Tumhukumu vipi binti aliyebakwa na kupewa ujauzito akiwa mwanafunzi?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,887
2,000
Ni kweli kuwa siyo jambo zuri kupeleka "wazazi" shule na hakuna mtu anayependa hilo limkute kamwe.

Sisi viongozi makini huwa mambo haya hatuyasemi hadharani kwa kuwa zipo sababu nyingi sana zinazotufanya kutumia busara za "kuuchuna kuhusu jambo hili kama alivyofanya yule bro"

Sababu ya kwanza ni kuwa kuna wasichana wengi sana wanakumbana na matukio ya ubakaji. Huyu aliyebakwa kwa bahati mbaya anakuwa kwanza kaumizwa kisaikoloja na pili anakosa haki yake ya kupata elimu kama anakumbana na ujauzito kutokana na msimamo mwingine ambao hauna maana kuusema hadharani kwa namna ile.

Jambo la pili ni kuwa sisi viongozi makini huwa tunakumbuka kipindi tukiwa katika balehe. Tulitamani, tulifanya na kwa bahati nzuri pengini hatukuharibu "future" za wenzetu kutokana na ufanyaji wetu. Leo hatuna mamlaka ya kurusha mawe kwa kuwa hata kama hatukufanya kwa wale wengine, basi hatukufanya kwa kuwa tulikosa fursa ya kufanya,tulitamani kufanya ili kuuona huo utamu halisi tuliokuwa tunahadihiwa au kuusoma kwenye vitabu, sasa leo tunasema vipi hovyo?

Yesu alipelekewa shitaka la zinaa, kabla hajatoa hukumu aliwaza sana. Aliwaza kwa kuwa alikuwa kiongozi makini, kiongozi makini kama mimi huwa nawaza sana kwa upande wangu kabla sijatoa hukumu.Yesu aliijua zinaa na ukweli wake kutoka ndani,alikasirishwa sana na wale waliopeleka shitaka kwake kwa kuwa aliwaona ni wanafiki. Pamoja na usafi aliokuwa nao Yesu, bado aliona kuwa lipo jambo na binti yule badala ya kuuawa akapewa tena nafasi.

Halafu mimi nilivyo kiongozi makini, huwa siongei mambo mabaya kisha nikaitabiria familia yangu kwa mfano. Hilo ni jambo baya kabisa, litaisononesha familia yangu nitakapolisema kwa namna hiyo.

"Mimi ni kiongozi makini, huwa sisemi hovyo hovyo. Sipendi kweli kusomesha wazazi lakini kabla ya kuhukumu huwa naangalia kwa jicho la ndani, jicho linalonikumbushia kitambo changu na jamii yangu.

Niwasalimu sana wana JF kwa kuwa nilipotea kidogo kutokana na kuwa huko kwenye nchi ambazo kuipataJamii Forum ni tatizo kubwa. Nimelazimika kusoma habari zote kuanzia siku nilipoondoka nchini ili kujua yanayoendelea nchini kwangu kwa kupitia chombo makini na cha uhakika cha habari cha Jamii forum. Ingawa bado sijafika Tanzania ila nipo nchi ambayo inapatikana Jamii forum.

Poleni na mauaji ya wale askari barabarani wa kule Kibiti. Poleni na kauli kama zile, hii pole ni kwa wale viongozi makini pekee!
 

inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
6,315
2,000
akitoka shule na wenzake akarud nyumbani mapema habakwi,akiwa nyumbani anasaidia kazi za jikoni na kujisomea badala ya kuzurura..habakwi
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,050
2,000
Sheria iko wazi Mkuu;

"Awe ameipata kwa kujitakia au kwa bahati mbaya, siko tayari kusomesha wazazi....'. waende VETA au wakajifunze vyerehani"
 

Van Pauser

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
393
500
Hili swali niliwauliza baadhi ya watu ambao nafanya nao kazi lkn majibu ambayo yametoka yan ilkuwa kama tupo kwenye debate kila mtu alikuwa anatetea upande wakee....!!! Mpaka muda huu natafakari lkn cjapata jibu la swali hili.
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,209
2,000
Hapo kama ni mimi.
Huyo mtoto atasimama masomo kabisa hadi atakapokuwa na uwezo wa kuingia darasani bila hayo mambo ya uzazi kuleta sintfahamu kwa wenzake.

Kisha shule anaendelea kwa mlango hata wa elimu ya watu wazima.
Tusikariri kuwa elimu mtu ukianza darasa la kwanza ni linear hadi Chuo bila kona wala pause yoyote katikati.

we are living in agile world.
Ila kuendelea ananyonyesha sijui na yeye apate MATERNITY LEAVE kati kati ya watoto wenzake hilo sijawahi wala siliungi mkono kabisa...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom