Tumpongeze Kikwete kuweka mbele maslahi ya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumpongeze Kikwete kuweka mbele maslahi ya taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzambia, Jan 6, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Send to a friend
  [​IMG] Rais Jakaya Mrisho Kikwete

  Wakati Rais Jakaya Kikwete akiendelea kupongezwa na wananchi wengi katika kila kona ya nchi yetu kutokana na uamuzi wa kijasiri wa serikali yake kukubali kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya, baadhi ya viongozi na makada katika chama chake wameghadhabishwa na hatua hiyo.

  Akilihutubia taifa kwa njia ya redio na televisheni wakati wa kuaga mwaka 2010 na kukaribisha mwaka mpya, Rais Kikwete alisema kuwa angeunda Tume Maalumu ya Katiba itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea ambayo itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali.
  Alisema kuwa jukumu la msingi la tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua.

  Tunadhani kuwa sio jambo la ajabu kwa baadhi ya watu ndani ya chama ambacho kimekuwa madarakani zaidi ya miongo minne kupinga mabadiliko ambayo wanadhani yatawapunguzia maslahi yao kwa namna moja ama nyingine.
  Itakumbukwa kuwa huko Zanzibar, Julai 31, 2010 ilipopigwa kura ya maoni kuhusu kuundwa ama kutoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, zaidi ya Wazanzibari asilimia 33 walikataa kuundwa kwa serikali hiyo, na iligundulika kuwa waliosema hapana ni wale waliokuwa wanafaidika na mitafaruku iliyokuwapo kati ya vyama hasidi vya Cuf na CCM. Kwa kuwa katiba iliyokuwapo ilikuwa inakifaidisha CCM Visiwani, baadhi ya makada na viongozi wa chama hicho hawakutaka kuwapo maridhiano na ndio maana walipiga kura za hapana.

  Hivyo, ghadhabu za makada na viongozi hao wa CCM zinatokana na hali hiyo, kwamba wangefurahi katiba iliyotungwa wakati wa chama kimoja iendelee kutumika katika mfumo wa siasa za vyama vingi ili chama chao kiendelee kubaki madarakani milele kwa maslahi yao tu.
  Ndio maana tunadhani Rais Kikwete hakutaka kupeleka hoja hiyo katika vikao vya chama chake kwani aliamini vingemkwamisha kutokana na kuwapo makada na viongozi mahafidhina, baadhi yao wakiwa wanakabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi, ambao hawataki mabadiliko.

  Ni kutokana na hali hiyo tunalazimika kumpongeza tena Rais Kikwete kwa ujasiri wake huo wa kutanguliza mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi ya vyama. Rais Kikwete ameona mbali, kwani sauti za mwangwi za kutaka katiba iandikwe upya zilizokuwa zinatoka katika vinywa vya wananchi wengi zilimfanya asome alama za nyakati na kukubali matakwa yao, hata kama suala hilo nyeti na muhimu lilipingwa na wahafidhina, hivyo halikuwamo katika Ilani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

  Rai yetu kwa viongozi wa vyama vya siasa, madhehebu ya dini, vyama vya wanaharakati na wengine ni kwamba wamuunge mkono Rais Kikwete ili mchakato wa kupata katiba mpya ufanikiwe na hatimaye nchi yetu ipate katiba mpya yenye kukidhi matakwa ya wananchi wote. Tungeomba pia wananchi tuwe wavumilivu wakati Rais Kikwete akiunda tume hiyo maalumu ya Katiba na kutayarisha adidu za rejea, kwani tukiendekeza ushabiki na maneno makali tutakuwa tunawafaidisha wahafidhina ambao hawataki katiba mpya.

  Ni imani yetu kuwa Rais Kikwete atasimama kidete hadi katiba mpya ipatikane na tungeshauri katiba hiyo iwepo mezani ndani ya miaka mitatu kuanzia sasa, ili iwe imeanza kutumika kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Ni imani yetu pia kuwa tume itakayoteuliwa itakuwa huru kweli na Rais Kikwete hataweka mkono wake katika utendaji wa tume hiyo ambayo itapaswa kufanya kazi kwa uwazi na ukweli.

  Kwa kuona uzito wa mchakato huo wa kuandika katiba mpya, Rais amesema atamteua mwanasheria atakayeongoza tume hiyo. Ili mtaalamu huyo asikwazwe, tunamshauri Rais asiwateue kuingia kwenye tume hiyo wanasiasa au viongozi wa Serikali waliokuwa wanapinga waziwazi kuandikwa kwa katiba mpya. Ni jambo jema kuwa Rais amesisitiza kuwa wananchi wote wahusishwe bila ubaguzi. Nasi pia tunadhani ni kwa njia hiyo tutaweza kupata katiba ya watu wote kwa maslahi ya taifa letu.
   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Joto ya jiwe ndo imemfanya kukubali yaishe.
  Sasa tumpongeze nini?
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ila jamani anapostahili sifa na apewe sifa siyo kila kitu kulaumu tu.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mzambia acha kujipendekeza kwa JK, kwa mtazamo wako JK ataunda tume ya aina gani kuhusu suala la katiba?
  Watanzania tunataka tume huru ya uchaguzi ambalo litashirikisha watu mbalimbali ikiwashirikisha vyama vya siasa.
  Tunasema hatutaki tume itakayoundwa na huyu MKWERE.
   
 5. Supervisor

  Supervisor JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 553
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mpongeze ww na wa.s.nge. Wenzio. Unapoteza muda ku post upupu. Huyu vp?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  correction
   
 7. L

  Lorah JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwambieni kama anatubeep tutampigia sisi sio wale watanzania wa zamani kwamba watabandika bandika vi technique vyao tusisome, Mwambie hatumuamini tunajua ni muongo, mwizi na mnafiki maana anataka kutuchezea akili tu huyu hakuna kitu....
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  The known propensity of a democracy is to licentiousness which the ambitious call, and the ignorant believe to be liberty.

   
 9. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :hat:
  I will do it a day of his burial.....tonterĂ­as
   
 10. w

  warea JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As long as brutality continues and our people die from oppression under CCM, I will not say congrats to them
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu alisema Kikwete ni maafa kwa Tanzania.......sikumbuki ni nani alisema usemi huu
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kikwete is not a LEADER, but a RULER
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  surely misplaced optimism can lead to a state of delusion
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Unajipendekeza tu wewe.
   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SASA aMEAMUA KUACHIA MAUAJI NA MATESO KULE ARUSHA HUYU SIO KIONGOZI WETU NI KIONGOZI WAO MAFISADI NA RAFIKI ZAKE
   
 16. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umepatia, hatabiriki yu upande upi huyu kiumbe.
   
 17. G

  Gurti JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii hoja ya kumpongeza kikwete isiletwa wakati tunajadili habari ya msiba wa vifo vya watu zaidi ya kumi Arusha iliyosababishwa na Kikwete. Ni uhakika kuwa Slaa na Mbowe - kiongozi wa kambi yaupinzani hawawezi kukamatwa na IGP bila kikwete na usalama kuhusika. Na haya ndo yameleta maafa Arusha.
  Pili Kikwete anaunda Tume feki kama alivyofanya wakati wa Buzwagi + Zitto. Anateka hoja ya wananchi ili watulie wakati yeye anajipanga jinsi ya kukwepa.
  Tatu, Kikwete ametoa hotuba ile bila kushirikisha Ccm, wala baraza la mawaziri. Je ametoa maoni yake binafsi? Huu ni uhuni. Urais si kuongea tu bila kushirikisha watu wanohusika. Urais ni taasisi na rais ni mkiti. Mkiti lazima ashrikishe wajumbe halali. Vinginevyo, Kikwete ameturushia changa la macho.
  Mwisho hakusema katiba yake iliyohuishwa ( kwa maneno yake) itaanza kutumika lini. Pengine 2020?. Naamini alipunguza presha tu ili tutulie.
  Thanks
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kama nina allergy vile
   
 19. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu UMEPOTEA NJIA hapa si sehemu ya KUPONGEZA huyu jamaa.

  Alikuwa wapi kuanzisha mchakato huu yeye binafsi?
  Kasubiri watu wazima CDM waanzishe halafu eti apongezwe yeye uliona wapi?

  Huyu jamaa hakuwa na pa kutokea, sasa kabanwa ndani kwa ndani imebidi atubu aombe msaada kwa janja ya PANYA.

  SISI WANANCHI NDIO TUPONGEZWE KWA KUANZISHA JOTO HILI NA KULIPANDISHA HADI hadi kufikia hatua ya huyu jamaa kukubali yaishe.

  Sasa tunaisubiri tuione hiyo tume itakuwa na watu wa aina gani, TUNAFUATILIA KWA KINA.

  WASALAAM
   
 20. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tanzania haina demokrasi kwa hiyo hakuna masilahi kitaifa yaliyowekwa mbele.
   
Loading...