Tumpe pole Mheshimiwa JK, tumwombe aachie urais hana cha kupoteza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumpe pole Mheshimiwa JK, tumwombe aachie urais hana cha kupoteza

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Watanzania, Aug 23, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binadamu wenye ubinadamu tunasikitika sana na kumpa pole JK kwa kuanguka jukwaani akiwa kwenye kazi za chama. Tunamtakia afya njema rais. Hali hii imemtokea JK mara nyingi akiwa kwenye kazi za siasa. Tunaona uhusiano wa kazi anazofanya sasa za kisiasa na kuanguka kwake. Tunaona ni jambo la busara kwa JK kuacha siasa za jukwaani kabisa kwa vile afya na uzima ni muhimu zaidi kuliko madaraka au mali. Tunaomba JK aache siasa ili atunze afya yake. Akifanya hilo hana cha kupoteza bali ataitunza afya yake kwa manufaa yake, familia yake n.k. Hana cha kupoteza kwa vile atatunza heshima kwa kukubaliana na hali ya afya yake. Hana cha kupoteza kwa sababu atawaacha watanzania katika mikono salama ya urais wa Dr. Slaa. Na atakuwa ameacha historia ya pekee kwa kuacha demokrasia ichukue mkondo wake kwa kukubali chama mbadala cha Chadema kuongoza Tanzania.
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi inawezekana kumpinga mahakamani kwamba asigombee Urais kutokana na hali yake ya afya? Mtikila yuko wapi Jamani? Kama kuna mwenye contact za Mtikila aniPM. Nafikiri kuna haja ya kwenda mahakamani kupinga JK kugombea Urais kwa kuwa kuna ushahidi tosha kwamba afya yake ni mgogoro. Asije siku nyingine akaanguka kwenye mkutano wa UN ikawa ni changamoto kwa Taifa.
   
 3. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo lazima kufanya hivyo. Ni kumuomba apime uzito wa kutunza afya yake. Hali inaonyesha kuwa kazi za siasa zinamharibia afya yake. Yeye ni mtu mzima, tukimwomba watanzania ataacha urais kwa hiari yake.
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Lukolo Ndeti???
  Huna habari kuwa kuna kesi tayari mahakamani ya kumzuia kugombea urais iliyofunguliwa na mtanzania mmoja mwalimu nani sijui, kwa hiyo kwa kesi kama hii sio mtikila mtafute huyo mwalimu ambaye ameshamfungulia kesi ya kumzuia kwa sababu za kutumia vibaya pesa za umma akiwa rais kipindi cha kwanza.
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ======
  Mimi nadhani kuna kifungu cha katiba kinachomtaka Rais awe na afya nzuri kiakili (Mental health). Huku kuzimika zimika ni aina fulani ya magonjwa ya akili, yaani kunagusa mental part of him ndiyo maana kuna wanaosema ana shida ya nerve fulani katika nerves za fahamu.
  Kwa maana hiyo, capacity yake ya kufanya kazi iko limited (no offense intended please). Ama kwa njia ya mahakama au heskima, zinahitajika juhudi za kufanya kitu fulani kuokoa afya yake na ya taifa. Anaweza kesho na keshokutwa akapitisha maamuzi fulani yakakataliwa kwa kutumia ushahidi huu wa kuzimia zimia.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Be mdimi Mbogela, hiyo kesi ya huyo Mwalimu ni tofauti na hii. Kwa hiyo kama watu kadhaa watafungua kesi ya kumpinga kwa sababu tofauti tofauti, naamini hata mahakama itazipa uzito hizo kesi. Kwanza yule Mwalimu mbona nasikia kesi aliyofungua imefutwa kwa kukosa ushahidi? sasa hii tuna ushahidi kabisa kwamba ameanguka mara tatu tena mbele ya hadhira. Hatujua ameanguka mara ngapi akiwa Ikulu au safarini huko nje ya nchi anakokwenda kila siku. Kwa hiyo hii kesi itakuwa na nguvu ukilinganisha na ile ya Mwalimu.
  Kwanza ashauriwe aachie ngazi, na iwapo hatataka kufanya hivyo basi aweke pingamizi mahakamani.
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Kama kweli watanzania na wana - CCM wanampenda sana basi ni busara kumpumzisha kwa kutomchagua - la sivyo yale ya Nigeria yatatukuta hapa TZ in the near future!
   
 8. m

  mapambano JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaota mchana....Dr Slaa na CHADEMA wataingia Ikulu kwa nguvu na jitihada zao sio kutegemea kuachiwa, that is not true democracy..afterall Kikwete is not the only person that can lead CCM
   
 9. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiyo ya mwalimu imeshakataliwa na mwendesha mashitaka
   
 10. L

  Luiza Gama Senior Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa nae kudondoka kama kawa.
   
 11. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunajua watu wanafaidika na urais wa JK. Lakini ni vizuri wawe na ubinadamu, wasimtumie bila huruma kwa tamaa za mali hadi iwe kama Michel Jackson ambaye alitumika na watu bila kujali afya yake hadi akapoteza uhai wake.
   
Loading...