Tumsaidie Rais wetu kwa kuwazomea hawa wezi wa Mali ya Umma bila kuchoka

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Tumesikia madudu ya kutisha, kama yalivyobainishwa na CAG, namna watanzania wenzetu, wasio na uzalendo hata kidogo, namna wanavyotafuna fedha zetu za Umma bila woga, Kwa kutuibia mabilioni ya pesa.

Hivi Hawa watumishi wachache wa Umma, wanatuona watanzania wote kuwa ni wajinga?

Hivi hizi Kodi zote na matozo mbalimbali, tunayokatwa watanzania masikini, kumbe zinawafaidisha watu wachache, ambao wao kazi yao ni Moja tu, kufanya "dili" ya kutuibia?

Ndiyo maana ninasema ni wajibu wa Kiila mtanzania mzalendo, Kwa hivi Sasa, kumsaidia Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonsha dhamira njema, Kwa nchi hii, tuizomee bila kuchoka, hii mijizi ya fedha ya Umma, Hadi hapo watakapoona aibu na kuiacha hii tabia mbaya ya wizu, ambayo inaelekea italiangamiza kabisa Taifa letu😎
 
Ni kosa kubwa sana kuwaadhibu wabadhirifu wa mali za umma kwa njia za kimaadili tu, na kuacha kuwachukulia hatua stahiki za kisheria. Njia za kimaadili, yaani " molarity" ni za hiari wala hazina meno ya kuweza kuwafungulia mashtaka yao kwa mujibu wa sheria, kuwaburuza mahakamani, kuwahukumu, na kisha kuwaadhibu na kuwatia kolokoloni. Njia za kisheria ndizo hasa sahihi kwa kuwa hazina uhiari bali ni lazima kuzifuata.

Sasa sijui ukitaka kuwazomea, kwanza utawaona wapi!? Kimakazi hauishi nao, kikazi wala haupo karibu nao! Kiuchumi wamekuzidi sana, kwenye nyumba za ibada uheshimika sana, kwani wao hutoa michango mikubwa mikubwa! Kiulinzi wanasindikizwa na ving'ora wawapo barabarani, nyumbani walinzi wakipishana kwa zamu!

Kibaya zaidi wengine ni wanasheria wabobevu ama wanauwezo wa kukodi wanasheria wenye ushawishi wa kupindisha aina ya mashtaka dhidi yao, ama wengine wana kinga ya kutoshtakiwa!

Sehemu moja tu wamepimwa na kuonekana hawatoshi, napo ni Mbele za macho Mungu aliye hai. Kwa kuwa ni watoto vipenzi wa Ibilisi, basi mauti na kuzimu huambatana nao. Sana sana wakifa watazikwa kwa mbwembwe na heshima kubwa ya kibinadamu na miili yao kuhifadhiwa katika majeneza ya kifahari. Lakini kiroho hao ni waliopotea kabisa.
 
Tumesikia madudu ya kutisha, kama yalivyobainishwa na CAG, namna watanzania wenzetu, wasio na uzalendo hata kidogo, namna wanavyotafuna fedha zetu za Umma bila woga, Kwa kutuibia mabilioni ya pesa.

Hivi Hawa watumishi wachache wa Umma, wanatuona watanzania wote kuwa ni wajinga?

Hivi hizi Kodi zote na matozo mbalimbali, tunayokatwa watanzania masikini, kumbe zinawafaidisha watu wachache, ambao wao kazi yao ni Moja tu, kufanya "dili" ya kutuibia?

Ndiyo maana ninasema ni wajibu wa Kiila mtanzania mzalendo, Kwa hivi Sasa, kumsaidia Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonsha dhamira njema, Kwa nchi hii, tuizomee bila kuchoka, hii mijizi ya fedha ya Umma, Hadi hapo watakapoona aibu na kuiacha hii tabia mbaya ya wizu, ambayo inaelekea italiangamiza kabisa Taifa letu😎
Umechoka sana. Wazomewe? Au washikwe na kufungwa? Ati Rais mwenye nia njema! Ukiona wanaiba kweupe kiasi hiki ujuwe hata wee Rais ni dhaifu. At stupid, nani kaliwa? Wewe ndiyo stupid maana umeliwa na umeishia kukoroma ati stupid! Tenda kama una uwezo
 
Ukiona Rais anatamka stupid, ujue kazidiwa na hao wezi wa Mali ya Umma.

Kwa hiyo ndiyo maana, Mimi nimetoa wazo, kuwa hao wezi wa Mali ya Umma, njia pekee tunayoweza kuitumia sisi Wallala hoi, ni kuwazomea bila ukomo!
 
Rais hahusiki. Ukicheza nao hao wezj nchi inayumba, na wataanza kumuwinda rais wammalize kama alivyowahi omba Dkt Magufuli kuwa vita ya kuwazuia wezi wa mali za umma ni ngumu akasisitiza kajitoa sadaka tumuombee.
 
Hela ya serikali sio yako ukipata nafasi ya kupiga zibua kweli kweli ukijidai una huruma wajuba hawana huruma wanapita nayo hawaachi kitu. Hiyo useless report ya CAG inatoka Kila mwaka kumpa CAG mwenyewe 15 minutes of fame afu upigaji unaendelea.
 
Tumesikia madudu ya kutisha, kama yalivyobainishwa na CAG, namna watanzania wenzetu, wasio na uzalendo hata kidogo, namna wanavyotafuna fedha zetu za Umma bila woga, Kwa kutuibia mabilioni ya pesa.

Hivi Hawa watumishi wachache wa Umma, wanatuona watanzania wote kuwa ni wajinga?

Hivi hizi Kodi zote na matozo mbalimbali, tunayokatwa watanzania masikini, kumbe zinawafaidisha watu wachache, ambao wao kazi yao ni Moja tu, kufanya "dili" ya kutuibia?

Ndiyo maana ninasema ni wajibu wa Kiila mtanzania mzalendo, Kwa hivi Sasa, kumsaidia Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonsha dhamira njema, Kwa nchi hii, tuizomee bila kuchoka, hii mijizi ya fedha ya Umma, Hadi hapo watakapoona aibu na kuiacha hii tabia mbaya ya wizu, ambayo inaelekea italiangamiza kabisa Taifa letu😎
Mpaka sisi wananchi tuwazomee inamaana sheria zetu zimeruhusu waibe?
 
Mama kaonesha mapungufu kinoma, analalamika huku mamlaka anayo sasa sie wakulima huku Namtumbo tufanyaje sasa??.
 
Umechoka sana. Wazomewe? Au washikwe na kufungwa? Ati Rais mwenye nia njema! Ukiona wanaiba kweupe kiasi hiki ujuwe hata wee Rais ni dhaifu. At stupid, nani kaliwa? Wewe ndiyo stupid maana umeliwa na umeishia kukoroma ati stupid! Tenda kama una uwezo
Halafu unakuta lile jizi sana ndiyo unakuta anasifia sana juhudi za mheshimiwa kuleta fedha nyingi mikoani
 
Tuwazomee au tuwaombe watuhurumie? unataka kuwazomea kwa nguvu gani ulizonazo za kuwakamata?

Bosi wao mwenyewe hana chakuwafanya, mpaka leo anawatazama tu, wewe mwenzangu na mimi unataka kuwazomea ili wakasirike watupige vizuri, unataka badala ya kutuibia billions waanze kutuibia trillions?
 
Tumesikia madudu ya kutisha, kama yalivyobainishwa na CAG, namna watanzania wenzetu, wasio na uzalendo hata kidogo, namna wanavyotafuna fedha zetu za Umma bila woga, Kwa kutuibia mabilioni ya pesa.

Hivi Hawa watumishi wachache wa Umma, wanatuona watanzania wote kuwa ni wajinga?

Hivi hizi Kodi zote na matozo mbalimbali, tunayokatwa watanzania masikini, kumbe zinawafaidisha watu wachache, ambao wao kazi yao ni Moja tu, kufanya "dili" ya kutuibia?

Ndiyo maana ninasema ni wajibu wa Kiila mtanzania mzalendo, Kwa hivi Sasa, kumsaidia Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonsha dhamira njema, Kwa nchi hii, tuizomee bila kuchoka, hii mijizi ya fedha ya Umma, Hadi hapo watakapoona aibu na kuiacha hii tabia mbaya ya wizu, ambayo inaelekea italiangamiza kabisa Taifa letu😎
Du. Ingekuwa kuzomea wezi kunafanya watu waache kuiba basi kusingekuwa na wezi Tanzania. Kwa nini unazunguka mbuyu? Rais ndiye anasababisha haya. Kurudia kufanya mambo yale yale huku ukitegemea matokeo tofauti ni wendawazimu. Kwa nini haongozi harakati za kubadili mfumo wetu wa uongozi ili kupata watu sahihi na kuzuia wezi kuingia kwenye mfumo? Au kuwagundua mapema?
 
Wabunge walioshinda kwa kishindo, kwa karibia 100%, wako wapi kupaza sauti zao na kuwachukulia hatua hawa watu?.
Kama tatizo ni kuogopana kwa vile wanatoka chama kimoja cha siasa, basi tuwe na katiba inayoruhusu mgombea binafsi.
Tanzania ni kubwa kuliko chama(kikundi fulani cha watu).
 
Correct Kwa asilimia💯

Tupate Katiba mpya ambayo itatoa nafasi ya kuwapata viongozi waadilifu
 
Tumesikia madudu ya kutisha, kama yalivyobainishwa na CAG, namna watanzania wenzetu, wasio na uzalendo hata kidogo, namna wanavyotafuna fedha zetu za Umma bila woga, Kwa kutuibia mabilioni ya pesa.

Hivi Hawa watumishi wachache wa Umma, wanatuona watanzania wote kuwa ni wajinga?

Hivi hizi Kodi zote na matozo mbalimbali, tunayokatwa watanzania masikini, kumbe zinawafaidisha watu wachache, ambao wao kazi yao ni Moja tu, kufanya "dili" ya kutuibia?

Ndiyo maana ninasema ni wajibu wa Kiila mtanzania mzalendo, Kwa hivi Sasa, kumsaidia Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonsha dhamira njema, Kwa nchi hii, tuizomee bila kuchoka, hii mijizi ya fedha ya Umma, Hadi hapo watakapoona aibu na kuiacha hii tabia mbaya ya wizu, ambayo inaelekea italiangamiza kabisa Taifa letu😎
Mkuu jibu la haya yote kuhusu uzalendo ni viongoz wa juu kbs ndio wanapaswa kuonyesha dhamiri ya kweli na wazi ya kupambana na wizi na ufisadi!! Utawala ukionyesha hayo yote hata sisi kama wananchi tutakua wazalendo sana tu!!
 
Acha kuleta ujinga hapa, sheria zipo zifuatwe, VEO akiiba siment 1 kesho mahakamani hawa wanaoiba mabilioni wao ni akina nani? washitakiwe na kufungwa
 
Du. Ingekuwa kuzomea wezi kunafanya watu waache kuiba basi kusingekuwa na wezi Tanzania. Kwa nini unazunguka mbuyu? Rais ndiye anasababisha haya. Kurudia kufanya mambo yale yale huku ukitegemea matokeo tofauti ni wendawazimu. Kwa nini haongozi harakati za kubadili mfumo wetu wa uongozi ili kupata watu sahihi na kuzuia wezi kuingia kwenye mfumo? Au kuwagundua mapema?
Eti ameonyesha dhamira shame on you, kuna dhamira ya dhati zaidi ya kuwakamata hawa majangili wa fedha za umma, hana akili kabisa eti kuzomea ndiyo adhabu imeisha kwa mtu ambaye ameiba mabilioni ya watanzania.
 
Tuwazomee au tuwaombe watuhurumie? unataka kuwazomea kwa nguvu gani ulizonazo za kuwakamata?

Bosi wao mwenyewe hana chakuwafanya, mpaka leo anawatazama tu, wewe mwenzangu na mimi unataka kuwazomea ili wakasirike watupige vizuri, unataka badala ya kutuibia billions waanze kutuibia trillions?
Hapo angekuwa VEO ameiba cement 2 hakuna rangi angeecha kuona.
 
Bila kuweka sheria ya kitanzi kwa wezi na wapiga dili wa mali za Umma ni kazi bure.

Hii Nchi fedha zitaendelea kuporwa tu.
 
Back
Top Bottom