Tumia Smartphone yako kuongeza thamani ya maisha yako

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Nini maana ya thamani (value) ya mtu?

Thamani ya mtu ni uwezo alionao katika kutatua matatizo yake binafsi na jamii kwa ujumla , pamoja na uwezo alionao katika swala zima la uzalishaji mali. Kwa mfano kama jamii inakabiliwa na gojwa fulani halafu akatokea mtu akapata tiba ya ugonjwa huo basi mtu huyo atakuwa ameongeza thamani yake katika jamii.

Kwa lugha nyingine , kama mtu atakuwa na uwezo wa kukidhi haja, changamoto na mahitaji ya binadamu wenzake basi hapa tunaweza kusema binadamu huyu atakuwa na thamani kubwa katika jamii.

Binadamu anaweza kuongeza thamani yake kwa kutumia Potentials(vipaji) alivyozaliwa navyo au kwa kutumia elimu na maarifa aliyojifunza katika ulimwengu huu. Wapo watu ambao ni Madaktari, Walimu, Wasanii, wacheza mpira , waandishi, ambao thamani yao ni kubwa sana. Kuna watu katika dunia hii kuingia tu ofisini kwake kwa ajili ya consultation inakubidi ulipe Pesa, hii ni kabla ya kupata huduma unayoihitaji.

SMARTPHONE YAKO

Watu wengi kwa sasa wanamiliki simu janja, lakini tafiti zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya wamiliki wa simu hizi wanazitumia katika , kupiga simu, kuandika meseji, au kuchati na kupost picha katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama, Facebook, Twitter, WhatsApp , Messager, Telegram na mitandao mingine.

Watu wengi hawajagundua siri iliyomo katika simu hizi. Ukiwa na Smartphone ni sawa na kumiliki chuo kikuu katika mikono yako. Maarifa yote yaliyomo katika ulimwengu huu kwa sasa yanapatikana katika simu yako. Ni jukumu la mtu binafsi kuamua kuyatafuta.

Katika sekata ya elimu vyuo vikuu mbalimbali vinafundisha kozi kwa njia ya mtandao kwa kutumia Platforms kama vile Edx, Cousera, Udemy, Udacity na zingine nyingi. Unachopaswa kufanya ni kujisajili kwenye kozi husika kwa kutumia simu yako na kuendelea na masomo mpaka utakapohitimu na kupewa cheti chako. Mimi binafsi nimesoma short courses kadhaa online kwenye vyuo kama Michagani University, Harvard, Oxford na Cambridge.

Lakini katika taaluma ya ualimu kwa sasa ziko Mobile apps nyingi tu ambazo zinatumika kufundishia bila kukutana na wanafunzi. Yaani mwanafunzi anafundishwa na kufanya exercise akiwa nyumbani kwao, mfano wa hizo Apps ni Padlet, Eddpazzle, Google classroom, Hangout, moodle, TED-Ed, Duolingo, Google forms na nyingine nyingi tu.

Katika swala zima la kufanya mikutano au vikao vya kiofisi, sio lazima watu mkutane kwenye chumba cha vikao. Kwa sasa kuna Mobile Apps zinazotumika kufanyia mikutano na vikao, mfano wa Apps hizo ni Zoom, Google meet, Jits na zingine nyingi tu.

Kwa matumizi ya shule zipo pia Mobile Apps ambazo zinatumika kuwasaliana na wazazi wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwatumia maendeleo ya wanafunzi hao , mfano wa Apps hizo ni Remind, Edu blogs, Class Dojo.

Hizi ni Web- based applications.
 
Ulimwengu una uvutano sana hasa kwenye mambo yasiyo na msingi ndio huonekana kuvutia. Ukiwa kinyume unaonekana mshamba.
Inahitaji akili na busara sana kwenye swala la technology.
 
Shukrani kiongozi

Ndo raha ya jf ukiboreka na comment za masafa ya siasa una-tune masafa mengine. akili inatulia kama ulihama kijiwe cha wapiga-story
 
Nini maana ya thamani (value) ya mtu?

Thamani ya mtu ni uwezo alionao katika kutatua matatizo yake binafsi na jamii kwa ujumla , pamoja na uwezo alionao katika swala zima la uzalishaji mali. Kwa mfano kama jamii inakabiliwa na gojwa fulani halafu akatokea mtu akapata tiba ya ugonjwa huo basi mtu huyo atakuwa ameongeza thamani yake katika jamii.

Kwa lugha nyingine , kama mtu atakuwa na uwezo wa kukidhi haja, changamoto na mahitaji ya binadamu wenzake basi hapa tunaweza kusema binadamu huyu atakuwa na thamani kubwa katika jamii.

Binadamu anaweza kuongeza thamani yake kwa kutumia Potentials(vipaji) alivyozaliwa navyo au kwa kutumia elimu na maarifa aliyojifunza katika ulimwengu huu. Wapo watu ambao ni Madaktari, Walimu, Wasanii, wacheza mpira , waandishi, ambao thamani yao ni kubwa sana. Kuna watu katika dunia hii kuingia tu ofisini kwake kwa ajili ya consultation inakubidi ulipe Pesa, hii ni kabla ya kupata huduma unayoihitaji.

SMARTPHONE YAKO

Watu wengi kwa sasa wanamiliki simu janja, lakini tafiti zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya wamiliki wa simu hizi wanazitumia katika , kupiga simu, kuandika meseji, au kuchati na kupost picha katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama, Facebook, Twitter, WhatsApp , Messager, Telegram na mitandao mingine.

Watu wengi hawajagundua siri iliyomo katika simu hizi. Ukiwa na Smartphone ni sawa na kumiliki chuo kikuu katika mikono yako. Maarifa yote yaliyomo katika ulimwengu huu kwa sasa yanapatikana katika simu yako. Ni jukumu la mtu binafsi kuamua kuyatafuta.

Katika sekata ya elimu vyuo vikuu mbalimbali vinafundisha kozi kwa njia ya mtandao kwa kutumia Platforms kama vile Edx, Cousera, Udemy, Udacity na zingine nyingi. Unachopaswa kufanya ni kujisajili kwenye kozi husika kwa kutumia simu yako na kuendelea na masomo mpaka utakapohitimu na kupewa cheti chako. Mimi binafsi nimesoma short courses kadhaa online kwenye vyuo kama Michagani University, Harvard, Oxford na Cambridge.

Lakini katika taaluma ya ualimu kwa sasa ziko Mobile apps nyingi tu ambazo zinatumika kufundishia bila kukutana na wanafunzi. Yaani mwanafunzi anafundishwa na kufanya exercise akiwa nyumbani kwao, mfano wa hizo Apps ni Padlet, Eddpazzle, Google classroom, Hangout, moodle, TED-Ed, Duolingo, Google forms na nyingine nyingi tu.

Katika swala zima la kufanya mikutano au vikao vya kiofisi, sio lazima watu mkutane kwenye chumba cha vikao. Kwa sasa kuna Mobile Apps zinazotumika kufanyia mikutano na vikao, mfano wa Apps hizo ni Zoom, Google meet, Jits na zingine nyingi tu.

Kwa matumizi ya shule zipo pia Mobile Apps ambazo zinatumika kuwasaliana na wazazi wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwatumia maendeleo ya wanafunzi hao , mfano wa Apps hizo ni Remind, Edu blogs, Class Dojo.

Hizi ni Web- based applications.
Mkuu, you are very intelligent.

Thread ya kisomi sana hii mkuu.

Be blessed...!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom