Tumuenzi Dr.Ulimboka kwenye kumbukumbu ya kudumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumuenzi Dr.Ulimboka kwenye kumbukumbu ya kudumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lyimo, Jun 29, 2012.

 1. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Bila kujali muhusika katika unyama aliofanyiwa Dr.Ulimboka, napenda ibuniwe namna ya kumuenzi Dr.Ulimboka ili abakie kwenye Historia ya upiganiaji wa Mazingira bora ya Afya kwa watanzania. Sina pendekezo la vipi tumuenzi, ila kupitia Jumuiya/Vyama vya Madaktari nchini, Chama cha wafanyakazi, watetezi wa haki za binadamu, watanzania wazalendo nk. tubuni namna ya kumuenzi kwa namna alivyojitoa katika kutetea Mazingira bora ya afya na hata kupelekea kumwaga damu na maumivu makubwa kutokana na kuteswa kikatili kwaajili ya msimamo/kuongoza harakati za mabadiliko. Jina hili libakie katika Historia ili iwe kama kielelezo cha kukumbushana kwenye mamlaka mbalimbali ni namna gani tunaweza kushughulikia mambo ya nayohusu Afya kwa uangalifu mkubwa na kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kama tulizonazo sasa. Wakati huohuo, tunaiomba serikali na Madaktari wote kwa pamoja waweze kurudi tena kwenye meza ya majadiliano ili watafute ufumbuzi wa busara katika mgogoro huu hatari. Tunaomba tofauti zote ziwekwe pembeni na pasiwe na ushindani ama kutafutwa aliyepelekea yanayoendelea. Lengo kuu liwe katika uhakika wa Afya ya Mtanzania katika mazingira bora tunayoweza kuyamudu. Ni vizuri pia pande zote mbili ziweze kufanya jitihada kwa vitendo katika kurudisha imani kwa wananchi kwenye serikali yetu na watu wenye dhamana juu ya Afya zetu. Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Siku yake ya kuzaliwa iwa siku ya haki za wafanyakazi wa Tanganyika. Mimi sipendi sana hawa wanaosheherekea siku za kufa watu, kama wachawi hivi. Kwa mfano Nyerere day ilitakiwa iwe siku yake ya kuzaliwa. Maana Mungu alitupa zawadi, kifaa, Sasa watu wanasherekea siku ya kufa. Mimi nafikiri hili taifa limelaaniwa, ama walikuwa hawampwendi.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Bila kuwasahao wote waliokufa kutokana na mgomo wa madaktari
   
Loading...