Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Natoa masikitiko makubwa kwa Mwenyekiti wangu aliyepita, Rais Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowalea wasanii wetu ndani ya chama chetu, CCM. Awali nilidhani kuwa ni uzalendo ndio uliowafanya akina Wema Sepetu na Steven Nyerere kuzunguka nchi nzima kuinadi CCM kupitia kampeni yao ya Mama Ongea na Mwanao. Kumbe haikuwa uzalendo na mapenzi kwa chama bali ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Ni kuuza na kununua. Ni Give and Take kama alivyothibitisha Wema Sepetu. Hata hivyo, ni wakati sahihi sasa wa kumsamehe Kikwete kwani kila mtu ana namna yake ya kushawishi watu.
Mbaya zaidi ni pale baadhi ya watu hao akiwemo Wema Sepetu kujinasibisha kuwa ni makada wa CCM tena walienda mbali na kugombea kuteuliwa nafasi ya ubunge ilhali wanajua kuwa uwepo wao ndani ya chama ni kwa maslahi zaidi kuliko mahaba. Niwapongeze wale waliosimamia mchakato wa mchujo wa wagombea na hatimaye kuwatema akina Wema. Wangetutia aibu. Wasingekuwa tofauti na akina Joyce Mukya ambao uwepo wao ndani na Bunge hauna maana yoyote.
Sasa chama kipo na Comredi John Pombe Magufuli ambaye anasisitiza umuhimu wa watu kufanya kazi ili wale. Si kuishi kwa kutegemea fadhila kama walivyolelewa na Baba Kikwete. Hali hii imewafanya baadhi ya watu akiwemo Steven Nyerere na Wema Sepetu kuwa na wakati mgumu ndani ya chama kiasi cha kuamua kuja na mikakati ovu ya kukiumiza chama. Thanks God. Wameumbuka hasa baada ya kuvuja kwa ile Voice Note ya Mama na Mwanaye ambao tunaweza kuwaita ni Mama na Serengeti Boy wake.
Nitumie fursa hii kuwaasa viongozi wangu. Huu ni wakati sahihi wa kujua kati ya pumba na mchele. Wenye mahaba ya dhati na CCM wanajulikana sasa na wale waliokuwa ndani ya chama kwa sababu ya matumbo yao wanaanza kuumbuka. Simamieni chama kilichoachwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa wale wote mliozamia chama. Huu ni wakati muafaka wa kujitafakari. Hatutaki tutakapofika mwaka 2020 tuwe na mizigo yenye mtima nyongo na viongozi wetu. Haya ndio maisha tuliyoamua kuishi wana CCM kwa sasa. KUFANYA KAZI. Kama umezoea kulelewa na kubembelezwa basi wakati huo umeshapita.