Tuna ardhi ya kutosha au hatuna akili za kutosha?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna ardhi ya kutosha au hatuna akili za kutosha?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, May 19, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Wale wanaoogopa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, moja ya hofu yao kuu ni kuporwa kwa ardhi yetu! Watanzania hawa ukiwasikiliza kuhusu Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, wengi wanatahadhalisha kwamba lazima tuwe makini kwavile nchi tunazoungana nazo zina matatizo makubwa ya ardhi wakati sisi tuna ardhi "kibao"! Watanzania wengi tunaogopa commercial agriculture, hususani itakayofanywa na wageni-hofu yetu kuu ni kuporwa ardhi yetu! Tunaogopa tusije porwa "our abundant land!" Hata Rais wetu nae anajigamba kwa majivuno kwamba tuna kila sababu ya ku-promote KILIMO KWANZA kwavile TZ ina ABUNDANT LAND!! Hivi ni kweli tuna ardhi ya kutosha hapa Tanzania? Je, TUNA ARDHI YA KUTOSHA AU HATUNA AKILI ZA KUTOSHA za kuibadilisha ardhi iliyopo kuwa economic activity?! Hadi mwaka 1888, Amerika ilikuwa imetenga kiasi cha ekari milioni tatu kwa ajili ya Indian Territory mahususi kwa ajili ya Native Indians! Mwaka 1889, serikali ikaamua kuigawa ardhi hiyo kwa ajili ya makazi na kilimo kwa mtindo wa FIRST COME FIRST SERVED. Baada ya masaa machache tu, tangu waanze kugawa ardhi hiyo, ekari zote milioni 3 zilikuwa zimeshachukuliwa! Je, sisi Watanzania tuna ardhi ya kutosha au hatuna akili za kutosha?! Tuanze na wewe unayesoma thread hii! Assumption yangu ya kwanza ni kwamba wewe upo Dar es salaam lakini hapa Dar es salaam sio nyumbani kwenu kwa asili! I hope utakuwa unatoka mkoa fulani ukiwa na asili kwenye kijiji fulani haijalishi hata kama hujawahi kuishi huko! Je, una ekari ngapi za ardhi ( sio za baba yako au babu yako au za kurithi) kutoka kijijini kwenu ambazo umezihangaikia wewe mwenyewe?! Una ekari ngapi za ardhi ulizononunua sehemu nyingine ya nchi?! Tunaoishi Dar es salaam na miji mingine; je kila mmoja ana kiasi gani cha ardhi huko vijijini? Hivi kweli wote waliopo vijijini, hususani vijana wana ardhi?! Jiji hili la Dar es salaam lina wakazi wangapi wasio na shughuli maalumu?! Na miji mingine je? Hivi hawa wote wakisema warudi vijijini na kila mmoja kujitwalia angalau ekari tano tu za ardhi na kuzifanyia kazi; je kweli Tanzania itabaki kuwa na abundant land? Kuna taasisi moja inajiita HAKI ARDHI! Waheshimiwa wa Haki Ardhi, hivi kweli wafanyakazi wenu wote hapo wana ardhi?! Je, ni Watanzania wangapi walijaribu kupata ardhi wakanyimwa kila walipoenda?! Sina hakika kama hoja yangu imeeleweka!! Hoja yangu kuu ni kwamba tuache kujigamba kwamba tuna ardhi ya kutosha wakati Watanzania walio wengi hawana hata kipande cha ardhi! Tuache kujigamba kwamba tuna ardhi ya kutosha wakati ukweli ni kwamba hatuna akili ya kutosha ya kuitumia ardhi yetu! Tuache kulalamika na kuwapigia kelele wenye akili za kutosha walioamua kuitumia ardhi yetu baada ya kuona sisi wenyewe tumeshindwa kazi hiyo!
   
Loading...