Tumvumilie ndio aina yake ya uongozi

madala mujipa

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
1,417
860
Ndugu wana jf,
Tangu mwenyekiti wa chama alipochukua nchi na kuongoza alileta aina mpya ya utendaji wa fukuza fukuza kwa kuibatiza jina la tumbua jipu,watu walishangaa na kumjadili tukaona kama watu wameonewa kiasi cha kuwapa ushauri waende mahakamani.

Baadae amekabidhiwa chama na mzee jk ,yeye mwenyekiti alitahadharisha tangu mwanzo kuwa afadhali chama kibaki na watu wachache kuliko kukaa na wanafki na wasaliti ndani ya chama.

Sasa ameanza kazi yake amelala mbele na hao waliowaona ni wasaliti na wapinga mabadiliko ya chama.

Kubwa tusishangae sana kwakua alishatamka kumwambia jk kuwa ana moyo wa uvumilivu angekuwa yeye wala asingekubali watu waimbe tuna imani na fulani alafu akawawacha tu ndani ya chama.

Hili jambo tulichukulie la kawaida wala tusilione la ajabu sana, wahanga walijijua hawako salama na ndio maana wengine walitangaza kutogombea tena nafasi za uongozi katika hicho chama.

Waliofukuzwa kwa mahaba sasa ni wakati wao wa kuonyesha mahaba ya dhahiri shairi kuwa popote alipo na wao watamfuata kuliko kubaki katika unafki kama mwanzo.

Tumvumilie ndugu mwenyekiti ndio aina yake ya uongozi na waliobaki wajue watafukuzwa muda wowote kwa kuwa waliofukuzwa ni maswahiba zao!
 
Back
Top Bottom