Tumieni jicho la tatu kuiona fursa ya Royal Tour

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
612
1,045
Ikiwa ni wiki ya pili muendelezo ya safari ya Rais Samia katika kurekodi vivutio vya Utalii kwa ajili ya kulitangaza Taifa letu katika mataifa mbalimbali Duniani katika Utalii.

Kalamu yangu iende kwa Gerson Msigwa, Vijana, Wasanii na Vyombo vya habari.

Kwa Msemaji wa Serikali kwanza kabla ya kufungia gazeti la Raia Mwema tungemaliza kuunganisha nguvu pamoja na mheshimiwa Rais katika kutangaza utalii kulipokea hili jambo la Royal Tour kama suala la kitaifa ni Faida kwa wote msemaji wa Serikali huu ungekuwa wimbo wako kama sala ya Asubuhi.

Sisi Vijana watanzania hatujajiandaa kuipokea Fursa hii. Ukitazama faida kubwa zitakazopatikana kwenye Tour hii muhimu unawaza na kujiuliza Vijana wa Tanzania wanakwama wapi kupokea Fursa hizi.

Kwa Vijana ambao wapo katika sekta ya Utalii na walio nje huu ulikuwa ni wakati wa kujiandaa kuitangaza nchi kimataifa juu ya vituo vya utalii vilivyopo nchini.

Royal Tour si kipindi kidogo kama wengi wanavyofikiri ni jambo la kupoteza muda ambalo linafanywa na Rais. Hapana hili ni jukumu zito ambalo mheshimiwa Rais amelibeba kama alama namba moja ya kuitangaza nchi kimataifa katika kuvutia watalii na wawekezaji katika sekta mbalimbali za Utalii.

Vijana Walitakiwa kutengeneza Tourism Logistics chart ya kueleweka, Season kwa mwaka ziko ngapi, Vivutio vipo vingapi na kijana kuchagua ni wapi anaweza kushika routes na safari za kwenda. Na anajua atapata shingi ngapi kila atakapompokea mgeni ambaye atakuja nchi kwa ajili ya utalii lazima vijana tuwe rasmi na tuunganishe nguvu kwa pamoja katika kuikimbilia fursa inayokuja kwenye Utalii nchini. Rais Samia anafungua Soko huru la Utalii freedom to work.

Unajiamulia mustakabali wa maisha yako kama kijana kwenye Utalii.

Mnyororo wa thamani katika soko la Utalii ni mkubwa umegawanyika katika makundi mbalimbali ni namna gani Vijana wachague katika kujiposition wapi utawekeza au wapi umeona Fursa kwenye Utalii.

Mambo yako wazi kwenye Utalii angalia Rwanda kiwango cha Pesa Rais Kagame alichowekeza na nafasi waliyopo sasa kwenye Utalii Afrika.

Rais Samia yupo wazi kwa Vijana kuwa Fursa hailetwi mikononi bali inatafutwa, show me you can, unapanda chati. Habebwi mtu, habembelezwi mtu, katika kutangaza utalii je Fursa kwenye Utalii hatuzioni mambo yako wazi sanaa. kwenye biashara ya utalii vijana hatuwezi kuipotezea kirahisi rahisi tu. Tayari Rais amefungua milango ya kutangaza utalii je tumsubirie Msemaji wa Serikali atufungulie Fursa...?

Si kwa Vijana tu Vyombo vya habari kuanzia TV, Radio Na Magazeti Tour hii ingetakiwa kuwapa homa ya kutengeneza nafasi nzuri ya kibiashara na mashirika ya Utalii kutoa punguzo za matangazo pamoja na kutoa zawadi kwa wasikilizaji katika kutangaza vivutio vyetu vya Utalii.

Ningepata nafasi niwakusanye Wasanii wote niwaingize studio kumtia Moyo Rais samia katika Safari yake ya kutangaza utalii nchini. Tusisubiri wakati wa majanga ndiyo tuunge nguvu kutangaza utalii nchini.
 
Huu ushauri ni mkubwa sana kupokelewa ni mtu yoyote anaetawaliwa na inferiority complex
 
Rais katimiza wajibu wake. Serikali imetimiza wajibu wake. Tanzania imewekwa kwenye platform za kimataifa rasmi kuhusu utalii na fursa za uwekezaji.

Sasa lililobaki ni Watanzania kujipanga vizuri kutumia izo fursa. Kuboresha kampuni zao za utalii na ma hoteli hasa kwenye huduma. Na kufanya mambo mengine uliyotasema Mleta mada.

Kwa pamoja Tunaweza.

Tanzania mbele Daima!
 
Kwakweli anaye beza hii kitu anamatatizo kichwani mama kajitolea siyo kitu kirahisi kwa raisi wa nchi kuchukua muda wake mwingi kama hivi kuwaandalia Watanzania vijana kwa wakubwa wafanya biashara wenye makampuni ya utalii wote hawa wanaenda kufaidika na kitu hii hebu tumuunge mkono mama kuliko kubeza juhudi zake tuone tutakavyonufaika

Neno la busara

Tukifanya wana sema
Tusipofanya wanasema
Ni bora tufanye ili hata kama awanasema tuje tuwaonyeshe tulifanya
 
Naunga mkono hoja, Watanzania bado tumelala sana katika suala zima la kuchangamkia fursa, fursa are there to grab, na sio kuletewa kwenye kisahani cha chai!, Watanzania wenzezetu badala ya kuangazia fursa, wanakalia kulia lia na kulalamika shilingi ngapi zinatumika!.

Hivi ni bado mlango wa free labor migration haujafunguka, ukifunguka mtashangaa Wakenya na Waganda watakavyomiminika nchini ku grab all decent jobs!. Sasa Bara zima la Africa linakwenda kwenye AfCFTA, ni free trade kwa bara zima, kama this is the trend, we Tanzania, where do we stand?!

Watanzania lazi tuamke kuangazia fursa, kuchangamkia fursa na ku grab the opportunities!
P
 
Naunga mkono hoja, Watanzania bado tumelala sana katika suala zima la kuchangamkia fursa, fursa are there to grab, na sio kuletewa kwenye kisahani cha chai!, Watanzania wenzezetu badala ya kuangazia fursa, wanakalia kulia lia na kulalamika shilingi ngapi zinatumika!. Hivi ni bado mlango wa free labor migration haujafunguka, ukifunguka mtashangaa Wakenya na Waganda watakavyomiminika nchini ku grab all decent jobs!. Sasa Bara zima la Africa linakwenda kwenye AfCFTA, ni free trade kwa bara zima, kama this is the trend, we Tanzania, where do we stand?!

Watanzania lazi tuamke kuangazia fursa, kuchangamkia fursa na ku grab the opportunities!
P
Unataka kuniambia kuwa Rais wetu ni mtu maarufu sn
 
MOVIE HAITOKAMILIKA KAMA CHATTLE KITOVUNI HAPATAKUWA KWENYE SCRIPT
 
Back
Top Bottom