Tumia njia hizi kupata kazi kwa haraka

Ndenji five

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
1,985
3,083
Niamini mimi ndugu kijana mtafuta kazi kumekuwa na tabia mtu kuandika post anatafuta kazi sizani kama mpo mliofanikiwa kwenye hili kama mpo kwenye kumi atapata mmoja

Ipo hivi mtu kukupa kazi kwa maelekezo tu natafuta kazi ni kazi nyingine kwa sababu huyo unayo muomba kazi kwa kuposti humjui hakujui kiundani sasa anakuamini vipi ikiwa hata yeye ana ndugu rafiki jamaa alafu akupe ww ulaji kilaini broo,sister kuwa serious basi

Ni hivi kazi zipo nyingi tena nyingi ila %85 hazitangazwi unaweza kuta unakaa hapo hapo mtaani kwako kuna kazi ila huwezi pata taarifa anakuja kupata taarifa wa mikoa ya mbali wew upo

Nasema haya sababu ni mzoefu wa haya mambo kuna muda nilikuwa hadi nashangaa inakuwaje mtu unakosa kazi mana ilikuwa bandika bandua leo huku kesho kule wenye kazi wananibembeleza

Naongelea kazi sio vibarua
Tumia mbinu hizi zitakusaidia

Connection kama unajijua ww dereva au mwalimu nk jitahidi sana uwe na ukaribu na walio kwenye hizo secta jikombe uwezavyo na ujitanabaishe kwa huyo mtu wako unatafuta kazi itakuwa rahisi kwako

Bakishishi: ukiweza hiko cha kwanza cha pili ni pesa mkono mtupu haurambwi hata kama hujaombwa jitahidi uwe na kasenti kakumpa moyo jamaa

hapa ndipo lengo la kuanzisha mada Fanya maombi ya mizim tafuta mganga mkali akufanyie mandingilingi yaan akukebue japo hiyi mbinu itafanya kazi kwa muda na sio kila tawile anaweza ukiona tawile anaendekeza pesa achana nae huyo tapeli utapigwa na ukiweza hili utafurahi mbona utaenda kuomba kazi na cheti cha kuzaliwa mwajili wako kila akicheki cheti anaona una cv zote kwenye tarehe ya kuzaliwa ataona umesomea chuo cha bora duniani NB sio lazima uamini nimekupa njia wanazotumia wana kubust mambo kama huamini tulia

Funga sali sana omba Mungu ujuavyo funga kwa imani zote afu nenda kaombe kazi

Niishie hapo ukifeli hizi hatua basi nyota yako sio ya kutafuta ajila ila unajilazimisha angalia kipawa chako kifanyie kazi
 
Napata shida sna kukuelewa na hasa point yako ya mizimu

Kuna watu hatuamini ayo mambo

But Things flow sometime with a Passion.

Ila naamini Imani ya Mtu inaweza kumvusha sehemu moja kwenda nyingine.

Ulimwengu una Siri sna
Na hisii mizimu imewaachia laana wanabaki kuhahaha mitaani maisha haya watu hawapo serious kabisa
 
Niishie hapo ukifeli hizi hatua basi nyota yako sio ya kutafuta ajila ila unajilazimisha
Nimekuelewa Sana hapa. Maana yake saa nyingine tunahangaikia kupata visivyo vyetu kumbe mtu umeandikiwa au unatakiwa ufanye kitu kingine kabisa either kutumikia kipaji Fulani au uwezo Fulani uliopewa. Ila Sasa kukijua ni kitu gani ndio mtihani
 
Nimekuelewa Sana hapa. Maana yake saa nyingine tunahangaikia kupata visivyo vyetu kumbe mtu umeandikiwa au unatakiwa ufanye kitu kingine kabisa either kutumikia kipaji Fulani au uwezo Fulani uliopewa. Ila Sasa kukijua ni kitu gani ndio mtihani
Hawajui kama Mungu kila mtu anampa kipawa chake wanataka woote tuwe serikali sijui Selemala watakuwa kina nani
 
Back
Top Bottom