Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,270
- 40,085
Tuanze na mtaji mdogo tu, labda una shilingi laki 5 na hujui ufanyie shughuli gani; fanya yafuatayo:-
- Nenda sokoni, na utafute wamama watu wazima watano wenye vibanda; ambao ni wapambanaji
- Tathmini utokaji wa biashara zao, kama unaridhisha nenda hatua inayofuata
- Hakikisha hawa wamama hawajuani, ikiwezekana kuwepo na umbali fulani kati ya kibanda cha mama mmoja mpaka mwingine.
- Ingia nao makubaliano, ya wewe kuwekeza kiasi cha laki moja kwa kila mmoja; na ikiwezekana kila jioni uwe unapita kwa ajili ya kupata mgao, baada ya mauzo.
- Ukiona biashara inaenda vizuri na uaminifu uko vizuri; ongeza mtaji.
- Kama inazidi kulipa zaidi, ongeza wamama wengine tena na tena.
- Nenda kwenye masoko mengine tena na tena, wilaya kwa wilaya, mkoa kwa mkoa
- Baada ya mafanikio kuwa mazuri sajili biashara yako kama micro-finance
- Jipigie makofi kwa kuwa CEO aliyejiajiri