Tumsaidie JK kupanga baraza jipya la mawaziri na "kusafisha UVUNDO" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumsaidie JK kupanga baraza jipya la mawaziri na "kusafisha UVUNDO"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Katibu Tarafa, Feb 8, 2008.

 1. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Napenda kutoa changamota kwa wana JF tusaidie huyu msanii kupanga upya kijiwe chake kipya kwa kupendekeza majina na nafasi ya uwaziri.
   
 2. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tumeshapata jina la Waziri mkuu,ndugu mizengwe pinda,hii inanipa picha kuhusu baraza jipya linalokuja huwenda mawaziri waliopita wakabadilishwa wizara kutoka moija kwenda nyingine.
   
 3. mwanamama

  mwanamama Member

  #3
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I hope hatotumia mawaziri wa zamani tena jamani. Kwani Tz hakuna wataalamu wanaojua wanachokifanya? Vyuo vya Tz vimejaa watu wana PHD zao wasomi, mawizara yamejaa watu waliosoma wanaoipenda nchi yetu, wanaojua unyama wa wazungu ni nini, kwa nini tu wasipewe fursa na wao wakaendesha hii nchi! kwani ni lazima wawe na majina tuliyozoea kuyasikia tangu uhuru wa Tanganyika? Hebu aanze upya, na watu wapya kabisa wasiokuwa na ties zozote, ili tuone sasa haya malalamiko yetu yatachukuliwaje na utendaji wao wa kazi utakuwaje.Lakini akirudi kuchanganya tu the same people kuwahamisha kutoka wizara moja kwenda nyingine, mambo ni yale yale tu hakuna litakalobadilika kwa kweli.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Feb 8, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Angalia uzalendo wa mtu siyo madigrii yake; Professor Malima alikuwa na Ph.D. bila uzalendo. Sokoine alikuwa na uzalendo bila Ph.D. Je, ni nani kato yao alitufaa zaidi?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Feb 8, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Basi tufanye hivi katika kupata mawazo hayo:

  To assume kuwa Baraza linapunguzwa na kuwa na wizara 21 au 22 (toka 30)

  Makundi Matatu:

  NANI ATOKE: (Watakaoungana na walioujiuzulu)
  - Lowassa
  - Karamagi
  - Msabaha
  -

  NANI ARUDI (Anayeungana na Pinda) NA WIZARA
  - Pinda

  NANI AINGIE: (Sura mpya) NA WIZARA
  -
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  JK atutafutie waziri wa fedha wa maana, hiyo wizara ikiwa na mtu fake, hakuna maendeleo. Pesa zitapotea kama zile bilioni za JK lakini hakuna kitakachofanyika.

  Hivi katika wabunge wetu nani ni kichwa kwenye uchumi wa kisasa? Tunataka innovative ideas, change and creativity kama kachumbari ya maendeleo TZ.

  Naangalia hivi nani anaweza kutufaa?

  Chenge mwondoeni ile wizara ya miundo mbinu. Ile ni wizara ya pili kwa umuhimu ukiachia ya fedha, kule kunahitaji watu wanaojua wapi dunia inaelekea na technologies zipi zitatufaa.

  Toka Chenge ameingia, kaiua ile wizara na sasa hakuna la maana linalofanyika zaidi ya kutengeneza barfabara. Je nani anatufaa huko?
  Kama hakuna mtu wamrudishe prof. Mwandosya kwenye hiyo wizara maana angalau yeye alikuwa na ideas and vision for the future.
   
 7. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kutesa kwa zamu!! Gadaymn!!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Feb 8, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  (a) Apunguze ukubwa wa serikali kwa kuunganisha baadhi ya wizara. Waziri yoyote aliyewahi kuwamo serikalini kabla ya 1990 nadhani mchango wake unatosha; aruhusu freshmen nao watumikie.

  (b) Vile vile awaondoe wababaishaji wa elimu wote, wanaleta mfano mbaya kwa watoto wetu:

  1. Mary Nagu
  2. Makongoro Mahanga
  3. Deodorus Kamala
  4. Emmanuel Nchimbi
  5. Dialo Mwandu
  6. Mathayo David

  (c) Vile vile aondoe hawa walioshindwa kutekeleza majukumu yao sawasawa:
  1. Zhakia Meghji <- huyu anaweza kutolewa kwa kigezo cha (a) hapo juu.
  2. Peter Msola
  3. Hawa Ghasia
  4. Andrew Chenge


  (d) Awarudishe bila mkwara jamaa hawa:

  1. Shukuru Kawambwa
  2. Pombe Makufuri
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwenye Wizara ya Fedha namshauri JK amteue kuwa mbunge na kumpa Uwaziri naye ni
  Prof Haidary Amani...........
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Mzee MwanaKijiji,

  Nijuavyo mimi baraza halitabadilishwa sana kwa ajili ya kuhakikisha business inaendelea bila kuwa na muda wa kujifunza ulisiokuwa lazima.


  Mawaziri wengi watarudi kwenye vyeo vyao... isipokuwa wafuatao.NANI ATOKE: (Watakaoungana na walioujiuzulu)
  - Lowassa
  - Karamagi
  - Msabaha
  - Mramba
  - Mungai


  Kutakuwa na mabadiliko kwenye ofisi ya Waziri mkuu kutokana na Vacant created! lakini hata hivyo Mh. Salha Buriana ataendelea kubaki pale pale.

  Ila kuna uwezekana wa kuletwa mchapakazi TAMISEMI, wanaweza kumpeleka naibu waziri wa maji pale, au wa kilimo... kushika nafasi ya Pinda...

  Tutegemee manaibu waziri ku-panda ngazi kujaza nafasi za mawaziri ambao wanaondoka....
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  I don't think that Jk anahitaji msaada wetu wa kupanga mawaziri wake.
  EL atampa list ya cabinet 'mwanafunzi' wake mtiifu aliyefanana naye sana - MP na JK will rubberstamp!
  Wake up and smell the coffee...
  (maybe a few non wanamtandao watawekwa kujaribu kuleta amani ndani ya chama lakini hata wao watakuwa ni akina Mramba tu!)
  Katika field ya Wizara ya fedha, forget it! Hawaweki mtu makini! Hebu niambie huyo bosi mpya wa BoT kafanya nini? Zero, zilch, nada! Nothing! Na ulaji utaendelea tu!
  I am so disappointed after a euphoric Thursday. More of the same!
   
 12. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Kati ya wanaoondoka, nadhani mzee wa wakimbizi mchango wake umetosha sasa. Tumpate mwingine atakayekuwa damu mbichi na mawazo mapya. Mzee wa Usalama wa Raia naye amepoteza uwezo sasa. Hana jipya, awaachie nafazi wengine. Hawa wasirudi. Nadhani hata Kapuya apewe nafasi zaidi ya kusimamia migodi yake kuliko public service.
   
 13. M

  Mr EWA JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2008
  Joined: Mar 15, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Nafikiri hapa JK kapata nafasi ya kupeleka ujumbe kwa wale wote walikuwa wababe na wenyekuyumbisha maamuzi ya serikali.
  Wanaotakiwa kuondoka:
  Mramba -jeuri na yaliyotokea BOT yanatosha kumwondoa.
  Megheji- kudaganywa haitoshi kuvunja uadilifu/kanuni za kazi na kusema hatajiuzulu inatosha kumwondoa.
  Chiligati- kubadilisha kauli za serikali kuhusu mishahara ya wafanyakazi na kusababisha migogoro kazini na kupelekea taifa kupata hasara kutokana na migogoro kazini inatosha kuondoka.
  Wazee sana- michango yao inatosha kwani mawazo mapya yanahitajika.
  Ngasongwa- kwa kauli ya kusema mfumko wa bei unasababishwa na uhaba wa chakula huu ni usanii kwa msomi kutoa kauli hiyo pia aondoke.
  Chenge- kwa ujanja wake wakuacha majukumu yake na kujishughulisha na kutumia ujuzi wake wa sheria kuzuia miswada yenye masilahi ya taifa naye aondoke.
   
 14. m

  mwewe Senior Member

  #14
  Feb 9, 2008
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 125
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  PEKECHA-PEKECHA. Akudo Sound.
   
 15. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  matamanio: jumla ya mawaziri+manaibu isizidi 25.

  hali halisi: watazidi 40. biashara kama kawa.
   
 16. m

  mwewe Senior Member

  #16
  Feb 9, 2008
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 125
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Ngasongwa mtu wa DS. Economic Planning wapi na wapi!

  Wizara za Fedha na Economic Planning ziunganishwe. Wizara ipewe mtu mwenye uelewa wa masuala haya. why not go for Prof. Wangwe?
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono maoni yako.
  Mie naongezea hapo katika kipengele (a)kama hivi,
  -Lowassa
  -Karamagi
  -Msabaha (Bangusilo)

  -Msola
  -Mungai
  -Meghji
  -Mramba
  -Mudhihir
  -Mwanyika
  -Mwakyusa
  -Magufuli
  -Marmo
  -Ngasongwa
  -Ghasia
  -Simba
  -Chenge  Kipengele (b) nitachangia hivi,
  -M. Pinda
  -D. Mathayo
  -L. Masha
  -M. Sitta
  -M. Mwandosya
  -L. Selelii
  -M. Mahanga
  -S. Mwangunga
  Nakuunga mkono kwa listi (d), ila Pombe bado namdai chenji ya mauzo ya nyumba zetu walipa kodi, bado nina shaka naye sana. Zile nyumba zangu bado zinaniuma, je akipewa wizara ya "mihogo" si atauza mbolea za ruzuku huyu?
   
 18. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Lazima tupate Mabilionea 100 ifikapo 2015, kwa sasa tumeshapata karibu 20 kupitia siasa, bado 80.

  Mwakyusa arudishwe aendeleze kazi ya kuirekebisha wizara ya Afya. apunguze upole. Wizara ziunganishwe.

  Natabiri Manaibu wengi kuwa mawaziri kamili
   
 19. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na wewe kuhusu kuwepo kwa Mwakyusa katika baraza jipya (ingawa sina mamlaka ya kuzuia uwepo wake). Nasema hivyo kwa sababu huyu ilitakiwa ajiuzulu wakati wale madaktari walipochanganya wagonjwa na kufanya upasuaji tata! Katika serikali ya utawala bora ilitakiwa ajiuzulu ili kuonesha kuwajibika.
   
 20. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe Idimi kuhusu Mwakyusa hakujiuzulu wakati ule. Lakini bado namuona ni mtu asiye na kashfa na siyo mpenda ubilionea among the rest tulionao. ni suala la yeye kubadilika sasa na kuwajibika ipasavyo.

  Nashauri pia JK aache ule utaratibu aliotumia wakati ule wa kuchomoa mawaziri kutoka kila mkoa. utaratibu huu haukuwa na manufaa yoyote kwa taifa zaidi ya kuingiza Mafisadi wengi serikalini. hatuitaji political balance, tunataka maendeleo that's all
   
Loading...