Tumzuie rais kuteua kwa kulipa fadhila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumzuie rais kuteua kwa kulipa fadhila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  [​IMG]
  Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 28 December 2011

  [​IMG][​IMG]
  MOJA ya sababu za baadhi ya watu kutaka katiba mpya, ni madaraka makubwa aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muungano. Ubaya wa madaraka haya, ni kule kuyatumia kulinda maslahi ya watawala .

  Katika wiki moja tu Rais Jakaya Kikwete ameonyesha vipi anaweza kutumia madaraka hayo ya kufisha na kufufua mara mbili. Na kwa kweli, wapo wanaoamini kungekuwa na taratibu za kupitia maamuzi ya Rais katika baadhi ya uteuzi wake, majina mengine yangekataliwa na umma.

  Tumeona jinsi alivyowarudisha "kwenye anga" na hata kuwapa "unga zaidi" makada walioshindwa katika harakati za kugombea ubunge. Walishindwa siasa, umma ungeyakataa majina mengine.


  Lakini kwa sababu zisizofahamika wazi, Rais Kikwete amewateuwa mawaziri wake walioshindwa kwenye uchaguzi – Dk. Batilda Buriani, Deodorus Kamala na Philip Marmo, kuwa mabalozi.


  Ni wazi kuwa wateule hao wa Kikwete, si wanadiplomasia kitaaluma. Hivyo kuteuliwa kwao kunalenga kubebana na kulipana fadhira kutokana na machungu waliyopata kwa kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge.


  Swali ambalo wengi wanajiuliza ni hili: Rais hajaona Watanzania wengine wazuri na wenye sifa wa kuwapa nafasi hiyo? Au wenye haki ya kushindwa katika siasa na kupewa uhai mpya ni wanachama wa CCM tu?


  Kwa hivyo ni rahisi wananchi kuanza kufikiri kuwa kuingia CCM ndio njia muafaka ya kujijenga kimaisha maana ukigombea na kushindwa, utazawadiwa ukuu wa wilaya, au mkoa, au mwenyekiti wa bodi ya mashirika ya umma na hata ubalozi.


  Na kwa maana hiyo tunaanza kutoa picha mbaya kwamba ubalozi si taaluma na kazi endelevu bali ni kazi ambayo inaweza kufanywa na yeyote aliyedoda.


  Je, umma unaweza kumuachia mtu mmoja tu, atumie "busara" yake katika maamuzi yenye athari kubwa kwa nchi wakati kuna vyombo vilivyopewa dhamana kubwa kama Bunge bila hata kuwa na sauti ya kuhoji? Si ajabu basi Rais Julius Nyerere aliposema mamlaka aliyonayo yaweza kumfanya kuwa dikteta.


  Miaka 26 tokea aondoke, uwezekano wa kuwa na rais dikteta kutokana na mamlaka aliyopewa chini ya katiba ungalipo; na hasa kama rais tuliyenaye hajawa dikteta lakini anafanya maamuzi yanayotia shaka katika picha kubwa ya taifa.


  Na picha kubwa si ya mabalozi tu: Kikwete ameteua viongozi wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akiwemo Jaji mstaafu Damian Lubuva na Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid.


  Nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa, Kikwete ameshauriwa na nani kumteua Jaji Hamid kuwa makamu mwenyekiti wa tume hii?


  Hivi amechaguliwa yeye kwa sababu tu kuwa ni Mzanzibari, kwa sababu ya kujaza tena nafasi ya kuondoka kwa Mzanzibari mwengine Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Makungu? Au kuna kigezo gani kingine kimetumika?


  Sihoji utamaduni mbaya unaoendelezwa wa Wazanzibari kutoteuliwa wenyeviti wa tume hii au kamisheni za serikali ya Muungano, ninachoangalia zaidi ni nafasi hiyo kupewa Jaji Hamid kama kwamba hakuna raia mwingine mwenye sifa.


  Katika miaka yake 22 ya ujaji mkuu visiwani Zanzibar, Hamid alisimamia uonevu mkubwa uliokuwa ukifanywa na vyombo vya dola dhidi ya upinzani tokea ulipoanzishwa tena mfumo wa siasa za vyama vingi, zikiwemo kesi za uhaini.


  Aliachia mahakama itumiwe kukomoa wapinzani kwa kuwasweka rumande, kuchelewesha kesi zao, kuzima mashtaka yao binafsi na hata kushutumiwa kwa kusikiliza amri za wanasiasa katika maamuzi ya kimahakama.


  Kesi za waandishi kadhaa zilirindima katika Mahakama ya Zanzibar na nyengine mpaka leo hazijaamuliwa. Nyingine zimebaki kama kitanzi kinachosubiri kukaba.

  Majuzi alikabwa koo na Chama cha Mawakili wa Zanzibar (ZLC) kutokana na kitendo chake cha ubinafsi kilichofanikisha kumpa mwanawe Fatma Hamid Mahamoud kuwa jaji wa makama kuu ya Zanzibar.

  Yeye mwenyewe alihusishwa na kitendo cha kuajiriwa upya kinyume cha taratibu ilhali akiwa ameshastaafu na hivyo kunasa fedha zake za pensheni na kisha kurudi tena ulingoni kwenye mahakama, huku wengi wa wanasheria wakiamini katika wakati wake mahakama ilikwama kustawi.


  Huyo ndie mtu ambaye Rais Kikwete amemtwika madaraka mengine tena ya kushika nafasi muhimu katika taasisi ya kusimamia uchaguzi wa ushindani na ambaye mambo yakienda sawasawa ataendelea kuwa madarakani wakati Katiba Mpya itapokuwa tayari 2014 na Uchaguzi Mkuu kufanyika 2015.


  Katika hali ya mabadiliko makubwa ya kisiasa na uwazi nchini, wengine tunaamini pia katika kutia fikra mpya, zenye mitizamo na matumaini mapya na sijui kwa nini hadi leo kigezo cha uongozi nchini kinategemea mambo ambayo kwengineko si vigezo tena.


  Kwa mfano, nafasi zote kubwa hapa nchini hupewa watu wa umri mkubwa, wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na wanaolipwa fadhila. Katika hili, rais hajali taswira ya mteuliwa mbele ya macho ya umma, wala hatizami uadilifu wake.


  Tunajua na tunaheshimu mamlaka ya rais ya kuteua, na tunajua na tunaheshimu kifungu cha katiba kinachosema hapaswi kufuata ushauri wa mtu yeyote yule, lakini ni njia ipi inayoweza kutumika kuudhibiti ubinaadamu wake kama vile kutenda upendeleo wakati wa kutenda kazi zake?


  Mfano hai, ni uteuzi wa majaji na mabalozi aliyoufanya sasa.


  Ni vema Rais Kikwete akafahamu kuwa mteule wake – Jaji Hamid - wengi hawamuamini na kumheshimu. Wanajua kuwa hawezi kusimamia haki ya kiuchaguzi ikiwa haki ya kimahakama alishindwa kuitoa.


  Pamoja na kwamba watu wanauheshimu uteuzi wako kwa kuwa umeufanya kwa mamlaka ya kikatiba, lakini umewafumbua macho wengi waliokuwa nyuma kuhusiana na suala zima la madaraka ya rais.


  Najua pengine hili halitakugusa au kukukera, lakini angalau tutakuwa tumesema, na rekodi itakuwepo kuwa tumesema na tumekwambia, lakini kwa mujibu wa tabia za viongozi wa ki Afrika, haitumainiwi kuwa utatengua uteuzi wako.


  Ndipo nisemapo wananchi wasifanye kosa katika suala la Katiba Mpya. Na moja ya mambo ya kuhimiza kuwemo ni kuleta kifungu kinachoshurutisha uteuzi wowote wa rais kuhojiwa au kuthibitishwa na mihimili mingine ya dola.


  Tunataka kuzuia uteuzi kwa misingi ya usuhuba, kulipa fadhila au kubeba watu wa chama chake.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hii itakuwa Vizuri kweli, kuondoa kulipana fadhila Mfano Mzuri Batilda Buriani hakufaa ubunge Arusha akapenyezwa akashinda akalazimishwa kukata rufaa akashidwa rufaa, angalia akapewa Ubalozi Eti Kenya awe karibu na Jimbo la Arusha ili awe karibu kila mara awe anakwenda Arusha kuangalia hilo jimbo na kama ikiwezekana agombee

  Katiba Mpya Ipige Mrufuku kabisa kwa Rais kufanya fadhila kama hizo; mfano mzuri Rais wa Zambia kakomesha hayo....
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  ....Hili litawezekana kama itapatikana katiba mpya ambayo itahakikisha wateuzi wote wa Rais wapate baraka toka bungeni angalau kwa kupata 60% ya kura zote za Wabunge wa vyama vyote vilivyo na Wabunge.
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana na wewe ndugu, lakini hilo kwenye red litawezekana kweli, will it be practical? Kwenye nchi ambayo rais anateua mpaka viongozi wa wilaya, tunaweza ligeuza bunge chombo cha kupitisha wateule wa raisi.

  Maoni yangu::

  Bunge lipitishe vyeo muhimu kama waziri mkuu (kama ifanyikavyo sasa), waziri wa fedha, gavana wa benki kuu, jaji mkuu, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama i.e JWTZ, TISS, JKT, POLISI nk. Hawa wote wapitie heavy scrutiny na sio kuteuana kwa sababu za "USHEMEJI".

  Hawa wengine, tutengeneze vigezo ambavyo vitazuia mtu "yeyote" kupewa kazi "yeyote". Kwa mfano tuwazuie watu ambao hawana elimu ya diplomasia kuwa wanadiplomasia. Huwezi kuwa msimamizi wa mazingira halafu ghala baada ya kushindwa uchaguzi unageuka kuwa diplomat. Ni udhalilishaji wa taaluma ya diplomacy.
  Na hawa kina "ENG STELA MANYANYA", kama atutawang'oa kabisa nao tuwawekea vigezo vikali, elimu ya uongozi, tena ikiwezekana iwe Masters degree. Haiwezekani tukawapa madaraka ya kuongoza the so called "kamati ya ulinzi na usalama za mikoa na wilaya" ambako wanafanya kazi za "kubaka" haki za raia.

  Tuna kazi ngumu kwenye katiba mpya.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzee wa cutting za magazeti tunaomba source!
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  ngoja nijipitishe pitishe kwa mkuu naona kuna nafasi ya Ombeni ipo wazi,nitamkumbushia mkuu enzi zile tulipokuwa middle school
   
 7. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2012
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kwenye red, hivi stela manyanya ni engeneer/mhandisi au technician/fundi mchundo. Maana naona kabisa hana elimu ya kuitwa mahandisi ama in kawaida ya chama cha magamba kujigawia vyeo/sifa fake. Huyu mama ana diploma tu, haitoshi kujiita mhandisi ili mradi tuu apate sifa ya kijinga kwenye siasa.
   
 8. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Si alisema urais wake hauna ubia, anafanya nn sasa.
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  oi Bunge lenyewe hili oi... Yale Yale  ''nisipo sain wabunge wa ccm hawatanilewa''
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  dr.Kamala

  Dr. Batilda Buriani

  Joel Bendera

  Mwantumu Mahiza

  Phillip Marmo.

  NA BAAAAAAAAAAAAADO TUTAIMBA HALLELLUYAH
   
 11. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #11
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.Suala la msingi ni kuhamasisha watu/wananchi tuking'oe hichi chama cha magamba madarakani.Kama CCM ingekuwa makini wangeweka utaratibu mzuri wa hizi nafasi kuepuka kuleta hisia mbaya kwa jamii.Inaelekea CCM mtu akishakuwa mwenyekiti basi chama kinageuka chake na familia yake.
   
 12. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tatizo lipo hapo kwenye RED maana watawala wa CCM wanajua faida wanayoipata kutokana na udhaifu wa katiba iliyopo; sikiliza wanaokwenda kuongea na JK kuhusu suala la katiba mpya, jambo la kwanza analolazimisha kukubalika ni kwamba katiba iliyopo ni nzuri (eti kwa kuwa imetufikisha hapa tulipo). Lengo la watawala wa CCM limekuwa kutumia mwanya mdogo wanaoupata kulinda udhaifu wa katiba iliyopo. Tangu awali watawala wa CCM wamekuwa reluctant na suala la katiba; kumbuka:
  • Waziri wa katiba alisema hakuna sababu ya katiba mpya
  • akaungwa mkono na mwanasheria mkuu
  • hata suala lilipokwenda Bungeni, spika wa bunge naye anathibitisha utamu wa udhaifu uliopo
  • pia wabunge wa CCM wameshibitisha hilo
  Kwa hiyo kupata Katiba mpya itakayoziba matundu ya udhaifu uliopo sasa ni shughuli kubwa, itakayohitaji jasho, tena ikiwezekana jasho la damu maana CCM wameshaweka yamini kutawala kwa miaka 50 ijayo. Wanajua wakikubali katiba nzuri sasa, hawawezi kukaa madarakani zaidi ya miaka 10 ijayo, na hilo linahatarisha mwendelezo wa ulafi wa keki ya Taia kwa mgongo wa katiba.

  Tatizo ni kwamba Watanzania wa kupigania katiba ya kuiondoa CCM ni wachache sana maana wengi tumeadhibiwa kwa umasikini na ujinga, silaha ambazo CCM imezitumia kukaa madarakani kwa miaka 50 iliyopita. Bado sioni mwanga kwa sababu mchakato wa kuipata katiba mpya ambayo ingeziba udhaifu uliopo sana umeshaharibika tangu ingali mapema. Walilotaka linatimia kwa sababu
  • tutakimbizana na kesi za kupinga utaratibu wa kupatikana kwa katiba mpya, jambo ambalo wao wanalitaka
  • mwisho watasema kimsingi wadau wengi wamekubali katiba iliyopo bado ni nzuri au
  • watahakikisha udhaifu unaowanufaisha sasa hauguswi
  Najiuliza na bado sipati jibu la tunafanye nini kuhakikisha katiba inapatikana na inakuwa na uwezo wa kuwabana wanasiasa wasiwe na uhuru wa kutekeleza udikteta wao nyuma ya pazia; wametushika pabaya!
   
 13. M

  Mlawa Zahir Member

  #13
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawewe kwa kuwa baba ako amekosa nafasi unaanza majungu kama baba ako akiteuliwa unasema hayo ama kwa kuwa huenda akakosa unaleta majungu
   
 14. pascal1989

  pascal1989 Member

  #14
  Jan 19, 2014
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona mawaziri ni wale2 wengine hata hawajasomea wizara hz
   
 15. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2014
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,485
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  hii mada naiona ina make sense
   
Loading...