Tumuenzi Rais Magufuli kwa kubana matumizi yasiyo ya lazima

Umasikini na ufinyu wa fikra unawafanya mataga wengi waone kujengewa miundombinu na serikali ni kama fadhila kwao yani kitu ambacho hawakustahili..kwa kifupi wanasiasa huomba kura ili wayafanye hayo so niwajibu wao kutekeleza maana fedha zinatoka kwa wananchi sio mifukoni mwao..ebu ficha ujinga wako.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ambao hawakujenga barabara na wamekula hizo hela zenu za kodi mmewafanya nini? Na yeye kama asingejenga bwawa la umeme mngemfanya nini? Wacha ujinga na chuki. Mzee nyerere rip alitumia kodi zetu kukombolea bara la Afrika mmemfanya nini? Wakati wa mzee JK kulikuwa na Richmond, Escrow mlimfanya nini?
 
Kauli zake za kubana matumizi nazikubali sana, Pesa nyingi ya Serekali hua inapotezwa kwa matumzi ya ovyo kabisa yasiyo na tija. Yani vitafunio katika hafla ya bunge tu zaweza tumika mamilioni, ni upuuzi na kutothmini pesa zetu ambazo zingetumika kwa masuala mengi ya kutusaidia mambo muhimu kama taifa.
Tatizo kiupande wake ni kuwa alikua akibana huku na kuzitumia kwengine, mambo ya kununua wapinzani na kuitisha uchaguzi mpya kila baada ya kununua wapinzani ziliondoa credibility yake yote katika hilo jambo.
 
Elimu bure/bila malipo
SGR
Bwawa la umeme
Barabara
Bandari upanuzi
Viwanja vya ndege
Ununuzi wa ndege cash cash
Ujenzi wa vituo vya afya/hospitali
Ununuzi wa rada na meli
Mikopo vyuoni
Hostel za wanafunzi
Nk
Hata ufanye mambo.mazuri kiasigani.
Lakin kitendo cha.kufikilia na kusubutu kuhalibu.kutoa roho ya binadam mwenzio kwasababu ya.kumziba mdomo bado huwezi kunishawishi kumuona mtu huyo ni.shujaa au ni mzuri.
Wanaomsifia ote kwasababu hili halijawatokea kwenye familia zao.
Sikuzote shujaa wa kweli hawezi kuogopa kusemwa.
Bahati mbaya au nzuri hakimu mkuu kabisa kaamua na hakuna wa kumpa rushwa ya aina yoyote ile.
Naamin furaha ya kweli iliyopotea kwa watanzania wasiokua wanafiki itarudi.
Na watanzania hawataogopa kusema.
 
1. SGR tiamaji tiamaji. Miaka mitano SGR iko Moro. Fedha hakuna hadi kakopa.
2. Rada ni mradi wa Kikwete, imefungwa awamu ya 5 baada ya terminal 3 kukamilika.
3. Labda barabara za mitaani. Hakuna mkoa aliojenga barabara ya kufika km 200. Kama ipo itaje.
4. Kajenga uwanja wa ndege mmoja tu, kwao Chato.
5. Ndege kanunua bila mipango ya kibiashara ndio manaa hasara kila siku. Ili kuficha hilo alikataza shirika la ndege lisikaguliwe na CAG. Katika kutapa tapa kibiashara akaona aue mashirika shindani japo haijasaidia.
6. Ujenzi wa vituo vya afya/hospitali- hii ni kweli.
7. Mikopo vyuoni ilikuwepo tangu enzi, tena ndio kaharibu kuliko alivyokuta. Zaidi kawanyima mikopo watoto waliosoma private.
8. Hostel za wanafunzi- hadhi ya urais si ya kujenga hostel mbili za milioni 500 kila mmoja. Rais wa nchi anasifiwa kwa hostel mbili?

Zaidi kaeneza chuki za kisiasa, ukanda, ukabila na kujenga matabaka. Mambo ambayo yalimgharimu sana Mwl kuyamaliza. Alikuwa anatupeleka kwenye mgawanyiko kama uliopo Kenya au Uganda
Nakwambia hivi...!!
Watanzania ni wapole sana.

Kwa bahatinzuri mwenyezi mungu hajawahi kuwaacha watanzania hawa wapole wasiokua na hatia ya kunyanyaswa hadi kufikia kila wanapokanyaga wanatetemeka kwa hofu ya mtu m1 na kundi lake la watu wachache wanaothubutu kufanya wanavyotaka bila ya hofu ya mungu wakati huo wanamtaja kila wakati kwa unafiki.
Kiukweli mwenyez mungu wa watanzania acha awapumnzishe kwa amani na kwa kasi.
Anayo majina yao mkononi na anazidi kuyakata.

Hakuna kitu.kilichoniuma kama tetemeko linapiga kule watu wanajitolea kutoa misaada ,misaada imetolewa zaid ya bilioni20.
Matokeo yake walengwa hawajapewa wameambulia masimango na kuambiwa wanajali sana katelelo na ndio maana tetemeko nalo limetetemeka.na wao watetemeke wajenge wenye.

Mambo kama haya labda kama hakuna mungu.

Mungu hadhihakiwi.
Lazima akutangulize pamoja ote tunaenda.
 
Umasikini na ufinyu wa fikra unawafanya mataga wengi waone kujengewa miundombinu na serikali ni kama fadhila kwao yani kitu ambacho hawakustahili..kwa kifupi wanasiasa huomba kura ili wayafanye hayo so niwajibu wao kutekeleza maana fedha zinatoka kwa wananchi sio mifukoni mwao..ebu ficha ujinga wako.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wamejenga barabara toka Mwanza hadi Dar, kilometa zaidi ya 1000, mwingine kaja kujenga daraja pale Ubungo wanasema ooh! kafanya kazi kubwa kuliko yeyote! Mataga wana shida.
 
Hata ufanye mambo.mazuri kiasigani.
Lakin kitendo cha.kufikilia na kusubutu kuhalibu.kutoa roho ya binadam mwenzio kwasababu ya.kumziba mdomo bado huwezi kunishawishi kumuona mtu huyo ni.shujaa au ni mzuri.
Wanaomsifia ote kwasababu hili halijawatokea kwenye familia zao.
Sikuzote shujaa wa kweli hawezi kuogopa kusemwa.
Bahati mbaya au nzuri hakimu mkuu kabisa kaamua na hakuna wa kumpa rushwa ya aina yoyote ile.
Naamin furaha ya kweli iliyopotea kwa watanzania wasiokua wanafiki itarudi.
Na watanzania hawataogopa kusema.
Mtu anawafanya watu wazima wenzie mazezeta, kila sentensi wanamtaja majina yake manne.
 
Ule msururu wa Magari ya kifahari ukiutizama kwa haraka haraka ukiambiwa nchii hii Kuna watu Bado wanakufa kwa kukosa dawa hautaamini asilani
 
Rais Magufuli (RIP) hakupenda matumizi ya hovyo kabisa kwenye maisha yake ya uongozi. Hivyo, hata kwenye mazishi yake lazima tuzingatie matumizi ambayo yanaongeza gharama ambazo sio za lazima katika kupunsishwa kwake kwenye nyumba yake ya milele ili pesa hizo zielekezwe kwenye ujenzi wa miradi aliyoiasisi.

Rais Magufuli alichukia sana matumizi yasio na tija, na wakati mwingine aliachana na sherehe za uhuru na mwenge ili aokoe hela zikatumike kwwnye miradi mingine.

Watanzania tusijekuambiwa maziko yake yalitumia mabilioni ya fedha, atasikitika sana huko aliko.

Upigaji usijeukarudi kwa kuanzia na ugongwa na mazishi yake.
Huu ni mradi watu wanapiga pesa sn kwa sasa
 
Umasikini na ufinyu wa fikra unawafanya mataga wengi waone kujengewa miundombinu na serikali ni kama fadhila kwao yani kitu ambacho hawakustahili..kwa kifupi wanasiasa huomba kura ili wayafanye hayo so niwajibu wao kutekeleza maana fedha zinatoka kwa wananchi sio mifukoni mwao..ebu ficha ujinga wako.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuna katiba mbovu sn yaani tunaamini maendeleo ni hisani ya mtu
 
Rais Magufuli (RIP) hakupenda matumizi ya hovyo kabisa kwenye maisha yake ya uongozi. Hivyo, hata kwenye mazishi yake lazima tuzingatie matumizi ambayo yanaongeza gharama ambazo sio za lazima katika kupunsishwa kwake kwenye nyumba yake ya milele ili pesa hizo zielekezwe kwenye ujenzi wa miradi aliyoiasisi.

Rais Magufuli alichukia sana matumizi yasio na tija, na wakati mwingine aliachana na sherehe za uhuru na mwenge ili aokoe hela zikatumike kwwnye miradi mingine.

Watanzania tusijekuambiwa maziko yake yalitumia mabilioni ya fedha, atasikitika sana huko aliko.

Upigaji usijeukarudi kwa kuanzia na ugongwa na mazishi yake.
Ila kwa miradi ya hovyo ya Chato kama airport kubwa ya kisasa mahali pasipokuwa na watu wengi yalikuwa ni matumizi sahihi
 
Msafara wa Magufuli ulikua na Zmagsri 60, ni matumizi gani aliyoyabana? Tunamuenzi jinsi alivyoishi kasoro tu hakuna wa kugawa pesa barabarani sasa hivi.
Na helkopta kwa juu.

Anahamia miezi kufanyia kazi nyumbani kwao. Wakuu na mabosi wote wanamfuata huko. Wanapishana hotelini tu.
 
Hata ufanye mambo.mazuri kiasigani.
Lakin kitendo cha.kufikilia na kusubutu kuhalibu.kutoa roho ya binadam mwenzio kwasababu ya.kumziba mdomo bado huwezi kunishawishi kumuona mtu huyo ni.shujaa au ni mzuri.
Wanaomsifia ote kwasababu hili halijawatokea kwenye familia zao.
Sikuzote shujaa wa kweli hawezi kuogopa kusemwa.
Bahati mbaya au nzuri hakimu mkuu kabisa kaamua na hakuna wa kumpa rushwa ya aina yoyote ile.
Naamin furaha ya kweli iliyopotea kwa watanzania wasiokua wanafiki itarudi.
Na watanzania hawataogopa kusema.
Wewe mbona upo hujapotea? Waliopotea walifanya nini?

Kaka yangu hata Marekani na Ulaya watu wanapotea sana na kufungwa jela mpaka basi. Kila kitu kina mipaka yake.

Lakini lazima ujue kuwa vibaraka wa mabeberu wako wengi sana wanaoifanya Afrika yote isiwe na maendeleo kwa wakati mmoja. Watu hawa ni ngumu sana kuwafahamu kwakuwa wengi wamejificha kwenye mashirika ya kidini, taasisi za masaada na hisani .
 
Back
Top Bottom