Tuna Kazi ya Kusafisha Jina na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna Kazi ya Kusafisha Jina na Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Cynic, Mar 5, 2009.

 1. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nadhani tuna kazi kubwa tu ya kusafisha jina na Tanzania. Leo ktk maongezi ya hapa na pale na jamaa ambao hata hawajawahi kufika Tz mmoja wao akaibua swala la maujaji ya Albinos TZ - nadhani makusudi akijua natoka Tanzania. Nikanywea kama vile nimemwagiwa maji - sikutarajia kwa kweli. Mmoja wao akaonyesha wasiwasi kwamba hata yeye anaweza kuwa victim kwa sabau ya rangi yake nyeupe. Ikabidi nianze kutetea, .. oh mara incidences kama hizo ni chache, ziko ktk sehemu chache tu,... blah blah .. ili mradi utetezi. Kwa kiasi kikubwa hawakuridhika na huu utetezi. Wanadhani hili liko ndani ya uwezo wa polisi na watu wa usalama.

  Naomba tusaidiane na tujadili hili: Ingekuwa wewe ungetumia hoja zipi kusafisha jina la Tanzania/kujisafisha? Maana kwa sasa ukijulikana unatoka TZ watu wanakuangalia mara mbilimbili.
   
 2. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180

  Ndugu yangu pole. Suala lenyewe ni gumu kulieleza, acha mbali kutetea jina la nchi. The best you can do is to condemn the acts, and pretend you will talk to the Presida personally and give your advice!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kweli Mkuu, kama ulivyosema ni gumu kweli kulieleza. Nilichogundua ni kwamba habari za haya mauaji yameenea sana. Yanaandikwa/kutangazwa hadi kwenye local news outlets.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa nini tunataka kutetea? Hatuoni kutetea ni kukubali unyama unaotokea?

  Almuradi mtu hapati picha isiyo ya kweli, hakuna ubaya kukubali kuwa kwetu kuna watu hawana elimu, wanadanganywa na matapeli wanaojifanya waganga, kuna watu washirikina, tunajitahidi kutokomeza haya mambo lakini uongozi wenyewe nao matatizo.

  Ukitetea unatetea uuaji.Penye ukweli uongo hujitenga. Angalia usije kuwa kama Kikwete alivyokuwa anawakia "Darwin's Nightmare" wakati documentary imeexpose mambo ya kweli.

  Kama mtu anapata an exaggerated picture, kwamba hili jambo linatokea kila mahala, hapo inafaa kumuelewesha kuwa ingawa kuna matatizo haya kuna watu wanalivalia njuga hili.Kuna kina Mwanakijiji wamelisema sana, kuna kina Pinda, ingawa katika a "comedy of errors" sort of way overzealously and quite possibly unconstitutionally embarked on a quest to stone the albino killers, as if that is not equally gross!

  Kwa hiyo mimi sina foolish patriotism ya kukataa ukweli, kwa sababu kila mtu ana kitu embarassing kuhusu nchi yake, na ni asiyekuwa na machon ya kimawazo tu ndiye atakayekataa ukweli kwamba ukweli ni ukweli.
   
 5. A

  Atanaye Senior Member

  #5
  Mar 5, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Cynic,

  Hayo yalishanitokea, bahati nzuri jamaa walikuwa ni wakenya. sikuweza kusafisha wala kujitetea lakini nilisema tuu kama nilivyosoma katika vyanzo vya habari kuwa ni Uchawi tu! Hao wakenya kweli wakasema 'mhh ni kweli, kwani hata Mwalimu Nyerere (RIP) alitumia uchawi katika vita vya Uganda..LOL

  Kwa kweli mie binafsi sijui kama nina hoja ya kusafisha jina la Tanzania pale inapofananishwa na Uchawi- ila tu, naweza kusema Katika dunia kuna wale wanaoabudu mavituvitu ya ajabu ajabu, imani zao hazielewki katika karne hii, hivyo basi tuishi nao tu kwa amani- I do not condemn the act.

  Atanaye
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni kweli image ya nchi imeharibiwa vibaya mno na hili suala la mauaji ya maalbino. Ktk dunia ya sasa ambapo information zinakuwa transfered kwa ulimwengu mzima kwa kasi, inasikitisha kuona mTZ kwa sasa anawakilisha picha ya mtu katili, mshirikina, mwonevu wa walemavu n.k.

  Hapo wazee tumeulawanya, inabidi tubebe consequences.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na Pundit kwamba unyama kama huu wa mauaji ya Albino ni kukubali kwamba upo Tanzania lakini unafanywa na watu wachache sana kama vile katika nchi za magharibi mbali mbali wapo wazungu wanaua weusi kwa kuwa ni weusi tu bila sababu nyingine yoyote au wafuasi wa dini moja wanavyoua wafuasi wa dini nyingine. Ni kuwahakikishia tu kwamba mauaji hayo yanapigwa vita na Watanzania walio wengi.
   
