Tumuombe Mungu kwa ajili ya viongozi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumuombe Mungu kwa ajili ya viongozi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Realist, Mar 9, 2010.

 1. R

  Realist Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Dec 11, 2006
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  OMBI MAALUM:

  Nimeamua kuliweka hapa hili ombi kwa sababu kuu mbili; Yakwanza ikiwa hapa ndipo wana-JF wengi zaidi wanafika ukifananisha na majukwaa mengi na sababu ya pili ikiwa ombi langu linawahusu viongozi wa kisiasa hivyo kama mod ataona halistahili basi anaweza kulipeleka anakoona yeye kunafaa.

  Ninawaomba wana-JF wote tuwaombee kwa Mungu viongozi wetu wakuu wa nchi hii, hapa ninamaanisha Rais aliyepo madarakani sasa hivi Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi na zaidi sana tumuombee Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa.

  Unaweza ukajiuliza tuwaombee juu ya nini, tumuombe Mungu awalinde hawa viongozi wetu. Sisi kama wanadamu tunajitahidi kuwapa ulinzi wa kibinadamu lakini ulinzi wa kweli unatoka kwa
  Mungu. Hivyo basi tumuombe sana Mungu awalinde. Ulinzi huu tunaomuomba Mungu uwe zaidi kwenye hii mishafara yao ya barabarani. Uwe ulinzi juu ya ajali za barabarani.

  Hawa ni viongozi wetu wa kitaifa ndio wakuu wa mamlaka ya taifa hili kwa vipindi tofauti hivyo kama ni mpango wa Mungu basi tumuombe mapenzi yake yatimizwe lakini kama ni mpango wa adui shetani basi ushindwe katika Jina la Yesu.

  Najua kila mtu anaushabiki na ufuasi wa vyama tofauti lakini kwa hili naomba wote tujinyenyekeze kwa Mungu juu ya hawa viongozi wetu wa kitaifa. Na kwa wale wanaoweza kuwafikishia taarifa hii basi nao wafanye hivyo ili na wao binafsi waweze kumuomba Mungu awalinde. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU UTULINDE WATANZANIA!
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajua Mungu huwa anaacha watu wabaya wawepo ili muendelee kumkubuka. Ukiangalia utaona Mungu aliacha Kennedy auawe, kwa kuwa watu waliona baada ya Kennedy kuingia madarakani alifaa sana, lakini baada ya Bush muuaji kuingia madarakani alimuacha aendelee kutawala kwa mvipindi vyote ili tuendelee kumkumbuka mungu.

  Same kwa Lumumba wa Zaire, Lumumba alikufa mapema sana lakini Mobutu aklikaa kweli. So, hata sisi hapa Tanzania tunaweza kuwa huko huko, tumepewa mzigo huu ili tumkumbuke mungu wetu. Kuwaombea vioingozi wa sasa itakuwa ni vigumu sana, sababu zote unazijua. Inawezekana kunawengine wanaweza kuwaombea.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mimi binafsi siwaombei mabaya. Ila siwaombei mema vilevile..
   
 4. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hizi ni fikra za kitwana, kwanini tusiwaombee wananchi wote walio kwenye hatari zaidi ya kupata ajali kuliko hao?kwangu mie hakuna mtu bora zaidi kuliko mwingine.
   
 5. D

  Donrich Senior Member

  #5
  Mar 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni bora zaidi kuliombea taifa letu kuwa na amani,Mungu anawajua vizuri hawa viongozi kuliko tunawavyowajua sisi.
   
 6. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ndugu Hili ndo linatupotosha Amani Tanzania itaondoshwa na sisi kuchagua kuwaacha madarakani watu wanaojipenda wenyewe, wakiwaacha masikini wanateseka. Hebu fikiria Wamasai walivyopoteza ngombe wao huku viongozi wakiuza ardhi kwa wageni
  Cheki GAVANA wa Benki kuu alivyokataa kukaa kwenye nyumba isiyo na swimming pool, huku wapiga kura wa waziri wa fedha nyumba zao zikiangushwa na maji yanayotiririka.
  BAADA YA MDA WATU WATACHOKA NA AMANI ITATOWEKA.
  Hivo tujiombee wenyewe, na hao viongozi wenye akili lakini wanajifanya mazuzu hawajui hali yetu.
   
 7. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #7
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kwalipi walilofanya lamaana mpaka tuwaombee huu utakuwa ni umbeya na ukache wako wa kupima wana jf imani kuwa wanwakubal;i kwa kiasi gani eee mungu baba walaani viongozi hawa kila waendapo ndege zilipuke tuwasahau kabisa kwani hapa tulipo ndy wamesababisha maisha mabovu kwa mtanzania, tena next uje na hoja siyo mada ambazo hazina kichwa wala miguuu
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  Tujiombee sisi tunaoishi maisha magumu sababu ya uongozi mbovu wa viongozi hawa.
  Angalia bei za bidha mbalimbali zilivyo juu sasa hivi, then eti tuwaombee?!
  Labda tuwaombee watubu dhambi zao za kukimbilia ikulu ilhali hawana uwezo wowote wa kutuongoza.
  Na tuwaombee, hasa huyu Raisi wa sasa, apewe moyo wa kutokugombea tena uraisi mwaka huu kwani kazi hiyo haiwezi kabisa!
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Abdul wewe ni mtata...hahaaaa
   
 10. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh, mi sijaelewa una mantiki gani ya kututaka tuwaombee wakingiwe ajali.

  Kwa nini sasa na kwa nini ajali?
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  kaka kwa hawa viongozi wetu unaweza hata kufunga siku 40 kifungo bila kula kama kubadilisha wangeshabadilika lakini hata dalili tu hakuna - cha msingi waondoke tu waje wengine - kama kuwaombe tunawaombea kila siku - madhehebu mengine hata kwenye Litungia ipo sehemu special kuombea viongozi wakuu wa serikali na Rais.

  Cha msingi tujiombee sisi wenyewe watanzania ili tusiwachangue hawa mafisadi come October 2010 - hilo ndiyo la kuongelea kwa wakati huu mkuu.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Unanionea bana.
  Ni philosophy tu sio utata.
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Kwa nini ulinzi huo uwe wa ajali za barabarani tuu? hili linahitaji kumwona Shk Yahaya.
   
 14. bht

  bht JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  nimekusoma bana.....I just laughed vile ulivoiweka....ndani haupo nje haupo......
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mimi nawaombee wagombane sana, wengine wajitoa kwenye chama, mikakati yao isambaratike, na CCM yao iishie.
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Tanzania kuna viongozi wabaya na hakuna maendeleo kwa sababu watu wengi wanaamini mungu.

  Ndiyo maana unakuta badala ya watu kuweka mikakati ya kuondoa viongozi wabaya, na kuongeza accountability, wanaongea habari za kuwaombea.

  Kuamini mungu (asiyekuwepo by the way) na kumuomba ni kuwa complacent, ni kuruhusu status quo, ni kuacha mungu (asiyekuwepo) akufanyie kazi unayotakiwa kuifanya mwenyewe.

  Ukiangalia historia ya dini na mungu utaona inaenda moja kwa moja na watawala kutumia saikolojia kuwatawala wanyonge.Kuanzia Wababeli mpaka kina Farao, Wafalme wa Kigiriki kina Alexander The Great, Kirumi kina Constantine na mapapa wao, wa Kiingereza kina Henry VIII, mpaka watawala wa Kimarekni kina George W. Bush.

  Kwa hiyo, kumuomba mungu kwa ajili ya viongozi wetu ni idea ridiculous.Unless you are one of them and aim to preserve the status quo.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  tumuombe Mungu awaondolee Baraka.. maana kwa miaka mingi tumekuwa tukiwaombea awabariki matokeo yake ndiyo hayo.. wamebarikiwa!
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji turudi nyma kidogo. Tuwaulize wale viongozi wetu wa dini waliotuambia mwaka 2005 kuwa kuna wagombea ambao ni "chaguo la Mungu" na wananchi wakawachagua kuwa viongozi, jee Mungu tukimwomba awaondolee baraka atakubali kufanya hivyo kwa chaguo lake? Au sasa watufafanulie vizuri maana inawezekana 2005 hatukuwaelewa, walikuwa wanamaanisha Mungu yupi ambaye aliwaagiza watutangazie hivyo?
   
 19. B

  BENE Member

  #19
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ya Tanzania yamekaa kiroho zaidi. Kwa hiyo mwenzetu analitazama swala la Tanzania kutoka kwenye mambo ya Kiroho, kwani hali ya mtu unayoiona katika uhalisia inatoka kwenye ulimwengu wa Roho. lazima uingie kwenye shule ya Roho Mtakatifu ndiyo uelewe haya mambo. Kama hujaenda shule ya Roho Mtakatifu huwezi kuelewa haya mambo.
  Swala la muhimu ni kuomba toba kwa Mungu ili asamehe yale tulliyomkosea kama vile kuabudu sanamu, (kila mkoa una sanamu lake kwenye keep left, mtu wa kawaida utaona ni kawaida kabisa ila tafuta kwanza chimbuko lake), kupitisha watoto kwenye moto (tunatembeza mwenge kila mwaka na tunachangia gharama kila mmoja). Haya tunayaona ya kawaida ila ni machukizo mbele za Mungu be careful ni mpaka uende shule ya Roho Mtakatifu. Kuna haja ya kliombea taifa seriously kila mtu kwa nafasi yake.
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  tafadhali tunaomba somo la chapchap juu ya mwenge na hizo sanamu basi...ambao hawatasikia na kuelewa...itakuwa kivyao...
   
Loading...