Tumzungumzie Dkt. Tulia Ackson baada ya kupata ubunge Mbeya Mjini

Sukuma Gang ni nini au ni nani?

Rais wa sasa alikuwa VP, baada ya kifo cha #1, kikatiba ameapishwa na kuwa #1; je na yeye ni Sukuma gang kwa kuwa alikuwa VP kwa miaka 5 ya kwanza, then JPM akamteua kuwa running mate kwa kipindi cha pili?

VP wa sasa alikuwa boss wa TRA kwa uteuzi wa JPM then waziri wa fedha, je, nae anaweza kuwa kuwa sukuma gang simply SSH alimkuta ni waziri wa fedha?

Chongolo ambae ni katibu mkuu CCM, ni JPM ndie alimpa u-DC. Je nae ni Sukuma Gang kwa kuwa SSH alimkuta akiwa DC

Naibu katibu Mkuu CCM bara alikuwa RC na SSH akamsogeza kwenye chama, nae aondolewe kwa hii dhana na sukuma gang?

Rais SSH amemrithi kila mtu aliekuwa kwenye serikali wa JPM na yeye akiwa VP ni sehemu ya serikali. Je avunje bunge lote na kuanza mchakato ili aepukane na Sukuma gang?

Kama kuna hoja ambayo inapwaya na inakosa logic na kuonekana fulani ni sukuma gang na fulani sio wakati watu walio kwenye mfumo wa utawala by 95% SSH kawakuta nae alikua sehemu ya mfumo huo huo.

Ni kama wakati wa JK kulikuwa na kundi linaitwa wanamtandao, yet baada ya tume teule ya bunge kuundwa na Spika Sitta (ambae nae wanasema alikuwa mwanamtandao) EL akalazimika kujiuzuru nafasi ya u-PM;

Kuna dhana huwa tunazijengea hoja ila zinakosa uzito na depth ikiwamo hii ya sukuma gang. Unless kama kuna criteria ziwekwe wazi ili kuwa na rejea kuliko kubaki na hisia.
Wakati ndio huu Sasa tumuone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom