Tumuhamishe Wizara Dkt. Ndugulile kwa sababu hakuna innovation yoyote anayoifanya

Kazi ya waziri sio kufungua keyboard, CPU, monitor au kuchambua mifumo ndio aonekane kuiweza wizara husika...Waziri ni kiongozi wa ki-sera Zaidi ambaye anakuwa na wataalamu chini yake kuanzia wakurugenzi,mameneja, maafisa na kadhalika ambao ndio wanafanya utendaji...Tusichanganye mambo
 
Na Thadei Ole Mushi

Serikali inaandaa sheria maalumu ya mtu kuwa na laini moja ya simu kutoka kampuni moja ikiwa ni njia ya kulinda faraga za watu inayolenga kudhibiti wahalifu mtandaoni.

Bado naona Kuna tatizo kwa Wizara yetu ya Technolojia ambayo ni Wizara Mpya kabisa.

Tatizo kubwa hawa wajamaa wamejikita kwenye kudhibiti badala ya kuwekeza kwenye uvumbuzi. Dunia kiteknolojia inakimbia Sana sisi bado tunahangaika na wanaomiliki line mbili za Simu.

Twende sawa hapa

Tuna tatizo mahali na tatizo hili linanzia kichwani kwa Mh Ndugulile. Kwa sasa laini zote za Simu zimesajiliwa kwa Kutumia alama za vidole (Biometric) kwa maana hiyo Mimi Ole Mushi hata nikiwa na Line mia Moja za Simu as long as nimezisajili kwa Kutumia fingerprint na kitambulisho changu nikifanya uhalifu popote ni rahisi kunikamata.

Au tuseme lile zoezi lilikuwa ni danganya toto? Kwamba pamoja na kusajili kwa alama za vidole bado hatujui ni kina nani wanaomiliki hizo line?.

Hivi wizi wa Mitandao anaujua Ndugulile?

Hawa wanaotuma sms kuwa nitumie hela kiasi Fulani au wanakupigia simu sio wezi wa Mitandao hawa ni vibaka wadogo Sana .

Wizi wa Mitandao kwa mfano hapa Tanzania tunafanya Transaction nyingi Sana online fikiria kuhusu kununua Luku, Kutuma Pesa kwenye Mitandao ya Simu nk. Ukisikia wizi wa Mtandao ni Mtu anazuia mifumo hiyo isifanye Kazi mfano Mtu anaweza kuhack mfumo wa Kutuma Fedha Tigo. Anazuia hakuna Fedha kwenda Wala kutoa. Halafu wanawapigia Tigo kuwa tupe bilioni kadhaa tuachie mfumo wako ufanye Kazi.

Ni kama walivyokuwa wasomali wanateka Meli wanakuambia tutumie Fedha tuachie Meli yako na huna Cha kuwafanya.

Sijui Mifumo yetu ya Transaction ipo secured kiasi Gani au tunazo server au tunategemea server za nje ya nchi lakini watu Duniani wanapigwa Sana kwenye uharamia huu.

Ninaposema ipo secured kiasi Gani ni kama unamtuma Mtu apeleke hela anaondoka Nazo Kinondoni anapeleka Tegeta hapo njiani Kuna maharamia wengi Sana je tunazilindaje zifikie? Ni vivyo hivyo online tunapofanya Transaction Kuna watu wanaweza ku generate code na wakazizuia au kuchukua na hutawajua.

Mh Ndugulile yeye anawaza line za Simu tu wakati Dunia ilishahama huko. Na akumbuke watu kumiliki lain zaidi ya Moja sio kwa kupenda ni kujaribu kutafuta unafuu wa maisha.

Naona Umuhimu wa Ndugulile kurudi kwenye masuala ya Afya akatusaidie kunyoosha mifupa iliyovunjika kuliko huku Aliko.

Hakuna innovation yoyote anayoifanya hapa.

Ole Mushi
0712702602

View attachment 1813157
Hii wizara ifutwe. Haina faida
 
Hiyo wizara angepewa Prof. Simon Msanjila (katibu mkuu-madini) au hata Godwin Gondwe! Suala la technolojia ni pana sana , pia Very Dynamic, Huwezi kumkabidhi mtu ambaye hana ufahamu wa kutosha katika eneo hilo! Vinginevyo ataishia kuhimiza uwajibikaji na makusayo ya mapato!
 
Huwez kuweka waziri, naibu waziri na katibu wa wizara ambao sio wataalam wa ICt wakaanzishe wizara ya ICT, hapa hakuna miujiza ni madudu tu ndo yatakayotokea huko.
Madaktari mbingwa wa binadamu ndiyo wamewekwa wote hapo unategemea nini?
 
Back
Top Bottom