Tumuombe Magufuli aende Congo kwa faida ya Tanzania na Congo

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,704
2,000
Washauri wa serikali ni lazima tujue hatuwezi kujifungia tu ndani ya Tanzania wakati majirani zetu wana mali ambazo zinachukuliwa na China, US na nchi za EU.

Mimi nafikiri Magufuli anatakiwa kusafiri kwenye Congo ili kuweka urafiki na kusaidia kwenye sehemu hizi kwa manufaa ya taifa.

 • Reli tutafute strategic investment kwenye reli yetu ya umeme ili Congo waweze kuitumia
 • Soko la Madini. Tufungue soko la madini Kigoma ili madini yaweze kuja Tanzania. Ombea kazi geologist wetu pale vilevile
 • Soko ya vyakula liwe kigoma hasa samaki wa ziwa Tanganyika na soko la vyakula. Ingine mikataba ya kuuza vyakula Congo. Lakini washauri watanzania waanzishe viwanda vya mazao kama Azam pale kigoma waweze kuuza vitu Congo

 • Yaani hawa China na wengine ndiyo pekee wanachukua madini pale wakati sisi tumekaa hapa tu na jeshi leo linashughulikia korosho.

  Tungepeleka jeshi jeshi kama patner pale na kuhakikisha hakuna wizi na sisi tunaweka soko pamoja na Congo na tunakuwa partners.

  Sisi tumekuwa watu wa kuchukuwa wakimbizi tu hawa wengine wanawaletea silaha waendelee kupigana wakati wanachukua Gold na mengine mengi.

  Tanzania tusijivutevute uwezo tunao, urafiki tunao, nia tunayo sasa tunasubiri nini wakati Congo inaliwa mbele yetu hivi?. Ni kwanini hatupati hata mbao za bei rahisi kutoka kwenye ile misitu ya Congo?
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,638
2,000
Bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Tunatumia muda na nguvu kubwa kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe! Nia ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa dhidi ya majirani zetu na dunia kwa ujumla, haijulikani kabisa kama ipo kweli mioyoni mwa viongozi wetu.
 
H sanny

JF-Expert Member
May 25, 2018
224
250
Nitarifika hili swala kwa uongozi wa juu, najivunia kuwa vijana kama nyie
 
Goldman

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
1,823
2,000
Wazo la maana sana naunga mkono hoja asilimia mia, drc congo ni bora mara kumi kwetu kuliko kuikumbatia ka rwanda!
 
K A B U R U

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
646
1,000
Mawazo mazuri sana, nilishangaa Tshisekedi alivyoanza ziara zake kwa kuelekea Kenya, nikasema kuna kitu tumekosea.
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,530
2,000
Washauri wa serikali ni lazima tujue hatuwezi kujifungia tu ndani ya Tanzania wakati majirani zetu wana mali ambazo zinachukuliwa na China, US na nchi za EU.

Mimi nafikiri Magufuli anatakiwa kusafiri kwenye Congo ili kuweka urafiki na kusaidia kwenye sehemu hizi kwa manufaa ya taifa.

 • Reli tutafute strategic investment kwenye reli yetu ya umeme ili Congo waweze kuitumia
 • Soko la Madini. Tufungue soko la madini Kigoma ili madini yaweze kuja Tanzania. Ombea kazi geologist wetu pale vilevile
 • Soko ya vyakula liwe kigoma hasa samaki wa ziwa Tanganyika na soko la vyakula. Ingine mikataba ya kuuza vyakula Congo. Lakini washauri watanzania waanzishe viwanda vya mazao kama Azam pale kigoma waweze kuuza vitu Congo

 • Yaani hawa China na wengine ndiyo pekee wanachukua madini pale wakati sisi tumekaa hapa tu na jeshi leo linashughulikia korosho.

  Tungepeleka jeshi jeshi kama patner pale na kuhakikisha hakuna wizi na sisi tunaweka soko pamoja na Congo na tunakuwa partners.

  Sisi tumekuwa watu wa kuchukuwa wakimbizi tu hawa wengine wanawaletea silaha waendelee kupigana wakati wanachukua Gold na mengine mengi.

  Tanzania tusijivutevute uwezo tunao, urafiki tunao, nia tunayo sasa tunasubiri nini wakati Congo inaliwa mbele yetu hivi?. Ni kwanini hatupati hata mbao za bei rahisi kutoka kwenye ile misitu ya Congo?
Huwezi amini miji kama Lubumbashi wanakula kuku broiler wanaotoka USA kuna fursa nyingi sana DRC maana wa congo hawalimi
 
mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
4,724
2,000
Bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Tunatumia muda na nguvu kubwa kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe! Nia ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa dhidi ya majirani zetu na dunia kwa ujumla, haijulikani kabisa kama ipo kweli mioyoni mwa viongozi wetu.

Na cha kushangaza tulikuwa na wana diplomasia fake as in Kikwete na membe lakini nao walishindwa kabisa kutumia ujuzi ama uzoefu wao kuifanya nchi yetu ipige hatua lakini wapi. Walikuwa bize tu kupishana angani kwenda kununua tie na suit China na miswaki Dubai.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
7,197
2,000
Mimi nafikiri Magufuli anatakiwa kusafiri kwenye Congo ili kuweka urafiki na kusaidia kwenye sehemu hizi kwa manufaa ya taifa.
Ngoja nielezee hili kwa kuamusha kumbukumbu kama msomaji anayo.

Wakati Tshisekedi anaapishwa uliona ujumbe uliowakilisha toka Kenya. Na baada ya hapo, huyo jamaa mpya amekwenda mara ngapi Nairobi? Na juzi tu Jaluo anayejifanya mkuu wa 'Miundombinu ya Afrika' alikuwa huko, eti kuhusiana na daraja linalounganisha Kinshasa na Braza.

Hawa jamaa sasa wanapigana kufa kupona wauze ujenzi wa reli yao ifike Kisumu, lengo kuu likiwa ni kuifikia DRC.

Kuna wakati walitumia sababu ya kuifikia Zambia kama faida itakayopatikana kwa kujenga reli hiyo. Sisi kufika Rwanda ndilo lilikuwa lengo letu kuu, tumemaliza!

Tunaendeleza tabia yetu ile ile ya kujitoa mhanga kwa kumwaga damu zetu; lakini inapofika wakati wa kunufaika, wanaonufaika ni wengine. Sijui sisi tunajiona kuwa watu wa namna gani?

Niliyosikia mapya, ni kwa yeyote atakayetaka kupigana, sisi tupo tayari kuwauzia chakula! Ukisema kujenga miundombinu ukiwa na lengo la kulifikia soko hilo, akili yetu haiko kabisa huko.

Hawa waChina na hiyo Belt na Road yao na ujenzi huu unaofanyika kandokando ya Bahari ya Hindi, kwa nini tusiuchukulie kama mkakati, fursa kwetu pia?
Chukulia mfano haya mataifa yaliyoko magharibi mwa Afrika, toka Nigeria/Ghana hadi Namibia. Kusafirisha mizigo yao toka Mashariki ya Mbali na China yenyewe ni lazima wazunguke njia ndefu kupitia Kusini. Reli/Barabara zitakazounganisha Magharibi ya Afrika na Mashariki, mizigo hiyo ikapakiwa melini Bagamoyo na kusafirishwa, itakuwa ni ya haraka na manufaa zaidi. Pamoja na kwamba hili ni la mipango ya mda mrefu, lakini mipango hiyo utekelezaji wake ndio haya tunayoyaona sasa ya Belt and Road Initiative (BRI).

Sisi haya yatapita pembeni tukiwa tunawadhibiti 'wasaliti'.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
34,649
2,000
Washauri wa serikali ni lazima tujue hatuwezi kujifungia tu ndani ya Tanzania wakati majirani zetu wana mali ambazo zinachukuliwa na China, US na nchi za EU.

Mimi nafikiri Magufuli anatakiwa kusafiri kwenye Congo ili kuweka urafiki na kusaidia kwenye sehemu hizi kwa manufaa ya taifa.

 • Reli tutafute strategic investment kwenye reli yetu ya umeme ili Congo waweze kuitumia
 • Soko la Madini. Tufungue soko la madini Kigoma ili madini yaweze kuja Tanzania. Ombea kazi geologist wetu pale vilevile
 • Soko ya vyakula liwe kigoma hasa samaki wa ziwa Tanganyika na soko la vyakula. Ingine mikataba ya kuuza vyakula Congo. Lakini washauri watanzania waanzishe viwanda vya mazao kama Azam pale kigoma waweze kuuza vitu Congo

 • Yaani hawa China na wengine ndiyo pekee wanachukua madini pale wakati sisi tumekaa hapa tu na jeshi leo linashughulikia korosho.

  Tungepeleka jeshi jeshi kama patner pale na kuhakikisha hakuna wizi na sisi tunaweka soko pamoja na Congo na tunakuwa partners.

  Sisi tumekuwa watu wa kuchukuwa wakimbizi tu hawa wengine wanawaletea silaha waendelee kupigana wakati wanachukua Gold na mengine mengi.

  Tanzania tusijivutevute uwezo tunao, urafiki tunao, nia tunayo sasa tunasubiri nini wakati Congo inaliwa mbele yetu hivi?. Ni kwanini hatupati hata mbao za bei rahisi kutoka kwenye ile misitu ya Congo?

Sisi akili yetu ni kuuzia wamachinga vitambulisho huku tukisema vitambulisho ni bure!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom