Tumombee Ammaar- Mtanzania Mwenzetu Kwenye Mashindano Ya Olympic Kesho Tare 31.7.2012 Ashinde | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumombee Ammaar- Mtanzania Mwenzetu Kwenye Mashindano Ya Olympic Kesho Tare 31.7.2012 Ashinde

Discussion in 'Sports' started by Ndallo, Jul 30, 2012.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Ammaar Ghadiyali will be swimming on Tuesday 31st July at 10am London time.The Dar time will be 12 in the afternoon.

  MAIL RECEIVED FROM AMMAAR:  Dear All

  I visited the Olympic village yesterday where all the atheletes are residing. Atheletes were given an opportunity to hold one of the actual "Olympic Torch" at the main center of the village where the symbol of olympic - 5 rings are erected.


  Here are some pictures...…..
  Ammar 1.png
  Ammar and his Father Shabbir Ghadiyali at Olympic Village in London 2012.

  Ammaar 2.png  Ammar 4.png
   
 2. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Ammaaar tuko nyuma yako tunajua ni juhudi binafsi zimekufikisha hapo na tunaamini umedhamiria kutufuta machozi kwa kutokuwa na medali miaka zaidi ya 30 .Mungu akutangulie na sisi tuko nyuma yako.
   
 3. w

  wasasa Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  kila la kheri.
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nimtakie kila la kheri
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  All the best mkuu!
   
 6. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Kila la kheri kijana ni lazima ututoe kimasomaso.

  Kama wafahamu wenzio wataingia kwa dharau sana wakiona kijana wetu unataka kuweka record lakini usibabaishwe wewe uwe focused na free style yako.

  Nikupe story kidogo mwaka 2000 kule Sydney kulikuwa na kijana mmoja kutoka Equtorial Guinea anaitwa Eric Moussambasi. Aliteka mawazo ya vyombo mbalimbali vya habari duniani kwa mtindo wake wa kuogelea polepole na ikawa inadhaniwa kuwa asingeweza kumaliza mchezo alipokuwa akitumia hiyo free style yake.

  Yeye katika hizo mita 100 alitumia dakika 1 na sekunde 52:72 kumaliza na hata kuwashinda wale wa mita 200. Eric aliingia kwenye timu ya kuogelea kwa mfumo wa wildcard baada ya waogeleaji wawili kutolewa kushiriki mashindano hayo kutokana na kushindwa kufikia viwango.

  Eric hakuwahi kutumia pool la kuogelea na alijifunza muda usiozidi mwaka mmoja akitumia pool ya hotelini alikokuwa amepangiwa na serikali.

  Lakini juhudi, bidii na maarifa vilimfanya aweze kumaliza kuogelea na kuwa gumzo kwa watazamaji. Bila shaka wewe umejiandaa vya kutosha na umetumua pools za aina nyingi tu na labda mzee wako amekusaidia vya kutosha.

  Kwahio kijana jitahidi sisi tunasubiri juhudi zako kesho, Mungu akubariki, Amen
   
Loading...