Tumsaidie Rais kwenye ujenzi wa taifa letu kwa nguvu zetu wenyewe

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Baada ya Rais Magufuli kuonekana akiipunguza rushwa Tanzania kwa nguvu zake zote, sisi watanzania inabidi na sisi tuonekane pia tukimsaidia Rais katika ujenzi wa taifa letu kwa nguvu zetu wenyewe kwakuwa sasa tuna uhakika kuwa kodi na michango yetu viko salama.

Mpaka leo hii miaka 56 ya Uhuru Tanzania tuna matatizo makubwa ya maji, usafiri hasa wa reli na majini, elimu, afya, umeme na kilimo, ufugaji na uvuvi duni visivyotosheleza kupata ziada. Wizi, ufisadi, siasa mbovu kabisa za kutaka kulikomboa bara lote la Afrika kwanza, utegemezi wa wahisani na mikopo ya benki ya dunia (WB) na fuko la fedha la kimataifa (IMF) yenye riba kubwa ndivyo vilivyotufikisha hapa tulipo.

Sasa tuseme baaasi, Tuwe tayari kumwambia Rais tuchangie kwa waziwazi nguvu zetu na vipato vyetu katika kulijenga taifa letu sisi wenyewe kwa muda mfupi tu sana. Tumwambie Rais kila mtanzania achangie kwa hiari na kwa lazima katika kulijenga taifa letu sisi wenyewe bila kutegemea watu wengine.

Sio vibaya kila mfanyakazi akakatwa asilimia 5 ya mshahara wake, kilamfanya biashara mbali ya kodi ya lazima lakini pia achangie asilimia 6-10 ya pato lake. Wakulima, wafugaji, wavuvi. viwanda, mahoteli n,k nao wakachangia kwa hiari na lazima ili tupate fedha za kujenga reli, barabara na madaraja, kusambaza maji nchi nzima, kuchimba marambo, kusambaza umeme, kujenga shule na vituo vya afya, kununua meli kuubwa kabisa za kisasa za uvuvi kwenye maziwa, mito na bahari zetu, kusomesha watoto wetu vyuo vikuu bure kabisa, n.k.

Kuchangia kwa njia za wazi (active) kama hizi itasababisha kila mtanzania ajione kama sehemu muhimu ya maendeleo yako pale anapoona hela aliyochangishwa kwa lazima na hiari inajenga daraja pale kwenye mtaa, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda au taifa lake. Hii itaibua moyo na ari kubwa ya uzalendo kwa taifa kwakuwa kila mtu atakuwa mlinzi wa daraja hilo aliloligharamia.

Sasa hivi watu tunalipa kodi wote lakini wengi wetu hatujui kama tunalipa kodi, hivyo hatuoni kuwa sisi ni sehemu ya maendeleo yanayofanywa na serikali, hivyo imekuwa ni vigumu kwa wananchi kumfukuza mwizi wa mafuta ya transfoma za umeme hata kama wanamuona akifanya uhalifu huo.

Rais fanya haraka bwana ulete kamswada haka au toa amri tu hata keshokutwa ili watu waanze kuchangia majogoo yao kwenye ujenzi wa haraka wa reli standard gauge badala ya kutumia hela zao kwa kunywa bia, matamasha ya kucheza uchi na kuongeza wanawake wengine. Itatuuma na kulalamika kidogo lakini baada ya mika 2 hivi tutazoea na kufurahia hasa baada ya kushuhudia maendeleo ya kasi ya ajabu.

Kwenye hili asibakie mtu kuanzia Rais, wanajeshi, polisi, usalama, matajiri, masikini, changudoa na hata wachawi bila kujali itikadi, dini wala utaifa. Wacha kulialia na wahisani, tumechelewa sana.
 
Kila wilaya ipite nyumba kwa nyumba kukusanya mayai, bata, mbuzi, ngombe, mahindi, mihogo kutoka kwenye kaya na kuzitafutia masoko wapate pesa za kujenga majosho ya mifugo, marambo, n.k
 
Back
Top Bottom