenye vinasaba na sisi.

✓ Matajiri wengi ni wale wale, yaani hakuna matajiri wapya wanaoibuka na kuleta ushindani. Hii inatokana na watu kutokuzifahamu fursa au fursa zinapojitokeza wale wale wenye mitaji wanazichukua. Serikali Ina wajibu mkubwa Sana wa kukuza, kutoa Elimu, na kusaidiwa kitaalamu kwa wanaotaka kujaribu Jambo fulan.

✓ Matajiri wanalisaidia Taifa katika Mambo makuu mawili, moja husaidia kutoa ajira kwa raia wake. Hivyo kila tunapopata Tajiri mpya Kama Laizer tumefungua ajira mpya mahali lakini la Pili wana kazi ya kulisiaidia Taifa pale linapokumbwa na majanga kwa kuchangia. Hili la Pili ni la kizalendo zaidi, mzee wetu Mengi alifanya na ziada kwa kuwatafuta Walemavu na kukaa nao meza Moja.

✓ Maeneo mawili ambayo kwa Sasa ukiwekeza unatajirika ni kwenye ujasiriamali na kwenye uvumbuzi (hasa Technology). Matajiri wengi wanatokea kwenye Sector hizi mbili. TUWEKEZE zaidi kwenye maeneo haya. Tuwekeze zaidi kwa vijana wetu wa veta na wabunifu wetu.

✓Katika Maelezo yake Laizer anataka kujenga shule na kufungua Mall kuna maswali mawili matatu najiuliza hiyo shule anajenga maeneo gani yasiokuwa na shule? (Do we have demand of schools in Arusha?) kwa kanda ya Kaskazini hatuna tatizo la majengo ya shule, ila tuna tatizo la walimu bora na mitaala mizuri.

Ukanda wa Kaskazini una shule lukuki zenye majina makubwa mno na ufaulu Bora kabisa. Hata shule za Serikali ukanda huu zinafanya vizuri Sana na wazazi wameshaelewa wengi hawapeleki private wanakimbizia shule za kawaida hili sio eneo sahihi la kupeleka mtaji kwa Sasa.

Kuhusu mall watanzania hatuna utamaduni wa kununua vitu malls, walikuja uchumi super markets kutoka kenya walifunga walikuja shoprites walifunga NAKUMAT walifunga, Moshi kulikuwa na mr. Price alifunga. Tanzania Tuna utamaduni wa kununua magengeni na kuamini malls ni za matajiri na ni expensive.

✓Laizer ajifunze kwa jamaa aliyeitwa Askofu yupo wapi kwa Sasa huyu jamaa alipataga pesa akazimwaga tokea Gorofani watu wakapigania chini ya Gorofa, kabla ya kutumia hizo fedha atulie Kama Mwezi mmoja au hata miwili then atafute washauri wa kibiashara wamshauri. Mtaji kwa Sasa anao lakini anahitaji mshauri Bora, Kuna kitu anapaswa kukifanya na kingemlipa haswa asiende haraka atulie na atafute washauri Bora.... Wala hana haja ya kuiga biashara za watu wengine. Narudia Kuna Jambo ambalo anapaswa kulifanya lingemlipa vibaya sana.....

Kila la Kheri Laizer tunatarajia baada ya miaka 10 uingie kwenye top ten hapa.
mbona matajori hapo juu karibia wote ni muslim
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,282
2,000
Kila mwenye bilioni Tanzania ni bilionea?

Wazimbabwe wote ni mabilionea?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom