Tumweke Magufuli pembeni, Tumwangalie Majaliwa

Rulleger

Member
Aug 29, 2015
84
60
Hoja (threads) kubwa na zenye mvuto kuliko zote kwenye jukwaa la siasa hapa JF ni utendaji wa Magufuli. Lakini nadhani zinachosha sasa. Mheshimiwa hafanyi kazi mwenyewe. Kwa nini tusiangalie pia wanaofanya vizuri sana chini yake na tupime utendaji wao. Kwa mfano Waziri Mkuu, Lukuvi, Mwijage, na Ummy wanafanya vizuri sana. Tuwape moyo pia.
 
Attachments

  • 2X6A9713-1.jpg
    2X6A9713-1.jpg
    23.9 KB · Views: 56
Jamani Ummy anafanya nini? Ile kufagia muhimbili sehemu safi ndio ana fanya vizuri! Mwijage nae amekurupuka juzi kusema issue za sukari baada ya miezi 2.....alikuwa wapi hadi nchi inaenda kombo? Au jeshi la mtu mmoja?
 
Mjomba uko dunia gani! Mwijage na Ummy wanafanya vizuri? Wewe umenunuliwa wewe au utakuwa una undugu na hawa watu! Du yaani wewe sijui unatumia kipimo gani kuwatambua watendaji.
 
Hoja (threads) kubwa na zenye mvuto kuliko zote kwenye jukwaa la siasa hapa JF ni utendaji wa Magufuli. Lakini nadhani zinachosha sasa. Mheshimiwa hafanyi kazi mwenyewe. Kwa nini tusiangalie pia wanaofanya vizuri sana chini yake na tupime utendaji wao. Kwa mfano Waziri Mkuu, Luk Mwijage, na Ummy wanafanya vizuri sana. Tuwape moyo pia.

Magufuli anasifiwa kimkakati, kumbuka yeye ndio anateua wakuu wa mikoa, wilaya, wakuu wa taasisi mbalimbali nk. Huyo Majaliwa hana power hiyo.
 
Jamani Ummy anafanya nini? Ile kufagia muhimbili sehemu safi ndio ana fanya vizuri! Mwijage nae amekurupuka juzi kusema issue za sukari baada ya miezi 2.....alikuwa wapi hadi nchi inaenda kombo? Au jeshi la mtu mmoja?
Dili la sukari sasa linapigwa na Waziri wa Wizara ingine kabsa ambayo haiendani na hiyo Wizara Yaani Tanzania kuna vioja, January Makamba kaichangamkia fursa mapema wakija kushituka atakuwa tayari kapiga pesa nyingi kwenye vibali vya sukari.
 
Mjomba uko dunia gani! Mwijage na Ummy wanafanya vizuri? Wewe umenunuliwa wewe au utakuwa una undugu na hawa watu! Du yaani wewe sijui unatumia kipimo gani kuwatambua watendaji.

Wala sijanunuliwa nawaza kwa kutumia media. Nipe habari.
 
Unapotaja mawaziri wachapakazi Mwijage usimtaje maana sukaritu imemshinda kamuachia waziri mkuu na Raisi.
Huo utendaji wake hapo unakujaje jamani?
Watu chai hatunywi kwani sukari imeadimika na pombe hatuwezi kisha unamsifia mtu hapa.
Mleta mada hata Mwijage atakushangaa akiona maneno yako
 
Mwaijage kashindwa kazi mjanja January anapiga Dili la sukari kupitia Wizara yake pasipo kujua.
 
Hoja (threads) kubwa na zenye mvuto kuliko zote kwenye jukwaa la siasa hapa JF ni utendaji wa Magufuli. Lakini nadhani zinachosha sasa. Mheshimiwa hafanyi kazi mwenyewe. Kwa nini tusiangalie pia wanaofanya vizuri sana chini yake na tupime utendaji wao. Kwa mfano Waziri Mkuu, Lukuvi, Mwijage, na Ummy wanafanya vizuri sana. Tuwape moyo pia.
Umemsahau Nape!
 
JPM ndio CEO kwa hiyo taswira nzima ni yeye - The Manager, The Capitano. hao wengine aaaa
 
Mwijage na ummy sio mawaziri wachapa kazi hamna k2 pale bora useme lukuvi,prof mbalawa utaeleweka
 
Back
Top Bottom