Tumwombee mwenzetu!

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,964
2,000
Habari zenu wapendwa wana JF. Nasikitika kuwafahamisha kuwa kuna mwanachama mmoja wa JF yuko mahtuti hospitali ya Aga Khan.

Huyu ni mwanachama ambaye namfahamu kwa kina lakini ni kwa ajili ya JF. Bila JF nisingeweza kufahamiana naye.

Ni mwanachama pekee ambaye wakati wa kutoa mahari yangu mkoani Kilimanjaro aliambatana nami na alijitolea kwa siku tatu kunisindikiza kwa usafiri wake pamoja na mmewe ambaye pia ni mwanachama wa JF. Ni vigumu kukutana na watu wa namna hii (mme na mke) wenye upendo kwa mtu ambaye wamekutana naye online tu wakubali kutoa magari yao kusafiri tokea Dar kwenda Kilimanjaro na kusimamisha kazi zao kwa muda wa siku tatu huku wakitumia gharama zao kwa kila kitu.

Mwanachama huyu alianza kuugua tangu mwezi wa nne (au tatu) akisumbuliwa na kichwa na sasa anapumua kwa nguvu za mashine. Ninapoandika hivi bado hali yake haijawa nzuri kabisa.

Kwa walio Dar mnaweza kuwasiliana nami ili tuweze kukutana na kwenda kumfariji walau mmewe ambaye nahisi yuko hospitali hapo (maana simwoni online kwa sasa).

Nawaomba tushirikiane kumwombea mwenzetu huyu na naamini ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwenzetu huyu.

Ukimaliza kusoma ujumbe huu pata walau sekunde kadhaa kumwombea mwenzetu huyu (sala ama dua) ili apate kupona na kurejea kuungana nasi.

NB: Samahani sijaandika nicknames wanazotumia hapa kwakuwa sijapata baraka za kuandika hivyo.

Ahsanteni
 

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,408
2,000
Nami naungana nanyi katika kumwombea. Mwenyezi Mungu Amjalie Neema Apate Ahueni na Kupona. Amina.

Nawapa Pole Wote Wanaouguza.

SteveD.
 

Alnadaby

JF-Expert Member
Sep 28, 2006
506
0
Ewe Mwenyezi Mungu,Muumba wa Ulimwengu na Viumbe vilivyomo,Ewe mwenye sifa ya kuumba na kuumbua,mpe uhai ndugu yetu na umbariki kwa rehema zako.AMIN.
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,964
2,000
Kamanda,
Tupo pamoja katika kumwombea!
kibunango, shukrani. Naamini kila mwana JF ambaye angekutana na mama huyu angejikuta anapata rafiki kweli. Hata mmewe pia ni mtu mzuri sana. Naamini akiingia online ataandika chochote ama kujitambulisha.

Nawasiliana nae kujua nini kinaendelea. Nitaenda hospitali hapo badae kidogo
 

Kinyau

JF-Expert Member
Nov 24, 2006
910
1,000
asante kwa ujumbe, unajua jf imekuwa kama familia, unaweza kukutana na watu wakarimu sana humu na mmoja wetu anapofikwa na tatizo ni tatizo letu sote. Mungu Muumba wa vyote amjalie afya, ampe mumewe nguvu na faraja waakti wa kuuguza.
 
Last edited by a moderator:

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
615
0
Mwenyenzi Mungu mpe nafuu huyu mwenzetu... Pia uwape familia nguvu na faraja katika kumuuguza.... Pia madaktari wake nao uwape nguvu ya kumhudumia vyema.... Amina!!
 

DMussa

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
1,314
1,500
Mac,
Ahsante kwa hizi taarifa....
Na mimi pia naungana na wanajamii wenzangu katika kumuombea mgonjwa apate nafuu na apone kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Zaidi pia Mungu amjalie mumewe apate ujasiri na amani katika kipindi hiki kigumu.

Amani ya Bwana na iwe nanyi wote - amen
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,964
2,000
asante kwa ujumbe, unajua jf imekuwa kama familia, unaweza kukutana na watu wakarimu sana humu na mmoja wetu anapofikwa na tatizo ni tatizo letu sote. Mungu Muumba wa vyote amjalie afya, ampe mumewe nguvu na faraja waakti wa kuuguza.
Hilo ndilo nimeligundua kinyau, huyu kwangu badala ya kuwa mwana JF mwenzangu tu nimejikuta namwona kama dadangu na kwa upande mwingine ni shemeji yangu!

Nafurahi ninapojua wana JF wenzangu ni wazima wa afya, inasikitisha pale magonjwa yanapowaandama. Najua kila jambo lifanyikalo linakuwa na sababu yake. Muhimu ni kumwomba Mungu amjalie afya njema na amponye dhidi ya ugonjwa unaomsumbua.

Ahsante
 

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,085
2,000
Eee Mungu wewe muumba wa vyote ambaye kwako hakuna lisilowezekana tunaomba kwa ajili ya mwenzetu aliyeko hospitali ya Agha Khan hatuna haja ya kumtaja jina ww wamjua kwani ulimuumba. Tunaomba umjalie afya ili arudi tuweze kuendelea naye kujenga ufalme wako. Pia Mungu tunaomba faraja yako juu ya mumewe ambaye anamuuguza mgonjwa, ni ukweli usipingika kwamba faraja ya kweli yatoka kwako hivyo tunaomba umjalie. Amina.
 

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,102
2,000
Eee Mungu wewe muumba wa vyote ambaye kwako hakuna lisilowezekana tunaomba kwa ajili ya mwenzetu aliyeko hospitali ya Agha Khan hatuna haja ya kumtaja jina ww wamjua kwani ulimuumba. Tunaomba umjalie afya ili arudi tuweze kuendelea naye kujenga ufalme wako. Pia Mungu tunaomba faraja yako juu ya mumewe ambaye anamuuguza mgonjwa, ni ukweli usipingika kwamba faraja ya kweli yatoka kwako hivyo tunaomba umjalie. Amina.

Hii inafariji kusema kweli. Am impressed. Wana JF tuendeleze ushirikiano huu!
 

Single D

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
458
195
Tunamwombea mwenzetu,rafiki yetu na ndugu yetu mwana JFapone haraka.
It is through the Almighty God love that she will get well because his mercies have no limit,They are new every day.Amen!
 

ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,901
2,000
Tunamwombea mwenzetu,rafiki yetu na ndugu yetu mwana JFapone haraka.
It is through the Almighty God love that she will get well because his mercies have no limit,They are new every day.Amen!


Eee Mwezi Mungu! Nakuomba umuafu huyu mwanaJF mwenzetu na maradhi yanayomkabiri, umpunguzie maumivu na iwapo maradhi yanayomkabili ni matokeo ya shari za wanadamu waovu, basi twaomba umuepushe na shari hiyo na iwapo ni mapenzi yako kwa mja wako, twaomba umponye haraka kwani ni miongoni mwa waja wako wenye kutambua utukufu wako.

Aaaaaaamina
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,951
2,000
MKuu tupo pamoja nawe tunamwombea kwa Mungu ili aweze kupona mapema..
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,272
2,000
Ewe mtawala wa milki zote na muumbaji wa vyote vilivyopo
Ewe mfalme usiyeonekana na mlinzi wa wanadamu
Ewe mponyaji usiyeshindwa na mbora kuliko wote
Ewe uliyekuwako, uko na mwenyekuja
Bwana Mungu Mwenyezi

Tunakusihii sana katika Jina la Bwana
Unyoshe mkono wako wa uponyaji
Na kwa nguvu za Roho wako zilizomfufua mwanao
Zile nguvu zilizofungua milango ya kuzimu na kuwatoa wafu
Zile nguvu zilizomrudishia uzima Mfalme Hezekia aliyekuwa karibu ya kufa
Zile nguvu zilizomnyanyua yule Kiwete kwa amri ya Mtume Petro
Unyoshe mkono wa uponyaji wako juu ya mgonjwa wetu

Wewe unamjua kwa jina na kila hali
Kwani ni wewe uliyemuumba
Na twatambua hufungwi na ujuzi wetu, muda au mahali
Unafanya kazi nje ya mamlaka ya wanadamu
Basi saa hii na dakika hii tunatangaza uzima na afya katika mwili wa mgonjwa wetu!

Tukiamuru nguvu za kuzimu na kampeni za Shetani kushindwa
Zitetemeke na kusinyaa
Zikauke na kuvunjika, zibomoke na kusagwasagwa ziwe tikitiki
Na uzima umrejee dada yetu na ainuke aweze kusimama na afya
Ili aweze kukutumikia wewe, familia yake, ndugu, na Taifa lake!

KATIKA JINA LA FAHARI NA UTISHO LA BWANA YESU KRISTU!

And the people of God say...
 

ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,850
1,250
pole sana hata mimi nimesikitika mno,ningekuwa sijaanza UE ningeenda kumuona jamani ,ni ndugu yetu huyo wa baba mmoja JF.
 

Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
642
0
Eeeeh Mungu Mwingi Wa Rehema Nyosha Mkono Wako Kwani Hakuna Usilo SHINDWAKtk Jiana La Yesu Pokea Uponyaji, Amina
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom