#COVID19 Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,876
20,285
Utangulizi- Nawaomba Mods msihamishe uzi huu.

Mchungaji Josephat Gwajima asimamia maeneo mawili katika hoja yake.

Kwanza, kilichomo kwenye chanjo na pili chanjo dhidi ya wanajeshi na walinda usalama wa nchi.

La kwanza kuhusu kilichomo kwenye chanjo au (content).

Mchungaji Gwajima anadai ni lazima madaktari wajiridhishe kuwa kilichomo katika chanjo nyingi zilizowasili Tanzania jana ni sawa na kilichomo katika chanjo walopewa raia wa nchi zilizoendelea.

Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu nchi nyingi zilizoendelea zilipokea idadi kubwa ya chanjo za Covid-19 na kufikia mwezi Juni mwaka huu Marekani pamoja na Uingereza zikaanza kusema kuwa zitapeleka dawa zilizobakia katika nchi maskini.

Ahadi hiyo ilitolewa na Raisi Biden na Boris Johnson wa Uingereza katika mkutano wa nchi tajiri 7 au G7 ulofanyikia katika mji wa Cornwall nchini Uingereza.

Covid vaccine: UK and US to give leftover doses to poorer countries kupitia BBC Covid vaccine: UK and US to give leftover doses to poorer countries - CBBC Newsround

Lakini siku moja kabla ya mkutano huo raisi Biden aliahidi kutoa msaada wa dawa za chanjo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500-

US to donate 500 million Pfizer COVID-19 vaccine doses globally: Report- US to donate 500 million Pfizer COVID-19 vaccine doses globally: Report

Sasa tukirudi katika hoja ya mchungaji Gwajima kwamba lazima tuangazie kilichomo (Content) katika chanjo hizo zote ni ya kuzingatiwa.

Wenzetu wazungu wao walikwishajipanga vilivyo katika suala zima la kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO -19 na kwa muktadha huo waliweza kutengeneza vipeperushi na vielelezo vingine ambavyo zinalenga kumuelimisha mchanjwaji mtarajiwa kuwa ni aina ipi ya chanjo anaweza kupata, imetengenezwa vipi kwa kutumia nini, na inabeba vitu gani na kisha madhara yake baada ya kudungwa au "side effects"

Hivyo taarifa zoote kuhusu UVIKO-19 zimo katika tovuti za serikali za nchi zote zilizoendelea na mtu aweza kusoma na kuelewa bila shida.

Serikali ya Tanzania ingeweza kabisa kufanya hili ilipokuwa ikijiandaa kupokea chanjo na kuondoa uwezekano wa mijadala ambayo yaonekana wazi kuwa haiwezi kuzuia utekelezaji wa kudunga watanzania chanjo hizo.

Sasa hizo chanjo zina namba maalum au bechi au kwa kiingereza batch number hivyo pfizer yaweza kuitwa BNT163C1 au 161C2 na kadhalika.

Hizi namba zinatofautina na ukiwa umedungwa BNT163C1 basi ni lazima uje udungwe dozi ya pili ambayo ni kutoka katika bechi hiyohiyo yaani yaweza kuwa BNT163C3 lakini haiwezi kuwa BNT200b1 ambayo yaweza kuwa ndo inoleta madhara kama kuganda kwa damu.

Ni hivyohivyo kwa chanjo za Moderna, Johnson &Johnson na Pfizer ambazo pia zinatumia bechi tofauti.

Moderna inayotumika kwa mtu A yenye bechi namba 3001729 ndo hiyohiyo itayotumika kwa mtu huyohuyo A lakini itafuatia kidogo na kuwa 3001830.

Mtu anechanjwa Pfizer BioNTech ni lazima achanjwe dozi hiyohiyo ya chanjo hiyohiyo.

Nchi kadhaa za Ulaya na Marekani wakiangalia namba ya bechi ambayo msafiri amechomwa kuna ambao wanakataliwa kuingia katika nchi hizo kwa kuwa amechomwa chanjo ambayo ni ya kutoka kwenye bechi ambayo ina matatizo ya kuleta kuganda kwa damu na homa kali isokwisha.

Katika chanjo zote chanjo ya Oxford Astra Zeneca ndo chanjo ambayo haihitaji baridi kali kuitunza hivyo kuifanya iwe rahisi kuihifadhi katika jokovu la kawaida kama yale ya majumbani.

Chanjo zingine zote huitaji majokovu maalum ambayo pia ni lazima yawe katika mazingira ya kutoweza kuvurugwa na waswahili au kuwa "compromised".

Hivyo hapa nina imani pia kuwa Serikali imewekeza vilivyo katika idara ya uhifadhi na ugavi wa chanjo hizi na hakutakuwa na dalili za kuzivuruga chanjo hizo.

Sasa basi, mchungaji Gwajima anadai ni lazima tujiridhishe kuwa dawa hizi za chanjo zina kiwango kilichomo (content) sawa na chanjo walochomwa wazungu huko Ulaya na Marekani.

Kwenye hili ana hoja kwani hatufahamu dawa hizi za chanjo zimepitia wapi, zimehifadhiwa vipi, zitabadilika vipi kiubora (yaani quality) na je zitaleta madhara yepi mwilini?

Lakini kwa kuwa dawa za chanjo zimekwishatua nchini na pamoja na maoni kadhaa yakiwemo niliyowahi kuyatoa huko nyuma kuwa tuwe waangalifu na chanjo hizi cha msingi ni kuanza na wale wananchi ambao wako hoi mahospitalini na wengine ambao wameathirika zaidi.

Kisha kama nilivyowahi kupendekeza huko nyuma ni kwamba serikali itengeneze makundi ya wataochanjwa na kuweka utaratibu kulingana na mahitaji yaani wazee, wale wenye hali tata kiafya na kisha wale wanotaka kusafiri kwenda nchi zingine ambako wanataka msafiri awe amechanjwa dozi mbili.

Nikija kwenye suala la pili kuhusu wanajeshi, watu wa usalama na wengine wenye majukumu mazito ya kuilinda nchi hii, hapa pia Mchungaji Gwajima ana hoja.

Tusishabikie tu kuwa kwa kuwa wanajeshi watachanjwa basi ni sawa, inatubidi kama taifa tuangalie maslahi ya taifa hili, usalama wake na mstakabali wake kwa miaka 5 na kuendelea.

Tujiulize ni kwanini Russia, Iran, Israeli, China na nchi zingine makini kwanini wao wametengeneza chanjo zao?

Vita ya sasa duniani imehamia kwa muda katika madawa, biolojia (bilogical warfare) kutoka kwenye vita ya kukimbilia silaha zingine.

Tukumbuke hakuna silaha mbaya sana kama silaha ya kibaolojia ambayo hukaa mwilini kwa muda mrefu usojulikana.

Hivyo viwanda vya madawa navyo vimeamua kujikita katika sekta hivyo ya vita kwa kushindana kutengeneza dawa za chanjo.

Si kwamba dawa hizi za chanjo hazikuwepo, bali kilichotokea ni kwa wenye viwanda hivi kufanikiwa katika kuomba fedha za ufadhili katika kufanya tafiti zao na suala la UVIKO-29 lilipoingia wote wakahamia huko.

Chanjo zote hizi zinatumia teknolojia maalum ili kuweza kutumwa kwenda mwilini na kukutana na chembechembe za damu, baada ya hapo ni utaratibu wa kubadili chembechembe hizi pamoja na Vinasaba au DNA na kutengeneza kitu kingine.

Hivyo je, baada ya miaka 5 hado 10 ijayo endapo rasilimali watu ya vyombo hivi vya ulinzi na usalama itaathirika Serikali itakuwa imejiandaa vipi maana hakutakuwa na jeshi imara, lenye uwezo wa kuilinda nchi ipasanyo dhidi ya uvamizi wowote wenye nguvu kubwa.

Hivyo haya Mchungaji Gwajima ana hoja asikilizwe na asibezwe kwani yeye anatumia jicho la tatu katika kuangalia na kusoma alama za nyakati.

Sie wengine wote tunapaswa kutafakari maoni kama hayo na kuyatumia katika kutafuta ukweli zaidi

Nimalizie kwa kusema mimi nilipokuwa nasoma sekondari enzi hizo, somo la jiografia lilikuwa ni moja ya masomo niloyapenda sana.

Kuna siku mwalimu alituuliza darasani nini vyanzo vya mmomonyoko wa ardhi na maporoko yake yaani "Landslide".

Lakini usiku wa jana yake palinyesha mvua kubwa sana na tukasikia kuna mifugo kadhaa imebebwa na na kusombwa na maji na kupotea ziwani.

Pia kulikuwepo na katetemeko kadogo ka ardhi yaani (Earth tremor) ambako kalisababisha nyumba kuyumba kidogo kwa muda wa dakika kadhaa.

Asubuhi katika kipindi mwalimu akasimulia juu ya ile "landslide" na vifo vya mifugo, kisha akauliza nini kinasababisha mmomonyiko wa ardhi khasa lile lilotokea usiku?

Mimi kwa kukumbuka ile hali ya usiku nikajibu kuwa moja ni tetemeko, na pili ni mvua kubwa pamoja na shughuli kama ukataji miti na ujenzi.

Mwanafunzi mwingine kajibu kuwa ni kuyeyuka kwa mapande ya barafu au Glaciers.

Mwalimu akatabasamu na kuinua kichwa kuashiria amekubaliana na majibu yote, lakini akamgeukia mwanafunzi mwenzetu na akamwambia" umesema Glaciers lakini hapa hatupo Greenland au Patagonia Pampas"

Akaendelea, "tujaribu sana kutafuta majibu katika mazingira tuliyopo kabla ya kwenda mbali na ng'ambo huko". akamaliza.

Hii sentensi yake sijaweza kuisahamu hadi leo na imenisaidia sana katika kutafuta masuluhisho ndani ya mazingira niliyopo.

Hivyo pamoja na misaada tuipatayo kutoka nje zikiwemo chanjo cha magonjwa kama UVIKO-19 bado tuna budi kama taifa kujiwekea utaratibu kuwa tunajenga maabara za kisasa na vituo vya kufanya utafiti na kuhakikisha tunamwaga fedha humo kutafuta chanjo ya UVIKO- 19 ya Kitanzania.

Kwa njia hiyo tutakuwa tumejitatulia matatizo yetu wenyewe kwa kutumia wataalam wetu wenyewe na rasilimali zetu wenyewe, huko nje tukazane kuomba misaada ya teknolojia.
 
Kumbe na wewe hauna akili kama Gwajima? Umeandika utopolo mtupu! Kwanza hizo chanjo hazidhuru DNA kama wewe na Gwajiboy mnavyowadanganya watu.

Chanjo ya COVID-19 haibadili au kuingiliana na DNA yako kwa njia yoyote. Chanjo zote za mRNA na virusi vya virusi vya COVID-19 hutoa maagizo kwa seli zetu ili kuanza kujenga kinga dhidi ya virusi vinavyosababisha COVID-19. Lakini, nyenzo hizo haziingii kamwe kwenye kiini cha seli, ambayo ndio huhifadhiwa DNA yetu.

Pia Gwajima anasema hiyo COVID-19 itaisha yenyewe na hataki mwananchi yeyote apate chanjo. Hilo la kusema zipimwe “chemicals” zake, ni kama tu tayari keshaaminisha watu kuwa chanjo ni mbaya na kuzipima ni ili kusapoti hoja yake. Labda angesema zipimwe kwanza ndiyo maamuzi yafanyike, lakini yeye anaongea as if tayari keshafahamu kuwa chanjo ni mbaya. Angeacha kauli ambayo imeshatewa kuwa chanjo ni hiyari na siyo lazima. Lasivyo atakuwa responsible kwa watakaopoteza maisha yao kwasababu ya vitisho vyake.

Kuna wale wanaosema kuwa chanjo haizuii kupatwa tena na COVID-19. Ni kweli, lakini imetokea zaidi kwenye wimbi hili la “Delta variant”, hata hivyo, chanjo bado inasaidia wale waliochanjwa wasipate madhara makubwa yanayosababishwa na virusi hivyo ikiwemo kupelekwa hospitali na hata kupoteza maisha yao.

Muwe munajishughulisha kufanya viji “research” vidogo vidogo ili kuweza kuelewa jambo badala ya kukurupuka tu.
 
Ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025 chini ya mwenyekiti wake Hayati Dr John Pombe Magufuli ilisema kuwa moja ya mipango yao ni kuhakikisha inatengwa bajeti ya kutosha ili kuisaidia NIMR iweze kufanya tafiti juu ya magonjwa mbalimbali na kutafutia chanjo pamoja na tiba zake.

Hayati Magufuli kafariki lakini sasa tunadikia kuna kiwanda kitajengwa kwaajili ya utengenezaji wa chanjo, ukiuliza chanjo gani utajibiwa hizohizo Johson Johson
 
Umeandika mambo mengi bila ya kufuatilia naona watu wengi bongo wanapenda kutokujua,yaani kitu kinachomfuraisha mbongo ni 'not to know' ndo maana tumejaa kebehi na ubishi.

Nchi nyingi tajiri ndo zimeathirika sana na covid, ivo kupatikana na chanjo kwao ilikuwa ni habari njema na wakataka kuchanja watu wao wote. Kufanya ivi wakaingia mikataba na kampuni zinazotengeneza chanjo ili wazipate wao kwanza kwa ufupi walijirimbikizia machanjo kibao kuliko mahitaji, sasa washachanja wengi na ma store zimejaa bado,ndo hizo wameamua kuchangia nchi maskini.

Israel hawajatengeneza chanjo yao wametumia Pfizer imegunduliwa na ujerumani na wanatengeneza kwa ushirikiano na America.

Masuala ya damu kuganda, yameisha zamani chanjo zaid ya billioni moja zimetolewa we umebaki na damu kaganda.
 
Kumbe na wewe hauna akili kama Gwajima? Umeandika utopolo mtupu! Kwanza hizo chanjo hazidhuru DNA kama wewe na Gwajiboy mnavyowadanganya watu...
Jifunze kutumia lugha ya kiungwana. Sie kila alie na maoni tofauti na weye hana akili.

Nimetoa maoni Mchungaji asikilizwe na si kubezwa.

Hayo pia ni maoni yangu haimaanishi kuwa naunga mkono ila nami pia nametoa maoni.
 
Jifunze kutumia lugha ya kiungwana. Sie kila alie na maoni tofauti na weye hana akili...
Maoni gani? Gwajima yeye anasema mtu yeyote asichanjwe. Wewe unasema asikilizwe kwa hilo?

Chanjo zenyewe ni hiyari, lakini mnaleta taharuki ambayo lazima itali cost Taifa. Subiri uone hii delta variant itavyowanyoosha ndiyo watie akili wenyewe.

Pia wewe umeona tu hapo pa kukosa uugwana, umeshindwa kujitetea uongo wako mwingine kuwa chanjo inaingia kwenye DNA.

Pia unataka tujifananishe na Urusi, China sijui na wengine waliotengeneza chanjo zao wenyewe. Hujui hayo mataifa kila kitu yanatengeneza vya kwao wenyewe? Unataka ionekane kuwa ni kwenye chanjo peke yake? Acheni kuleta taharuki, mna manufaa gani na wakati ni wazi kuwa chanjo ni hiyari?
 
Maoni gani? Gwajima yeye anasema mtu yeyote asichanjwe. Wewe unasema akilizwe kwa hilo?

Chanjo zenyewe ni hiyari, lakini mnaleta taharuki ambayo lazima itali cost Taifa. Subiri uone hii delta variant itavyowanyoosha ndiyo watie akili wenyewe.
Basi punguza jazba maana chanjo ndo zipo kwenye majokofu zatusubiri.
 
Acha unafiki, kama wewe hauchanjwi, waache wenye kutaka wachanjwe. Upo huko Uingereza lakini exposure haijakusaidia.

Halafu unajibu fasta sana, na haujibu hoja kwasababu unaongea kama upo kwenye kijiwe cha kahawa bila facts. Weka ushahidi kuwa chanjo inaingia kwenye DNA.
 
Umeandika mambo mengi bila ya kufuatilia naona watu wengi bongo wanapenda kutokujua,yaani kitu kinachomfuraisha mbongo ni 'not to know' ndo maana tumejaa kebehi na ubishi...
Mchungaji Gwajima anahoji, je chanjo wanopewa huko duniani ni sawa na hizi chanjo zilotua jana Dar?

Vipi content yake ni ileile

Je, ni zipi bechi zake ni zilezile zinazosababisha blood clot?

Huoni kuwa huyu mtu auliza masuali ya msingi?
 
Acha unafiki, kama wewe hauchanjwi, waache wenye kutaka wachanjwe. Upo huko Uingereza lakini exposure haijakusaidia.

Halafu unajibu fasta sana, na haujibu hoja kwasababu unaongea kama upo kwenye kijiwe cha kahawa bila facts. Weka ushahidi kuwa chanjo inaingia kwenye DNA.

How does the AstraZeneca/Oxford vaccine work?​

The vaccine – called ChAdOx1 nCoV-19 – uses a harmless, weakened version of a common virus which causes a cold in chimpanzees.

The virus is genetically modified so that it is impossible for it to grow in humans.

Scientists have transferred the genetic instructions for coronavirus’s specific ‘spike protein’ – which it needs to invade cells – to the vaccine.

When the vaccine enters cells inside the body, it uses this genetic code to produce the surface spike protein of the coronavirus.

This induces an immune response, priming the immune system to attack coronavirus if it infects the body.

Source: PA

Hapo penye BOLD ndipo DNA inafanyiwa kitu chaitwa tweek.

Na hapo ndipo ilipo hoja ya mchungaji Gwajima.
 
shida ni ujuaji mwingi...we umeshaambiwa chanjo ni hiari unahamasisha watu ujinga yani wataalamu na watafiti wapitishe maoni ambayo wamegaramika elimu na muda wao wewe uje tu na conspiracy za hearsay,gwajisay without any official utafiti...hata hivyo ndio domokrasia bt use it kwa manufaa na sio kupotosha
 
Mchungaji Gwajima anahoji, je chanjo wanopewa huko duniani ni sawa na hizi chanjo zilotua jana Dar?

Vipi content yake ni ileile

Je, ni zipi bechi zake ni zilezile zinazosababisha blood clot?

Huoni kuwa huyu mtu auliza masuali ya msingi?
Hakuna dawa wala chanjo yoyote ambayo haina “side effects “. Hata hizo “blood clots “ ni “side effects” kwa baadhi tu ya watu. Sijui kwanini haufanyi “research” kabla ya kufikia “conclusion” ambayo unakuja nayo humu JF kisa Gwajima kasema? Wewe una “exposure”, lakini unashikiwa akili.

Zenyewe kufanyiwa uhakiki kuhusu “ingredients”, ni suala zuri. Lakini kusema eti hizo dawa zinasababisha damu kuganda, ni upotoshaji!

Dawa nyingi ambazo tumezoea kuzitumia, ukiwekewa “side effects effects” zake hapa utashangazwa na kuogopa.

Sasa wewe unakuja na “blanket statements”, halafu unatoa eti “reference” ni Gwajima. Kwani muna i “politicize” hii issue?
 
Utangulizi- Nawaomba Mods msihamishe uzi huu.

Mchungaji Josephat Gwajima asimamia maeneo mawili katika hoja yake.

Kwanza, kilichomo kwenye chanjo na pili chanjo dhidi ya wanajeshi na walinda usalama wa nchi.

La kwanza kuhusu kilichomo kwenye chanjo au (content).

Mchungaji Gwajima anadai ni lazima madaktari wajiridhishe kuwa kilichomo katika chanjo nyingi zilizowasili Tanzania jana ni sawa na kilichomo katika chanjo walopewa raia wa nchi zilizoendelea.

Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu nchi nyingi zilizoendelea zilipokea idadi kubwa ya chanjo za Covid-19 na kufikia mwezi Juni mwaka huu Marekani pamoja na Uingereza zikaanza kusema kuwa zitapeleka dawa zilizobakia katika nchi maskini.

Ahadi hiyo ilitolewa na Raisi Biden na Boris Johnson wa Uingereza katika mkutano wa nchi tajiri 7 au G7 ulofanyikia katika mji wa Cornwall nchini Uingereza.

Covid vaccine: UK and US to give leftover doses to poorer countries kupitia BBC Covid vaccine: UK and US to give leftover doses to poorer countries - CBBC Newsround

Lakini siku moja kabla ya mkutano huo raisi Biden aliahidi kutoa msaada wa dawa za chanjo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500-

US to donate 500 million Pfizer COVID-19 vaccine doses globally: Report- US to donate 500 million Pfizer COVID-19 vaccine doses globally: Report

Sasa tukirudi katika hoja ya mchungaji Gwajima kwamba lazima tuangazie kilichomo (Content) katika chanjo hizo zote ni ya kuzingatiwa.

Wenzetu wazungu wao walikwishajipanga vilivyo katika suala zima la kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO -19 na kwa muktadha huo waliweza kutengeneza vipeperushi na vielelezo vingine ambavyo zinalenga kumuelimisha mchanjwaji mtarajiwa kuwa ni aina ipi ya chanjo anaweza kupata, imetengenezwa vipi kwa kutumia nini, na inabeba vitu gani na kisha madhara yake baada ya kudungwa au "side effects"

Hivyo taarifa zoote kuhusu UVIKO-19 zimo katika tovuti za serikali za nchi zote zilizoendelea na mtu aweza kusoma na kuelewa bila shida.

Serikali ya Tanzania ingeweza kabisa kufanya hili ilipokuwa ikijiandaa kupokea chanjo na kuondoa uwezekano wa mijadala ambayo yaonekana wazi kuwa haiwezi kuzuia utekelezaji wa kudunga watanzania chanjo hizo.

Sasa hizo chanjo zina namba maalum au bechi au kwa kiingereza batch number hivyo pfizer yaweza kuitwa BNT163C1 au 161C2 na kadhalika.

Hizi namba zinatofautina na ukiwa umedungwa BNT163C1 basi ni lazima uje udungwe dozi ya pili ambayo ni kutoka katika bechi hiyohiyo yaani yaweza kuwa BNT163C3 lakini haiwezi kuwa BNT200b1 ambayo yaweza kuwa ndo inoleta madhara kama kuganda kwa damu.

Ni hivyohivyo kwa chanjo za Moderna, Johnson &Johnson na Moderna ambazo pia zinatumia bechi tofauti.

Moderna inayoyumika kwa mtu A yenye bechi namba 3001729 ndo hiyohiyo itayotumika kwa mtu huyohuyo A lakini itafuatia kidogo na kuwa 3001830.

Mtu anechanjwa Pfiser BioNTech ni lazima achanjwe dozi hiyohiyo ya chanjo hiyohiyo.

Nchi kadhaa za Ulaya na Marekani wakiangalia namba ya bechi ambayo msafiri amechomwa kuna ambao wanakataliwa kuingia katika nchi hizo kwa kuwa amechomwa chanjo ambayo ni ya kutoka kwenye bechi ambayo ina matatizo ya kuleta kuganda kwa damu na homa kali isokwisha.

Katika chanjo zote chanjo ya Oxford Astra Zeneca ndo chanjo ambao haihitaji baridi kali kuitunza hivyo kuifanya iwe rahisi kuihifadhi katika jokovu la kawaida kama yale ya majumbani.

Chanjo zingine zote huitaji majokovu maalum ambayo pia ni lazima yawe katika mazingira ya kutoweza kuvurugwa na waswahili au kuwa "compromised".

Hivyo hapa nina imani pia kuwa Serikali imewekeza vilivyo katika idara ya uhifadhi na ugavi wa chanjo hizi na hakutakuwa na dalili za kuzivuruga chanjo hizo.

Sasa basi, mchungaji Gwajima anadai ni lazima tujiridhishe kuwa dawa hizi za chanjo zina kiwango kilichomo (content) sawa na chanjo walochomwa wazungu huko Ulaya na Marekani.

Kwenye hili ana hoja kwani hatufahamu dawa hizi za chanjo zimepitia wapi, zimehifadhiwa vipi, zitabadilika vipi kiubora (yaani quality) na je zitaleta madhara yepi mwilini?

Lakini kwa kuwa dawa za chanjo zimekwishatua nchini na pamoja na maoni kadhaa yakiwemo niliyowahi kuyatoa huko nyuma kuwa tuwe waangalifu na chanjo hizi cha msingi ni kuanza na wale wananchi ambao wako hoi mahospitalini na wengine ambao wameathirika zaidi.

Kisha kama nilivyowahi kupendekeza huko nyuma ni kwamba serikali itengeneze makundi ya wataochanjwa na kuweka utaratibu kulingana na mahitaji yaani wazee, wale wenye hali tata kiafya na kisha wale wanotaka kusafiri kwenda nchi zingine ambako wanataka msafiri awe amechanjwa dozi mbili.

Nikija kwenye suala la pili kuhusu wanajeshi, watu wa usalama na wengine wenye majukumu mazito ya kuilinda nchi hii, hapa pia Mchungaji Gwajima ana hoja.

Tusishabikie tu kuwa kwa kuwa wanajeshi watachanjwa basi ni sawa, inatubidi kama taifa tuangalie maslahi ya taifa hili, usalama wake na mstakabali wake kwa miaka 5 na kuendelea.

Tujiulize ni kwanini Russia, Iran, Israeli, China na nchi zingine makini kwanini wao wametengeneza chanjo zao?

Vita ya sasa duniani imehamia kwa muda katika madawa, biolojia (bilogical warfare) kutoka kwenye vita ya kukimbilia silaha zingine.

Tukumbuke hakuna silaha mbaya sana kama silaha ya kibaolojia ambayo hukaa mwilini kwa muda mrefu usojulikana.

Hivyo viwanda vya madawa navyo vimeamua kujikita katika sekta hivyo ya vita kwa kushindana kutengeneza dawa za chanjo.

Si kwamba dawa hizi za chanjo hazikuwepo, bali kilichotokea ni kwa wenye viwanda hivi kufanikiwa katika kuomba fedha za ufadhili katika kufanya tafiti zao na suala la UVIKO-29 lilipoingia wote wakahamia huko.

Chanjo zote hizi zinatumia teknolojia maalum ili kuweza kutumwa kwenda mwilini na kukutana na chembechembe za damu, baada ya hapo ni utaratibu wa kubadili chembechembe hizi pamoja na Vinasaba au DNA na kutengeneza kitu kingine.

Hivyo je, baada ya miaka 5 hado 10 ijayo endapo rasilimali watu ya vyombo hivi vya ulinzi na usalama itaathirika Serikali itakuwa imejiandaa vipi maana hakutakuwa na jeshi imara, lenye uwezo wa kuilinda nchi ipasanyo dhidi ya uvamizi wowote wenye nguvu kubwa.

Hivyo haya Mchungaji Gwajima ana hoja asikilizwe na asibezwe kwani yeye anatumia jicho la tatu katika kuangalia na kusoma alama za nyakati.

Sie wengine wote tunapaswa kutafakari maoni kama hayo na kuyatumia katika kutafuta ukweli zaidi

Nimalizie kwa kusema mimi nilipokuwa nasoma sekondari enzi hizo, somo la jiografia lilikuwa ni moja ya masomo niloyapenda sana.

Kuna siku mwalimu alituuliza darasani nini vyanzo vya mmomonyoko wa ardhi na maporoko yake yaani "Landslide".

Lakini usiku wa jana yake palinyesha mvua kubwa sana na tukasikia kuna mifugo kadhaa imebebwa na na kusombwa na maji na kupotea ziwani.

Pia kulikuwepo na katetemeko kadogo ka ardhi yaani (Earth tremor) ambako kalisababisha nyumba kuyumba kidogo kwa muda wa dakika kadhaa.

Asubuhi katika kipindi mwalimu akasimulia juu ya ile "landslide" na vifo vya mifugo, kisha akauliza nini kinasababisha mmomonyiko wa ardhi khasa lile lilotokea usiku?

Mimi kwa kukumbuka ile hali ya usiku nikajibu kuwa moja ni tetemeko, na pili ni mvua kubwa pamoja na shughuli kama ukataji miti na ujenzi.

Mwanafunzi mwingine kajibu kuwa ni kuyeyuka kwa mapande ya barafu au Glaciers.

Mwalimu akatabasamu na kuinua kichwa kuashiria amekubaliana na majibu yote, lakini akamgeukia mwanafunzi mwenzetu na akamwambia" umesema Glaciers lakini hapa hatupo Greenland au Patagonia Pampas"

Akaendelea, "tujaribu sana kutafuta majibu katika mazingira tuliyopo kabla ya kwenda mbali na ng'ambo huko". akamaliza.

Hii sentensi yake sijaweza kuisahamu hadi leo na imenisaidia sana katika kutafuta masuluhisho ndani ya mazingira niliyopo.

Hivyo pamoja na misaada tuipatayo kutoka nje zikiwemo chanjo cha magonjwa kama UVIKO-19 bado tuna budi kama taifa kujiwekea utaratibu kuwa tunajenga maabara za kisasa na vituo vya kufanya utafiti na kuhakikisha tunamwaga fedha humo kutafuta chanjo ya UVIKO- 19 ya Kitanzania.

Kwa njia hiyo tutakuwa tumejitatulia matatizo yetu wenyewe kwa kutumia wataalam wetu wenyewe na rasilimali zetu wenyewe, huko nje tukazane kuomba misaada ya teknolojia.
You must be joking ndugu.

Unamwongelea Gwajima yupi? Huyu huyu aliyedai anafufua wafu lakini akashindwa kumfufua rafiki yake kipenzi Magufuli?
 
Hakuna dawa wala chanjo yoyote ambayo haina “side effects “. Hata hizo “blood clots “ ni “side effects” kwa baadhi tu ya watu. Sijui kwanini haufanyi “research” kabla ya kufikia “conclusion” ambayo unakuja nayo humu JF kisa Gwajima kasema? Wewe una “exposure”, lakini unashikiwa akili.

Zenyewe kufanyiwa uhakiki kuhusu “ingredients”, ni suala zuri. Lakini kusema eti hizo dawa zinasababisha damu kuganda, ni upotoshaji!

Dawa nyingi ambazo tumezoea kuzitumia, ukiwekewa “side effects effects” zake hapa utashangazwa na kuogopa.

Sasa wewe unakuja na “blanket statements”, halafu unatoa eti “reference” ni Gwajima. Kwani muna i “politicize” hii issue?
Nafikiri hujasoma mada nzima niloandika.

Nimesema zipo nchi kadhaa ambazo huingii kama bechi namba ulodungwa sindano ya chanjo ni moja ya zile zenye matatizo hivyo hio yaonyesha kuwa bado zipi dawa ambazo zina matatizo.

Hii pia ni kutokana na sababu kwamba hizi dawa hupitia viwanda hadi vinne katika hatua tofauti kabla ya kukamilika kuwa dawa kamili.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom