Tumlaumu Nani Kati ya Serikali, Madaktari na Wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumlaumu Nani Kati ya Serikali, Madaktari na Wabunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Masulupwete, Mar 7, 2012.

 1. Masulupwete

  Masulupwete JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 655
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Serikali ilionekana kuridhia kirahisi sana mapendekzo ya waheshimiwa kuongezewa posho pale mjengoni. Bila shaka waheshimiwa walifanya hivyo wakiamini hakuna atayeleta 'zengwe' pengine wakiamini kwa kuwa wao ndo kila kitu. Madaktari wamewaprove wrong! Kwani waheshimiwa si binadamu nao? na wao si wanahudhuria hospitali kama binadamu wengine?

  Ombi la madaktari limeleta shubiri kwa serikali na kwa wananchi kwa ujumla. Nakumbuka kuna wadau walitoa hadhari juu ya hatua ya serikali kukubali maombi ya waheshimiwa kuwa ingechochea makundi mengine kudai maslahi yao pia. Serikali haikuwa tayari kusikiliza ndoto hizi.

  Na sasa hali ndo hiyo, jamaa wanakusudia kurejea kwenye mgomo kwa mara nyingine tena...hivi kwa hali hii ni nani wa kulaumiwa....Serikali, Madaktari au Waheshimiwa?
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  safari nataka nione kiburi cha JK kupuuzia maazimio yanayotolewa kitaishia wapi? amekuwa nakawaida ya kupuuza bunge lake na akafikiri madaktari nao watanywea.lets wait and see!
   
Loading...