Tumhukumu na kumtetea Magufuli kwa haki hadi 2020

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,913
Kila siku naona humu JF kama tunatoka nje kidogo ya mstari tunapotaka kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu hasa kwa kuangalia jinsi John Pombe Magufuli anavyotenda kama Rais wetu. Kwa mujibu wa Katiba yetu, Rais ndiye dira ya taifa na wala si kitu kingine chochote kile. Rais ndiye Mkuu wa nchi na pia Mkuu wa Serikali.

Lakini Magufuli kama Rais wetu ni kweli anakosea kuendesha nchi ama tunaona anakosea kwa kuwa tu tunadhani ni lazima akosee? Au ni kweli kuwa Rais yupo sahihi kwenye kila jambo analolifanya kwa kuwa tu tunaamini kaumbwa kutokukosea? Lazima Magufuli kama Rais wetu apewe haki yake ya kukosolewa ama kushtumiwa kimantiki. Asikosolewe ama kutetewa kwa kuwa tu ni Rais ama kwa kuwa ni mwanachama wa chama chetu ama ni wa chama cha wapinzani wetu.
 
Back
Top Bottom