Tumuenzi Ruge Mutahaba kwa kuyaishi mambo yote aliyoyaamini na kuhimiza

Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
348
500
Kama kuna zawadi Mwenyezi Mungu alituzawadia Vijana wa Tanzania basi ni zawadi ya maisha ya Ruge Mutahaba, ambaye mara zote alisimama katika uzalendo na upendo wa kweli wa nchi yake na vijana wenzake.

Waswahili wanasema ishi ukashifiwe na kufa usifiwe. Kwa kawaida utasikia sifa nyingi za mtu baada ya kutangulia mbele za haki. Hii maana yake wakati wa uhai hatutilii maanani mambo mazuri yanayofanywa na watu. Kama kuna zawadi Mwenyezi Mungu alituzawadia Vijana wa Tanzania basi ni zawadi ya maisha ya Ruge Mutahaba, ambaye mara zote alisimama katika uzalendo na upendo wa kweli wa nchi yake na vijana wenzake.Kila mtu ana mtazamo wake lakini naona ameleta mabadiliko makubwa ya kifikra miongoni mwa vijana na alileta mapinduzi makubwa kwenye sanaa ya Tanzania na kuwainua vijana wengi sana katika tasnia ya muziki wa Bongo Flavour. Tunamkumbuka Ruge kama kijana ambaye Mwenyezi Mungu alimjaalia vipawa vingi lakini kubwa kuliko yote ni akili ya asili ambayo aliitumia vyema kuleta mabadiliko na maendeleo katika nyanja mbalimbali.
pic+ruge.jpg

Ruge alitamani kuona kizazi hiki hasa vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na changamoto na kuzitatua badala ya kuwa sehemu ya walalamikaji.Alikuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano katika jambo lolote ambalo anajua litaleta matokeo chanya kwa jamii. Mawazo na ushauri wa Ruge daima utaendelea kudumu miongoni mwetu hasa vijana wa Taifa hili wenye kupenda kuiona Tanzania inapiga hatua kimaendeleo.
Mawazo na fikra za Ruge hayatafutika kirahisi kwa kuwa amekuwa msaada wa kweli na amebadilisha maisha ya wengi kupitia maono yake na mipango yake.Muhimu ni kuyaishi yale yote mema aliyoyahimiza kwa maneno na vitendo ili kutimiza ndoto zake kwa vijana wa Taifa hili.
Kujiamini, kujituma, ujasiriamali, ushiriki wa ujenzi wa Taifa ni miongoni mwa mambo aliyoyaamini. Tumuenzi kwa kuyaishi.

Source: Inatosha kumuenzi Ruge Mutahaba kwa kuyaishi mambo yote
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000

View attachment 1036501

Ni kweli, ili kumuenzi kiukweli na siyo "kisanii" inabidi tuyatekeleze yote yale mazuri aliyokuwa akiyaamini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom