Tumuunge mkono Mhe.Rais kwa kupigania rasilimali za nchi zisipotee lakini tuzuie wajinga wachache .

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Anaandika Malisa Godlisten
Tumuunge mkono Mhe.Rais kwa kupigania rasilimali za nchi zisipotee lakini tuzuie wajinga wachache wanaotaka kubeba jambo hili kisiasa. Nimemsikia Polepole akiwalaumu watanzania na viongozi wa dini eti wamekaa kimya wakati rasilimali za nchi zikiibiwa.

Ndugu Polepole hajawatendea haki watanzania wala viongozi wa dini, anapaswa awaombe radhi. Hivi waliotuingiza kwenye mikataba mibovu ni viongozi wa dini? Polepole anasahau kuwa mikataba yote ya hovyo inayoliangamiza taifa hili imepitishwa na serikali ya CCM na kuungwa mkono kwa kura nyingi za NDIYO kutoka kwa wabunge wa CCM?

Kimsingi Polepole hana "moral authority" ya kujadili suala hili maana CCM yake na wabunge wake ndio waliotuingiza kwenye matatizo yote haya. Kikubwa anachoweza kufanya Polepole ni kuomba radhi kwa niaba ya chama chake, kwa serikali yake kuliingiza taifa kwenye hasara kubwa. Na sio kuwalaumu viongozi wa dini.

Viongozi wa dini hawatungi sera, hawapitishi sheria, hawana nguvu ya dola. Sasa wanalaumiwa kwa lipi? Yani uache kulaumu wabunge wa CCM waliopitisha sheria mbovu za madini, uje kulaumu wachungaji, mapadri na masheikh? Upuuzi gani huu?

Serikali ya Rais Mkapa ndiyo iliyopitisha sheria inayoruhusu mchanga kusafirishwa nje ya nchi. Kwahiyo kama ni kuibiwa tumeibiwa tangu wakati wa Mkapa. Lakini Mkapa hakuwa TLP wala TADEA. Alikua CCM. Na wabunge wa CCM ndio waliopitosha sheria hiyo kwa wingi wao.

Leo watu walewale waliopitisha utaratibu huo kwa makofi ya shangwe, ndio haohao wanaompigia makofi aliyetengua utaratibu huo. Unafiki.!!

Wabunge wa upinzani walipokataa kupitisha sheria ya madini kwa dharura walifukuzwa bungeni. Walipohoji kwanini sheria nyeti inayolinda rasilimali zetu ipitishwe kwa dharura wabunge wa CCM walizomea.

Waziri Muhongo akasimama na kuwadhihaki wanasheria wa madini kuwa hawajui kiingereza. Spika akawafukuza wabunge wa upinzani, wale wa CCM wakabaki ndani na kupitisha sheria hiyo kwa kura ya NDIYO. Leo watu walewale, wa chama kilekile kilichotuingiza kwenye matatizo badala ya kuomba radhi, wanaibuka na kuwalaumu viongozi wa dini. Huu ni wendawazimu.!

Serikali ya CCM na wabunge wake wametuingiza kwenye matatizo makubwa sana kama taifa. Rais anapochukua hatua tunapaswa tumuunge mkono kwa umoja wetu kama taifa. Rais anafanya kazi ya nchi, sio kazi ya CCM. Kama mnataka afanye kazi ya CCM jengeeni matawi aje kuzindua.

Viongozi wengi wa upinzani walipohoji mambo haya waliitwa wachochezi. Leo Rais anafanya yaleyale ambayo wapinzani walihoji then viongozi wachache wa CCM wanataka kujivika ushujaa. Ujinga wa kiwango cha lami.

Na hili la madini ni moja tu kati ya mengi ambayo serikali ya CCM imetuingiza kwenye matatizo. Huko kwenye utalii, maliasili, uvuvi, uwekezaji etc kuna mengi mazito kuliko haya. Kwa mfano Loliondo kuna mwekezaji amepewa kibali cha uwindaji lakini amegeuza eneo hilo kuwa sehemu ya nchi yake. Ukiingia ktk himaya yake network ya simu ya mitandao ya ndani inapotea na inasoma United Arabs Emirates.

Mwarabu huyo anadaiwa kuwafukuza wakazi wa eneo hilo ambao ni wamasai na kuwachomea nyumba zao na kuchoma mifugo yao. Pia amejenga uwanja mkubwa ambapo ndege hutua moja kwa moja huko mbugani na kubeba wanyama kwenda uarabuni bila kukaguliwa na mamlaka yoyote ya ndani.

Jambo hili limepigiwa kelele na wapinzani kwa muda mrefu lakini wakaitwa wachochezi. Lakini siku Rais Magufuli akiamua kumfukuza huyu mwekezaji, viongozi wa CCM watakua mstari wa mbele kumpongeza Rais, wakati CCM hiyohiyo na wabunge wake wamemlinda Mwekezaji huyo kwa muda wote huu.

Tuache unafiki kwenye masuala ya kitaifa. Polepole aache kuwalaumu viongozi wa dini, instaed akilaumu chama chake na wabunge wake wa CCM kwa kupitisha mikataba ya hovyo inayoligharimu taifa. Rasilimali za nchi hii sio za CCM, sio za CHADEMA sio za ACT. Ni za watanzania wote. Yoyote anayezitetea tutamuunga mkono bila kujali tofauti zetu za itikadi za vyama.!

Malisa GJ
 
Sheria mbovu, za kijinga. Mikataba ya Kipuuzi, ya kinyonyaji iliyopitishwa na Baraza la Mawaziri ikashangiliwa na Wabunge wa CCM.
Wakati miswada ya kipuuzi ya madini ikipitishwa bungeni Mhe. Raisi alikuwa mbunge if m keeping my records well hakuwahi kusimama kupinga..
 
Naamini Rais ana nia njema sana na ana uchungu mkubwa na rasilimali za taifa. Hatua moja muhimu ni kurudi kwenye mchakato wa katiba. Tuanze alipoishia mzee Warioba. Mambo mengi ya hovyo yanatokana na mianya ya katiba tuliyo nayo. Tumwombe mkuu ashughulike na vyanzo sii matokeo.
 
Tunamuungaje? kwa kwenda pale alipo au? tupe mwongozo. Mi hata sijasoma hiyo report au kuelewa naanzaje sasa? haya wanafanya wana CCM wakati wakila rasilimali zetu, kama ambavyo tumeshauriwa tusiongee tunapokuwa na chakula mdomoni.
 
Naamini Rais ana nia njema sana na ana uchungu mkubwa na rasilimali za taifa. Hatua moja muhimu ni kurudi kwenye mchakato wa katiba. Tuanze alipoishia mzee Warioba. Mambo mengi ya hovyo yanatokana na mianya ya katiba tuliyo nayo. Tumwombe mkuu ashughulike na vyanzo sii matokeo.

Kama ana nia njema kwa nini alisimamisha mchakato wa katiba? Kwa nini hakujitoa katika baraza la mawaziri wakati hii mikataba ikipitishwa? Kwa nini hakutoka bungeni wakati miswada inaletwa na kupitishwa kuwa sheria?
 
Wakati unajadili ili usisahau kuna kitu kinaitwa HATI YA DHARULA(ghafla) na NDIOOOOOO MZEEE wakati wa kupitisha sheria hizi.
Jamani breakfast tayari uko?
 
Rais Magufuli hana muda wa kuongea na wezi wa Mali za nchi.

Maamuzi ya Rais Dr Magufuli yako sahihi kuisambaratisha net work ya wezi wa madini.

Vyombo vya dola fanyeni kazi kama sheria zinavyowataka kuwashughulikia wote walionufaika na wizi wa madini
 
Rais Magufuli hana muda wa kuongea na wezi wa Mali za nchi.

Maamuzi ya Rais Dr Magufuli yako sahihi kuisambaratisha net work ya wezi wa madini.

Vyombo vya dola fanyeni kazi kama sheria zinavyowataka kuwashughulikia wote walionufaika na wizi wa madini
Serikali ya Rais Mkapa ndiyo iliyopitisha sheria inayoruhusu mchanga kusafirishwa nje ya nchi. Kwahiyo kama ni kuibiwa tumeibiwa tangu wakati wa Mkapa. Lakini Mkapa hakuwa TLP wala TADEA. Alikua CCM. Na wabunge wa CCM ndio waliopitosha sheria hiyo kwa wingi wao.

Leo watu walewale waliopitisha utaratibu huo kwa makofi ya shangwe, ndio haohao wanaompigia makofi aliyetengua utaratibu huo. Unafiki.!!
 
Wajinga Wachache? CCM Nzima kwa mbwembwe akiwemo Magufuli ndio Walioiuza nchi kupitia Mikataba ile! Leo hii wanalia Machozi ya Mamba!
 
Katika hili nakubaliana na Malisa GJ, Pole pole anazeeka vibaya, viongozi wa dini wanaingiaje kwenye lawama hii?
Vingozi wetu wa dini mala zote wakiingilia
mambo ya kitaifa utasikia huyu huyu pole pole anawaonya wasiingilie mambo ya kisiasa.

Pole pole apuuzwe hana hoja viatu alivyovalishwa vinapwaya. Kabla ya kusema fikiri kwanza.
 
Mkuu marcus rojo
Pole pole akili zake ziko matakoni kama gigy money
 
Back
Top Bottom