Tumsaidie JK kupanga baraza jipya la mawaziri na "kusafisha UVUNDO"

Mtalii,
Hayo yote ni mawazo ya mtu kama navyoweza andika kitabu kuhusu Utawala wa Kikwete na kuuhusisha na tuseme kamati ya ufundi..

Naweza andika kitabu kumhusisha Karume na kanisa la anglican ama Kotoliki Zanzibar yote haya ni tungo za mtu kutokana na kuwepo uhuru wa kila mtu kuimani anachokitaka...
Kesho utakuja sikia kuwa mimi hapa nimebadilisha dini na kuwa Baniani kwa sababut nilionekana jamatini kuhudhulia mazishi ya Patel, basi yakavutwa mahusiano yote ya kibiashara kati yangu na huyo Patel kuonyesha jinsi nilivyoiacha dini yangu na kuwa singasinga...
Please hao wote walioandika vitabu hivyo are loosers kimaisha na pepo, na kwa hasira zao wakaja na hizi habari za kuingiza Utawala na dini hali tunaoyafanya yote haya ni sisi waislaam wenyewe. Nilikwisha kwambia kuwa Mauaji ya mwembechai nakumbuka kabisa mmoja wa wapeplelezi wakubwa wa kituo cha Mwembechai alikuwa Muislaam na alihusika sana na mauaji hayo pamoja na kwamba anaweza sema order ilitoka juu.

Wewe na mimi ni part ya huu mchezo na kama walivyochezewa Wahutu na watusi, Wajaluo kwa Wakikuyu ni mchezo wa kisiasa ambao unatafuta sababu kukamilika... Kwa Tanzania Dini ni njia pekee ya kutenganisha watu na siasa inafanya kazi yake.
 
Ok,

Basi tuone JK kama atateua tu mawaziri just blindly- bila kuangalia representation ya dini, mikoa, gender n.k

Hii kitu ya kushabikia kuwa hakuna kunangalia dini???

Nchi hii ina Waisalamu, Wakristo, Wahindi n.k. Ndo maana nauliza kwa nini JK asipange tu baraza lote liwe na Waislamu tupu au Wakristo tupu?

Tuyajadili! Ni sehemu ya maisha yetu ya kisiasa, na kijamii, tusifumbe macho!
 
hahahah.. we have been there na rafiki yetu hachoki kurudi na "yale yale"...


Mtalii, hivi kila ishu lazima iwe udini tu? Yaaani majuzi tu ulikuwa unamtetea Lipumba, kisa dini!, sasa unamtetea Msabaha, kisa dini! Kwa mwendo huu mkuu kweli tutafika? Haiwezekani kila ishu ikawa udini, mbona hujasema kuhusu Mtawa, mjomba wake Muungwana kuwa msaidizi wake, lakini umewaona kina Apiyo tu?

Mambo ya udini hayana nafasi mkuu kwenye siasa zetu, na yasipewa kabisa hiyo nafasi.
 
Miye nilishasema, sijali kuishi katika nchi inayoongozwa na waislamu watupu, kwa kadiri ya kwamba uongozi wao hautokani na dini hiyo na ni jamhuri (republic). Sijali kama Kikwete atateua Waziri Mkuu au Mawaziri wote toka Uislamu as long as wanapoenda kutekeleza majukumu yao wanafuata Katiba Ya Tanzania na sheria zetu.

Hivi kwa kuangalia majina tu unaweza kujua nani mkristu na nani muislamu? Hawa waliotuletea richmond Lowassa dini gani na Karamagi dini gani? Mmoja tena si aliombewa na Askofu wake awe "aenende duniani na kuwa mkuu wa mafisadi"..? (kidding)
 
Mzaendo halisi.

Nyerere alikuwa akibagua watu kwa dini zao aliwapendelea sana wakristu soma hata kitabu cha the mwembechai killings.na ikulu aweka ndugu zake kama mzee Apiyo kuwa katibu mkuu wa Ikulu.

halikadhalika MKAPA aliweka waziri mkuu mkristu huku rais akiwa yeye mkristu makatibu wakuu wengi wakristu na wizara nyeti zote aliweka mawaziri wakristu.

kwenye chama chake yeye alikuwa Mwenyekiti-mkristu, katibu mkuu mangula-mkristu, makamu mwenyekiti John Malecela-mkristu,katibu mwenezi -Jackson Msome -mkristu, kulikuwa na kina Chizi , barongo wote wakristu. makatibu wa mikoa na wenyeviti wengi wakristu. hakuona aibu kuendeleza udini.
SIPENDE HISIA HIZI ZA UDINI ,ZIKIENDELEA KUKUA KATIKA JAMII NI HATARI.KILA JAMBO UANZA MOYONI KWA MTU MMOJA AKAMSHAWISHI WA PILI NA WATATU KISHA UKAWA NI MJADALA MKUMBWA MIONGONI MWA WANAJAMII .HUU NI MWANZO WA MGAWANYIKO KIDINI .TUPIGE VITA KUU
 
Huku ni kujifanya mbuni. Kwamba hatuuoni ukweli ulio mbele yetu!

Lets say Kikwete angemteua Salim kuwa PM, angepitishwa bungeni?

Kama jibu ni ndio, basi sisi ni wakweli!

Kama ni No, sisi tunajitia umbuni kuzamisha kichwa ndani ya mchanga na kuacha uhalisia wa mambo.

Suala la kuangalia dini lipo wazee hapa Tz labda tuseme tu kwamba hii mada sio sehemu yake.
 
Nungu Nungu
Umesema kweli nenda kwenye kumbukumbu za redio ya mwanakijiji alilaani sana mahakama ya kadhi Tanzania huku yeye si muislam na ni mkristu mwenye elimu ndogo ya Biblia, ona DR Rowan anapigia debe sharia Law ndani ya nchi ya uingereza huyu ni mkuu wa kanisa la ANGLIKANA na ana phd ya dini amekuwa mkweli sio wewe Mnafiki mwanakijiji.

http://news.bbc.co.uk/2/hi/uk_news/7232661.stm

huyu bwana alimlaani sana JK kuchagua mabalozi watano waislam aliandika humu JF kuwa JK ni mdini mbona kigezo cha uwezo hakusema?

juzi juzi ameandika tena kwenye gazeti la Chadema kuwa JK ni mdini kawasaidia mahujaji kwenda Makkah kweli mwanakjj ulikuwa unafurahi kuona raia wenzako 1600 wakisota uwanja wa ndege kwa wiki nzima?
kumbuka watu hawa waliingia mkataba na ndege ya serikali na kama wanafungua kesi ya madai leo hii, basi ATCL inakufa kabisa kwa fidia watakazo chukua.

wameachwa wiki nzima bila chakula wala malazi ukaleta uongo kwenye gazeti kuwa ni mahujaji mia tatu tu huku ukiujua ukweli na ukadanganya kuwa walilishwa na kuhudumiwa na serikali.

Mwanakijiji kama angekuwa shangazi yako kakaa wiki nzima ametoka bunda hana ndugu Dar na hapati huduma yeyote ungefurahi?
kauli zenu kama za wanasiasa kuwa rushwa na uchawi kwao ni mwiko huku wakila rushwa na kushinda kwa waganga. huko si kumdanganya mtu bali mnajidanganya wenyewe.

Es pitia michango yako alipoteuliwa mkuu wa usalama Muislam ulilalama kama Mbwa.
 
SIPENDE HISIA HIZI ZA UDINI ,ZIKIENDELEA KUKUA KATIKA JAMII NI HATARI.KILA JAMBO UANZA MOYONI KWA MTU MMOJA AKAMSHAWISHI WA PILI NA WATATU KISHA UKAWA NI MJADALA MKUMBWA MIONGONI MWA WANAJAMII .HUU NI MWANZO WA MGAWANYIKO KIDINI .TUPIGE VITA KUU
if that is the case.
mbona mliipiga vita OIC?
na mwanakjjj kapiga vita kubwa kwenye podomatic yake.
unafiki na uongo.
 
JK haangalii DINI ktk mtazamo wa Members wa JF akina Nungwi na Mtalii na wengine. JK anajitahidi aweke Timu ya Kuikomboa nchi ktk DIMBI la DHULMA na UMASKINI lkn kazungukwa na Hapindui..ndo maana JF members wana siku ya 3-4 hadi sasa wameshindwa kupanga Baraza la Mawaziri wa KUFIKIRIKA.

Huyo JK hata muda wa kuswali hana, Wakati anafanya ziara za WIZARA nilishangaa kuona ratiba hadi IJumaa ipo.So JK yeye kaka yeye mambo ya DINI hana. ila si kwamba anadharau anayajua Fika na kama mtanzania mwingine amekuwa akiyaangalia kwa umakini. FIKIRIA JK angechagua Mwislam Mtendaji ktk nafasi ya PM nani Angemwelewa? vita dhidi yake ingekuwa kubwa...the so called Utendaji ungewekwa Kando.

Hakuna MTZ ambaye anapenda nchi yetu ikae ktk DIMBWI la Umaskini, lkn pia HAKUNA ambae anapenda nch yetu itokee siku iwe kama Kenya au Burundi. Leo wapo Waislam ambao wanakwenda UK kuishi lkn watawala wake wote wakristo,UK wanajitahidi kuleta Maisha bora na HAKI, pia Wapo watu wanakwenda Dubai kufanya biashara n kazi pamoja na kwamba viongozi wake waislam..lkn wanaangalia HAKI na Maisha bora kwa Wakazi na Wageni...nimetoa nchi 2 zenye mwelekeo wa DINI tofauti lkn wao wanangalia nini ktk TAWALA zao.
 
Lets say Kikwete angemteua Salim kuwa PM, angepitishwa bungeni?

Mkuu Nungunungu,

I am not sure na huu mjadala, lakini Salim si alishawahi kuwa PM huko nyuma, sasa kwa mantiki yako hii alipitaje bungeni?
 
hoja za kidini ktk siasa mara nyingi udhihirisha jambo moja! nalo ni ufukara wa kimawazo na hoja.
natamani wazungu na waarabu wasingetuletea balaa lao hili la dini za kikoloni.
tabia ya kuingiza dini ktk siasa pia ni UFISADI, I hate it!!!. wadini dini wooooooote, mshindwe, mlegee na aibu nyingi ziwafike!!.
 
hoja za kidini ktk siasa mara nyingi udhihirisha jambo moja! nalo ni ufukara wa kimawazo na hoja.
natamani wazungu na waarabu wasingetuletea balaa lao hili la dini za kikoloni.
tabia ya kuingiza dini ktk siasa pia ni UFISADI, I hate it!!!. wadini dini wooooooote, mshindwe, mlegee na aibu nyingi ziwafike!!.
Kati ya point zote zilizotolewa..MI NAIFAGILIA HII!Ni ukweli usiopingika kwamba dini zililetwa Africa na waarabu na wazungu ili kutupumbaza na kututawala vyema..wameitumia kama ni manipulative tool kuwasaidia kututawala!Nilkuwa nikiheshimu uamuzi wa Kingunge wa kutumia katiba wakati wa kuapishwa..sema sikubaliani na uprimitive wake!
At the same time mimi nilzaliwa na wazazi ambao ni wakristo..sidharau dini hata mara moja!I also believe in one God!Lakini historia ya dini hizi mbili imejengwa kwenye misingi ya kujaribu kuifanya moja kuwa superior zaidi ya nyingine..na kudemonize each others!
Pointi yangu sasa ni kuwa..lazima tusimamie uafrika wetu,mara zote ninapoongea na familia yangu huwa nawaambia dini tumeletewa lakini maajabu zinatugawanya!Tumegawanywa vya kutosha jamani!
Tatizo ni kwamba hatuwezi kupuuzia mjadala wa dini pale tunapojadili mambo ya siasa na mistakabali a nchi yetu!Hii ni kwasababu imeshatokea mara nyingi watu kupuuzia dini za watu wengine licha ya kwamba ni watu wenye elimu za kutosha!
Kighoma Malima(mungu amlaze pema) ni mfano hai!The guy was well educated with leadership qualities..lakini alitaka kuipeleka nchi yetu mahali pabaya na ni wazi kuwa alikuwa mdini!Ni muhimu tuchague viongozi lakini baada ya uchunguzi na uchambuzi yakinifu kwasababu sio wote ambao ni noble when it comes to that issue!Na kuna wengine wanatumia dini zao kama turufu..kwamba kwasababu mimi ni mkristo ama mslam mwenzako so mambo poa!Hiyo haifai!MASLAHI YA NCHI KWANZA THEN MSIKITINI ANU KANISANI!
 
Field marshall Es,
lakini Salim si alishawahi kuwa PM huko nyuma, sasa kwa mantiki yako hii alipitaje bungeni?
Yes kweli aliwahi kuwa PM tena kipindi cha Mwinyi ingawa hakukaa muda mrefu, Lakini kama alivyouliza mshirika ... tunamjibu hivi Yes, Salim alipitishwa Bungeni...
 
Kati ya point zote zilizotolewa..MI NAIFAGILIA HII!Ni ukweli usiopingika kwamba dini zililetwa Africa na waarabu na wazungu ili kutupumbaza na kututawala vyema..wameitumia kama ni manipulative tool kuwasaidia kututawala!Nilkuwa nikiheshimu uamuzi wa Kingunge wa kutumia katiba wakati wa kuapishwa..sema sikubaliani na uprimitive wake!
At the same time mimi nilzaliwa na wazazi ambao ni wakristo..sidharau dini hata mara moja!I also believe in one God!Lakini historia ya dini hizi mbili imejengwa kwenye misingi ya kujaribu kuifanya moja kuwa superior zaidi ya nyingine..na kudemonize each others!
Pointi yangu sasa ni kuwa..lazima tusimamie uafrika wetu,mara zote ninapoongea na familia yangu huwa nawaambia dini tumeletewa lakini maajabu zinatugawanya!Tumegawanywa vya kutosha jamani!
Tatizo ni kwamba hatuwezi kupuuzia mjadala wa dini pale tunapojadili mambo ya siasa na mistakabali a nchi yetu!Hii ni kwasababu imeshatokea mara nyingi watu kupuuzia dini za watu wengine licha ya kwamba ni watu wenye elimu za kutosha!
Kighoma Malima(mungu amlaze pema) ni mfano hai!The guy was well educated with leadership qualities..lakini alitaka kuipeleka nchi yetu mahali pabaya na ni wazi kuwa alikuwa mdini!Ni muhimu tuchague viongozi lakini baada ya uchunguzi na uchambuzi yakinifu kwasababu sio wote ambao ni noble when it comes to that issue!Na kuna wengine wanatumia dini zao kama turufu..kwamba kwasababu mimi ni mkristo ama mslam mwenzako so mambo poa!Hiyo haifai!MASLAHI YA NCHI KWANZA THEN MSIKITINI ANU KANISANI!

Mushi...umeongelea vema kuhusu UDINI, lkn nafsi yako ikakusuta UDINI wa nafsini mwako kumponda Marehem Malima eti ALIKUWA MDINI. Uonavyo wewe na wengine mtu akitetea UISLAM wake ni MDINI, ila mwingine akiipa fursa kubwa wakristo wenzake si MDINI..please MAKENGEZA punguza. Marehem Malima alikuwa mtetezi wa HAKI. Hakumuoneo Mkristo yoyote, kama unae Mkristo ambae alidhulumiwa au hata kutukanwa na Marehem Malima mwambie aje JF alete ushahidi.sisemi alikuwa Malaika, lkn ktk Suala la DINI yeye ndie aliekuja kufichua UOVU wa KANISA ktk Serikali na ndio mushi na wenzako mnamchukia...mlikuwa mkitaka Keki ya UHURU mle peke yenu...

Muslim hawataki Upendeleo, wanachotaka HAKI itendeke
.
 
Ila wana JF, mimi ningeshauri wafuatao wasinuse kama sio kuwekwa kwenye baraza la mawaziri, ila maoni yanakaribishwa:

Zakia Meghji - Huyu mama hana elimu ya kutosha kushikilia wizara ya fedha, labda akawe waziri wa wanawake, jinsia na watoto. Wizara ya fedha inatakiwa kushikiliwa na mtaalamu wa maswala ya fedha ili uzembe kama ule wa kudanganywa na BOT eti mpaka akasign document feki, usiwepo tena. Pia mtu ambaye akishtuliwa na waandishi wa habari kuongelea maswala ya kiuchumi aweze japo kuongea neno sio kukurupuka na kuongea vituko kama alivyowahi kuongea. Mfano wa sababu ya kuongezwa kodi katika petrol na mengineyo.

Chenge: Huyu mheshimiwa alihusika sana katika mikataba ya miaka hiyo. Na hivyo, hata hii mikataba feki ya madini inayovurumishwa na wadau wazalendo, alikuwemo. Pia anaonekana anatetea sana ufisadi kiasi kuwa kwenye mada nyingi kama hizo huwa anaonekana kutetea kwa kuongea pumba bungeni. Mfano kwenye kashfa ya Buzwagi na hata kwenye kashfa ya Richmond alipoonyesha kutoipa kipaumbele kiasi cha kutaka kujadiliwa kwa mada nyingine instead ya issue sensitive kama hiyo. Kwa kweli ningekuwa mbunge ningemzomea kule kule bungeni hata kama kanuni zinakataza.

Mramba: Naomba nisiongee, nahisi mnaelewa. Ila kwa ufupi, huyu ni one of the vipanga katika serikali although nashindwa kuelewa kwa nini hatumii vizuri ukipanga wake. Ni msomi but ananiuzi pale anapojichanganya kiasi cha kuhusishwa na tuhuma mbali mbali za ubadhirifu. Hivyo, hapa nitaomba maoni ya wadau, kama abaki kwenye list ya uwaziri au ang'oke.

Mungai: Huyu nahisi kama inawezekana, hata bungeni asikanyage. Huyu jamaa katuingiza kwenye hasara nyingi sana, mojawapo ikiwa ni ile ya kufuta masomo ya biashara, ufundi na kilimo. Hakutumia kama sio akili basi hekima katika kufanya maamuzi hayo. Na cha kuchekesha, viongozi wakubwa wa nchi akiwemo Rais na Waziri Mkuu hawaku-question hilo swala. Taasisi mbali mbali za kihasibu, kiufundi na kilimo zilihoji hili swala but mheshimiwa akaziba masikio na kuendelea na libeneke hilo. Sasa hivi tunaingia gharama ya kurudisha hayo masomo as kuna shule zilishuka status n.k.

Batilda Buriani: Huyu mama sijui binti, alishiriki kwa kiasi kikubwa kutetea kashfa za EPA na Buzwagi pale zilipoletwa na wapinzani bungeni. Alikuwa akitumia nguvu nyingi sana kupinga na kuponda wapinzani. Na alitumia nguvu kubwa katika kumg'oa Sir. Zitto Kabwe bungeni. Please, maoni zaidi, nafikiri wengine mnamfahamu more than me.

Wana JF, naomba maoni na pia mnakaribishwa kuongeza list.
 
Mh jamaa kama atafuata uchama ameharibu maana kwenye chama sijui atamchukua nani ambaye hakushika Wizara nakuborongoa totally... Achqague na Mawaziri wengine kutoka upinzani bwana hii selikali ni yetu wootee na Wapinzani nao ni Watanzania please mpeni Wizara Kabwe jamani
 
Back
Top Bottom