Cynic
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 5,144
- 1,648
Nadhani tuna kazi kubwa tu ya kusafisha jina na Tanzania. Leo ktk maongezi ya hapa na pale na jamaa ambao hata hawajawahi kufika Tz mmoja wao akaibua swala la maujaji ya Albinos TZ - nadhani makusudi akijua natoka Tanzania. Nikanywea kama vile nimemwagiwa maji - sikutarajia kwa kweli. Mmoja wao akaonyesha wasiwasi kwamba hata yeye anaweza kuwa victim kwa sabau ya rangi yake nyeupe. Ikabidi nianze kutetea, .. oh mara incidences kama hizo ni chache, ziko ktk sehemu chache tu,... blah blah .. ili mradi utetezi. Kwa kiasi kikubwa hawakuridhika na huu utetezi. Wanadhani hili liko ndani ya uwezo wa polisi na watu wa usalama.
Naomba tusaidiane na tujadili hili: Ingekuwa wewe ungetumia hoja zipi kusafisha jina la Tanzania/kujisafisha? Maana kwa sasa ukijulikana unatoka TZ watu wanakuangalia mara mbilimbili.
Naomba tusaidiane na tujadili hili: Ingekuwa wewe ungetumia hoja zipi kusafisha jina la Tanzania/kujisafisha? Maana kwa sasa ukijulikana unatoka TZ watu wanakuangalia mara mbilimbili.