 8. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hli ni jambo linaloumiza sana kichwa... siku za nyuma akati mauaji ndo yanaanza kupamba moto kaka yangu ambae yupo huko ughaibuni alinipigia simu baada ya kuon a taarifa kuhusiana na mauaji haya kutoka katika Televisheni moja ya kimataifa....nilikuwa na kazi ngumu sana kumuelewesha ni nini haswa ambacho kinatokea lakini swali lake la mwisho lilikuwa ni lile lile ambalo mimi nilikosa jibu... Serikali inafanya nini kuhakikisha ya kwamba inadhibiti mauaji haya ya kinyama kwa Albinos?

  Kwa kweli mpaka leo nikiulizwa swali hili ntakosa kwa kutokea, niweze kulijibu na kumridhisha mtu... Kitu pekee ambacho naweza kusema ni kwamba kama Watanzania tutasimama kwa pamoja na kuhakikisha ya kwamba ni jukumu la kila mmoja wetu katika vitakupambana na wauaji hawa tutaweza safisha jina letu ila mpaka sasa hali ni mbaya sana...
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nawashukuru (baija bolobi, Pundit, Atanaye, Mtindiowaubongo, Bubu Ataka Kusema na
  Mzozo wa Mizozo) kwa analysis nzuri. Baada ya kusoma michango yenu, I think next time I'll be more prepared & talking points zangu zitakuwa kama ifuatavyo: Nita:

  1. Condemn the acts

  2. Avoid denial (e.g. Rwanda hawakatai kuwepo mauaji ya kimbari, wengi hawakatai holocost)

  3. Toa picha halisi kama kuna exaggeration (e.g. elezea kwamba hizo incidences zipo lakini ziko ktk sehemu chache)

  4. Elezea kwamba waTZ wanalisema sana hili jambo kwa lengo la kulikomesha

  5. Unganisha kwa kusema kwamba hii ni crime and kwamba nchi nyingi tu zina vitu embarassing (e.g. ethnic/race/ crimes).

  Nawashukuruni tena
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nawashukuru (baija bolobi, Pundit, Atanaye, Mtindiowaubongo, Bubu Ataka Kusema na Mzozo wa Mizozo) kwa analysis nzuri. Baada ya kusoma michango yenu, I think next time I'll be more prepared & talking points zangu zitakuwa kama ifuatavyo: Nita:

  • Condemn the acts
  • Avoid denial (e.g. Rwanda hawakatai kuwepo mauaji ya kimbari, wengi hawakatai holocost)
  • Toa picha halisi kama kuna exaggeration (e.g. elezea kwamba hizo incidences zipo lakini ziko ktk sehemu chache)
  • Elezea kwamba waTZ wanalisema sana hili jambo kwa lengo la kulikomesha
  • Unganisha kwa kusema kwamba hii ni crime and kwamba nchi nyingi tu zina vitu embarassing (e.g. ethnic/race/ crimes).

  Nawashukuruni tena
   
 11. M

  Mwanafunzi Member

  #11
  Mar 6, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefurahi vyombo vya habari kimataifa vimeamua kushupalia habari hii. Tangu utotoni nilikuwa nasikia kuwa maalbino (enzi hizo: mazeruzeru) huwa wanayeyuka. Ni vizuri watu wote waelewe mauaji ya kikatili wanayofaanyiwa watu kwa sababu za kishirikina. Na si wao pekee, kuna wazee pia. Cha muhimu kama walivyosema wote waliotangulia ni kwa jumuiya na serikali ya Tanzania kutafuta jinsi ya kukomesha unyama huo.
   
 12. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2015
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mbona bado?
   
 13. nistdanavigator

  nistdanavigator JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2015
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 718
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo kuna kipindi cha CNN kuhusu nchi za Africa kilipofanya kipindi Tanzania walitoa ripoti kuwa watanzania wengi wanaamini katika uchawi na watu wakapinga sana hapa jamiiforums lakini sasa yaani hatuwezi hata kujitetea kabisa tena kwa haya mauaji yanayohusishwa na ushirikina.
   
 14. mng'ato

  mng'ato JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2015
  Joined: Oct 27, 2014
  Messages: 6,247
  Likes Received: 3,854
  Trophy Points: 280
  kuna watu wanasema hakuna albino mmasai lkn nadhani wamasai hua wanawaua hao watoto wakiwa wadogo
   
Loading...