Tuna haki ya kuidai fidia TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna haki ya kuidai fidia TANESCO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BongoLogik, Jun 26, 2011.

 1. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ikiwa unatumia LUKU na umenunua na kuweka umeme wa kutosha kwa matumizi yako mbali mbali, kama vile TV, music system,fridge, cooker etc. ina maana umelipia huduma ya umeme na hivyo inatakiwa upate umeme kwa kulingana na kiasi ulichonunua na kwa wakati muafaka, sasa inapotokea TANESCO wanakata umeme ovyo ovyo kwa sababu ambazo tumechoka kuzisikia miaka nenda rudi bila kuona juhudi za makusudi kukabiliana na kutatua tatizo hilo na badala yake tunapewa misamiati kama mpango mkakati,mpango kabambe,upembuzi yakinifu, mchakato unaendelea,mkandarasi ameshapatikana n.k inanisaidia nini mimi niliyeshanunua perege wangu kilo tano au kumi na kuwaweka kweye friji nikiwa na imani nitasogeza siku kadhaa, leo nina hasira nilinunua perege wangu juzi mama watoto akawaweka kwenye friji, nimeamua nishinde nyumbani jumapili hii ili tujinome ubwabwa kwa perege na familia yangu, nimeshindwa kumuelewa mama watoto eti perege wamechina kisa nini?! kisa kukatika ovyo kwa umeme! hivi hawa TANESCO wanadhani mimi nitakula nini leo na familia yangu? sasa naona hawa TANESCO wanataka kutupangia ratiba ya milo majumbani kwetu! imebidi mama ambilikile(mwanangu anaitwa ambilikile) akaniombee mlenda kwa shosti wake nikala na ubwabwa na sasa nataka nielekee palee nikapate tusker bariiidi nipunguze kama si kuongeza ghadhabu. Mimi nadhani tuna haki ya kudai fidia kwa TANESCO, ni kama vile mtu anapolipia huduma ya ulinzi kwa mwezi mmoja kwenye kampuni fulani ya ulinzi halafu walinzi wasifike kwenye lindo siku kadhaa ndani ya siku ulizolipia na uhalifu ukatokea, si utakuwa una haki ya kudai fidia? na sio wakuambie eti kwa kuwa walinzi hawakuja lindo siku tatu basi watazifidia hizo siku! si inatakiwa walipe hasara iliyotokana na uhalifu huo? hivyo hivyo na TANESCO inatakiwa wanilipe perege wangu na pia kwa wengine wote walioshapata madhara na hasara kwa kukatika umeme ovyo ovyo.
   
 2. I

  Igangilonga Senior Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yaani leo ndo umenifungua macho!! Sikuwahi kujua km hiyo ni haki yangu, baada ya kusoma hii topic yako nimegundua kuwa kweli Tanesiko hawatutendei haki kabisa. Nadhani wengi pia hawalijui hili..... Km ni hivyo bora warudishe zile mita zao za zamani ambazo unatumia then end of month ndo wanakutumia bill but hii ya kulipia kabla then wanashindwa kutu-supply umeme sio haki kabisaaa. Pole kwa kupata hasara ya kuoza perege wako kilo 10, nakushauri kesho nenda Taanesiko head-office omba kuonana na kibosile wao yoyote na ukifika mmwagie hao perege wanukao usoni kwako then timka manake ukisema udai, hadi ulipwe sio leo inaweza kufika mwaka 2020
   
 3. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na bahati nzuri sijawatupa kwa maana inatia uchungu sana, sasa umenipa akili, nitakachofanya nitawapack vizuri then nitawaDHL kwa mkurugenzi wa tanesco ndg. william mhando nikiambatanisha na hati ya madai.
   
 4. I

  Igangilonga Senior Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  teh teh teh
   
 5. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sijajua kama kuna kifungu cha sheria kitakachotusaidia sisi wateja, nina imani kama kungekuwa na kifungu Tanesco wangeshika akili kama sio adabu.
   
Loading...