Tumuombee Mwenzetu

Status
Not open for further replies.

Mwawado

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
993
250
"NDUGU WANA JAMBO KUNA MDAU MWENZETU HUMU NI MGONJWA MAHUTUTI.HABARI NILIZOZIPATA HIVI PUNDE NI KWAMBA MWENZETU HUYO YUPO HOSPITALI HUKO HOUSTON TEXAS,ANAENDESHA MAISHA YAKE KWA MSAADA WA MASHINE,NA KWA MUJIBU WA MADAKTARI NI KWAMBA PENGINE IJUMAA WATAONDOA HUDUMA HIYO .WOTE KWA PAMOJA TUJIUNGE NA FAMILIA YAKE KWA KUMTAKIA NAFUU NA MWELEKEO WA KUPONA KWA HARAKA".
 
Ingawa haujamtaja, tunamwombea kila la heri, kuondoa life support inamaanisha kuwa hali yake ni mbaya kiasi kwamba recovery is almost impossible
 
"NDUGU WANA JAMBO KUNA MDAU MWENZETU HUMU NI MGONJWA MAHUTUTI.HABARI NILIZOZIPATA HIVI PUNDE NI KWAMBA MWENZETU HUYO YUPO HOSPITALI HUKO HOUSTON TEXAS,ANAENDESHA MAISHA YAKE KWA MSAADA WA MASHINE,NA KWA MUJIBU WA MADAKTARI NI KWAMBA PENGINE IJUMAA WATAONDOA HUDUMA HIYO .WOTE KWA PAMOJA TUJIUNGE NA FAMILIA YAKE KWA KUMTAKIA NAFUU NA MWELEKEO WA KUPONA KWA HARAKA".

Ni vema atajwe kwa jina la hapa Ukumbini.
 
"NDUGU WANA JAMBO KUNA MDAU MWENZETU HUMU NI MGONJWA MAHUTUTI.HABARI NILIZOZIPATA HIVI PUNDE NI KWAMBA MWENZETU HUYO YUPO HOSPITALI HUKO HOUSTON TEXAS,ANAENDESHA MAISHA YAKE KWA MSAADA WA MASHINE,NA KWA MUJIBU WA MADAKTARI NI KWAMBA PENGINE IJUMAA WATAONDOA HUDUMA HIYO .WOTE KWA PAMOJA TUJIUNGE NA FAMILIA YAKE KWA KUMTAKIA NAFUU NA MWELEKEO WA KUPONA KWA HARAKA".

Mwawado, ni nani huyo ambaye hana Jina? Tunashindwa kumuombea huyo 'anonymous'.
 
Tunamwombea yeye na ndugu zake. Mungu atawapa nguvu za kukabiliana na yote yajayo.Nadhani asitajwe jina maana itakuwa rahisi kuunganisha na kujua ni nani mhusika. Tusimwondolee siri yake bila ridhaa yake.
 
Jamaa zake wa karibu wameshauri litajwe jina lake halisi.Mdau anaitwa Felix Makene
 
Nami pia naungana na wana JF kumuombea apate nafuu na kupona kabisa. Ila next time muwe mnataja basi jina la mlengwa sio lazima liwe halisi ila la kwenye Forum.
 
Mungu aamjaalie heri kadri ya mapenzi yake.
Nafikiri si vibaya kama tukaambiwa ni nani huyu mwenzetu!
Na tumaini pia tutakuwa tunafahamishwa maendeleo ya afya yake.
 
Hizo pole mnazotoa na dua mnazofanya ni kwa ajili ya nani hasa? Mwawado hebu sema ili dua iwe specific; kuna ndugu mmoja laiwahi kusema Mwenzetu Ibrah kalazwa Mirembe Hopsital tumwombee na watu bila shaka waliniombea. Ni vizuri utuambie anaweza kuwa ndugu wa watu hapa na nduguze wasijue. Tuambie kwa Jina analotumia hapa JF
 
Waungwana kwa wale waliotaka kujua Huyu Mdau,nimeshauriwa na watu wake wa karibu kutaja jina lake kamili,na kuwacha kumtambulisha kwa jina lake la humu,kwa sababu kuna jamaa hapa wamekwishakwenda kumuona Hospitali na haitokuwa vyema kumjua kwa jina lake la hapa . Jamaa anaitwa Felix Chambi (Makene).

Bado hali yake si nzuri na tutaendelea kutaarifiana Maendeleo ya hali yake,Naomba tuwiane radhi kama Tangazo limemkwaza mtu!!!
 
Tunakuombea sana ndugu yetu Felix, Mungu akujalie afya, neema na nguvu mpya ya kukabiliana na maradhi na maumivu ulonayo. Neema zake ziwe pia pamoja na familia yako. Upone haraka ili rejee ukumbini kumkoma nyani giledi. Amin.
 
Tunamuombea ndugu yetu Makene apate nafuu na kurudi katika hali yake.... Pia twawaombea duaa nduguze na waganga wanaomhudumia......
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom