Tumsaidieje mkulima huyu asiye na akili

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Hadithi hadithi

"Katika kijiji kimoja cha wawindaji, ufugaji wa mbwa ilikuwa ni jambo ambalo haliepukiki ili watumike kwenye uwindaji.

Pakawepo mkulima mmoja ambaye katika kujikusanyia mbwa wa kufuga akakutana na katoto ka mbwa kalikoonekana kazuri sana. Akakachukua akakafuga nyumbani kwake. Kadiri kalivyozidi kukua, kale ka mbwa kalikuwa hodari kwa uwindaji. Uhodari wake ulizidi kwani kalikuwa na uwezo wa kwenda porini kenyewe au na mbwa wenzake bila ya bwana wake, na kaliwinda na kurudi nyumbani na mawindo lukuki.

Uhodari wa ka mbwa haka pia ulizidi kwa kuwa kalikuwa na uwezo wa kuleta vimbwa vingine pale nyumbani kwa bwana wake ambavyo kalikuwa kanavilisha na mawindo yake. Kakakua kakawa jibwa kubwa na hodari. Jibwa hili likajenga himaya yake ya mbwa wengi lakini wote wakiwa chini ya bwana wake. Kutokana na uwezo wa jibwa hili kwenda mawindoni na mbwa waliochini yake na kuleta nyama nyumbani, mfugaji wake akawa haendi tena mawindoni, akawa mvivu. Kila siku analetewa nyama za kila aina.

Jibwa likawa linaleta nyama na za ziada, mfugaji akawa anauza kwa wingi na kuwa tajiri, hali iliyomfanya awe mtawala katika kijiji kile.

Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda, kukaanza kutokea malalamiko kuwa jibwa lile la mtawala hakuwa mbwa. Watu wakaanza kutoa ushuhuda kuwa jibwa lile lilipotoka kwa bwana wake lilijibadilisha na kuwa dubwana la kutisha. Chui si chui, simba sio simba, ili mradi lilikuwa dude la kutisha. Sio lenyewe tu bali hata mbwa liliowaleta pale kwa bwana wake ambao walikuwa chini yake nao walikuwa wanajibadilisha na kuwa viumbe wa ajabu. Tena wanakijiji wakalalamika kuwa jibwa lile lilikuwa linakula mifugo yao na mawindo yao. Hata hivyo mtawala yule ambaye ndiye mwenye jibwa akawapuuza. Kila walipolalamika akawapuuza.

Malalamiko yakaongezeka na sasa ikawa watu wanalalamika kuwa jibwa lile la ajabu lilikuwa linaua na kula watoto wao!. Mwenye jibwa akapuuza na zaidi kila aliyelalamika aliadhibiwa vikali.

Kwa kuwa kila shughuli pale kwa mtawala zilitawaliwa na jibwa lile, hata mtawala aliwapuuza na hata kuwasahau wanae. Baadhi ya watoto ambao waligundua hujuma za jibwa lile na wakataka kwenda kulalamika kwa baba yao, jibwa lile liliwadhibiti na hata wengine likawaua.

Siku zikaenda mkulima yule akaanza kuzeeka na akataka kurithisha utawala wake kwa mwanae. Jibwa lile likamfuata na kumuambia sasa ni wakati wake wa kutawala. Mfugaji akataka kukataa... lahaula! Jibwa likajibadilisha na kuwa dude la ajabu. Likafunua mdogo wenye moto kwa hasira na kumuambia mfugaji kuwa kama hatalipa mamlaka ya kutawala litammeza.

Mkulima akabaki ameduwaa hajui afanye nini. Jibwa pamoja na himaya ya mambwa menzake yakabadilika na kuwa midubwana ya kutisha. Mkulima hana la kufanya na hana pa kuomba msaada. Huko nje wanakijiji wamechachamaa wanataka waichome ile kaya moto. Wameizunguka pande zote, mfugaji hana pa kukimbila. Wanampa sharti moja tu ili kuokoa maisha yake na kaya yake. Kuwa aliue jibwa lile na majibwa menzake. Mkulima hawezi, kabaki analalamika na hana cha kufanya"

Jamani tumsaidieje mkulima huyu. Alionywa tangu zamani kuwa kimbwa chako sio mbwa, ni shetani, akaziba masikio akawa anakishangilia.

Hebu semeni tumsaidieje...

Wanalalamika kila siku... ooh kaanza kampeni mapema... ooh anatumia milioni 500 kununua vyombo vya habari... ooh anatumia bilioni 5 kutangaza nia...

Lakini si wao ndio walikuwa wanamshangilia na kumtukua?. Wanajivunia umaarufu aliowajengea?

Tuwasaidije... sisi tunawaacha, kama hamuwezi kuteketeza jibwa lenu, kaya nzima tunaichoma moto...

Kwaherini...
 
Nimeipenda sana hadithi yako.your real a great thinker.nimejifunza kitu.
 
Back
Top Bottom