Tumkumbushe Kadinali Pengo juu ya hili

Septem

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
313
403
Maaskofu mwezi machi walitoa waraka ukielezea mambo kadhaa juu ya nchi yetu katika awamu ya 5 ya Uongozi/Utawala. Waraka wenyewe umeonya mambo kadhaa juu haki za kiraia na kisiasa, unaweza usoma hapa (WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini). Siku chache kadhaa Kadinali Pengo alitoa 'maoni' yake huku akiukana waraka huo, na kwenda mbali kuonya kuwa 'maaskofu' wamechanganya dini na siasa. hili binafsi lilinistua. kwani kwa uelewa wangu 'mdogo'- dola ya kirumi na hadi leo 'chapel'-haijawahi 'kumpa kaisari ya kaisari'.

Tumkumbushe tu dogo hili.

Hii ni ilani ya uchaguzi ya 'maaskofu' ya 2010. Baadhi ya vipengele ni hivi.
"Dira
Uchumi ni kwa ajili ya kuhudumia watu ili wawe na maisha mazuri: wapate mahitaji msingi na walindwe dhidi ya hali zinazowakuta na kutishia usalama wao na majanga mengine yanayoadhiri ubora wa maisha. Maadili katika shughuli ya kiuchumi na kuhakikisha mahitaji haya muhimu katika kumpatia mtu maisha mazuri yanapatikana. Sera za kiuchumi ni lazima ziweke kipaumbele kwa kuzingatia maadili na hivyo kufikia manufaa kwa wote na kulinda utu wa kila mmoja. Kwa hiyo tujadili pamoja na kama jumuiya za kanisa ni lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Maoni yetu yasikilizwe na kufanyiwa kazi, tunu za kikristo tunazosimamia zionekane katika sera na katika mgawanyo wa bajeti ya serikali.

- Tunaweza kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa katika nchi yetu ikiwa watu wataelewa wajibu wao na kushiriki katika kutatua matatizo yetu: kwa mfano: kushiriki katika namna ya kupata huduma ya maji vijijini, namna ya kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumwa katika serikali za mitaa.
- Ni kwa njia gani madiwani watafikisha maombi ya watu wao katika mgawanyo wa bajeti ngazi ya wilaya.
- Je, matumizi katika serikali ngazi ya chini yanawekwa wazi kwa wananchi kujua?
- Wabunge na viongozi katika ngazi ya Mkoa wanatoa fursa ya watu kuwauliza na kuwaeleza mahitaji yao? Tunawezaje kuboresha hali hiyo?
- Je, wakristo wetu wanazielewa fursa zilizopo; huduma zinazotolewa na serikali, mipango ya kusaidiana kama SACCOS, MVIWATA, vyama vya ushirika, jitihada za TASAF. Kwa nini wakristo wetu hawafanyi bidii kuanzisha vikundi/mipango ya kusaidiana? Pia parokia zetu ziwajibike vema katika kujenga ushirikiano na kujenga uwajibikaji wa kijumuiya ili kuboresha maisha.
- Kwa nini watu wetu hawaaminiani? Na tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu miongoni mwetu?
- Kwa nini wakristo wetu wanaogopa kuzungumza na wenye mamlaka na walio katika huduma za utawala ili kupeleka malalamiko na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi yaliyofanyika. Pia tutafakari namna ya kupambana na tabia ya uvivu.
- Tuna mali nyingi, lakini kila mara tunasubiri “wengine “ au “Serikali” kufanya kitu au kutuletea fedha. Lazima tujifunze kutumia vipaji vyetu na uwezo wetu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Kusaidiana kwa kuunganisha nguvu zetu na uwezo wetu ni wajibu wa kikristo. Mungu ametupa vipawa, lazima tuvitumie.
- Umaskini wa fikra, umaskini wa utashi duni na uwajibikaji ndio hasa husababisha umaskini. Ni kwa vipi jumuiya ya wakristo wanaweza kuwa mahala pa uwajibikaji ili kuweza kuboresha hali yetu.
 

Attachments

  • aa.jpg
    aa.jpg
    8.5 KB · Views: 25
  • BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA_ ILANI YA UCHAGUZI 2010.pdf
    310.2 KB · Views: 40
Back
Top Bottom